SoC01 Tanzania mpya lazima iwatunze vijana wake na kuushughulikia ukuaji wa kizazi cha vijana

SoC01 Tanzania mpya lazima iwatunze vijana wake na kuushughulikia ukuaji wa kizazi cha vijana

Stories of Change - 2021 Competition

Jo Africa Tz

Member
Joined
Jul 23, 2019
Posts
10
Reaction score
10
STUDIO.png


DUNIA NI YA NANI?

Dunia ni yenu (vijana), pia ni yetu (wazee), lakini katika uchambuzi wa mwisho, ni yenu. Nyinyi vijana, mkiwa mmejaa hamasa na nguvu, maisha yenu ndio kwanza yanachanua, ni kama jua la saa mbili au tatu ya ahsubuhi. Matumainio yetu (Wazee) yapo juu yenu. Dunia ni yenu. Mustakbali wa Tanzania ni wenu.

WAZEE SAIDIENI VIJANA

Lazima tuwasaidie vijana wetu wafahamu kwamba nchi yetu bado ni masikini sana kwamba hatuwezi kuigeuza hali hii kwa msingi katika muda mfupi, na kwamba kwa bidii za pamoja za vijana wetu na watu wetu wote, wakifanya kazi kwa akili na mikono yao wenyewe, ndio Tanzania itaweza kuwa nchi yenye nguvu na iliyostawi katika muda wa makumi kadhaa ya miaka.

NCHI KONGWE NA MPYA

Kwa sababu ya upungufu wao wa maarifa ya kisiasa na ya kijamii, vijana wengi hawawezi kuona vyema tofauti baina ya Tanzania kongwe na mpya, na si rahisi kwao kuelewa barabara shida nyingi zilizowapata watu wetu katika mapigano ya kujikomboa kutokana na ukandamizi wa serikali yetu.

Ni lazima siku zote tuendeleze elimu ya kisiasa ya hamasa na ifaayo miongoni mwa umma na siku zote lazima tuwaambie ukweli juu ya shida zinazotokea na tujadiliane nao juu ya namna ya kuzishinda shida hizo.

NGUVU YA HARAKATI

Vijana ndio nguvu ya harakati yenye uhai kabisa katika jamii yote. Wao ndio wenye hamu kubwa ya kusoma na wasio na fikra nyingi za kung'ang'ania mambo yalio ya zamani.

Bila ya shaka, vijana lazima wasome kutoka kwa wazee na watu wazima, na wapiganie kama inavyoyumkinika kukubaliwa nao kujishughulisha na mambo yote yenye faida.

Wataalamu mara nyingi huwa wanayaangalia mambo kwa jinsi wanavyoyafikiria wenyewe tu na huwa na ubinafsi, fikra zao huwa haziambatani na hali hasa ya mambo na si imara katika vitendo vyao mpaka wanapojiingiza kwa moyo wao wote katika mapigano ya kimapinduzi ya umma, au wamekata shauri kuyatumikia maslahi ya umma na kuwa kitu kimoja na umma.

KIZAZI CHA VIJANA

Tanzania mpya lazima iwatunze vijana wake na kuushughulikia ukuaji wa kizazi cha vijana. Vijana inawapasa kusoma na kufanya kazi, lakini wamo katika umri wa ukuaji wa kiwiliwili. Kwa hivyo, kazi na masomo yao na pia starehe, michezo na mapumziko yao, yote haya yaangaliwe kwa ukamilifu.

MWANA-MAPINDUZI

Vipi tuamue kama kijana ni mwana-mapinduzi au la? Vipi tunaweza kuwapambanua? Uko mpambanuo mmoja tu, nao ni, kama yuko tayari au la kujichanganyisha na umma mkubwa wa wafanya kazi, wakulima, wajasiriamali au wanasiasa na anafanya hivyo kwa vitendo. Ikiwa yuko tayari kufanya hivyo na anafanya hivyo kwa vitendo, yeye ni mwana-mapinduzi.

MIKONO YA VIJANA

Vijana wasitumike kama mikono ya wazee wapumbavu, wala miguu yao isikimbie kutekeleza maovu ya wazee wao. Wajifunze kutoka kwa wazee na watu wazima na watumie akili katika kujifunza huku. Wakumbuke kuwa hata vichaa nao huzeeka.
_____________
 
Upvote 2
Back
Top Bottom