SoC04 Tanzania mpya yenye matumizi bora ya nishati ya gesi asilia

Tanzania Tuitakayo competition threads

Gentlemen_

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
4,431
Reaction score
13,876

KURASA 1: UTANGULIZI

Maono ya Serikali hivi karibuni yameonyesha ni jinsi gani imepania kufanya mapinduzi ya sekta ya nishati hapa nchini, rejea maagizo ya viongozi wetu wa juu hasa Mheshimiwa Rais
Mwananchi.JPG

Chanzo: Mwananchi

Pia, Rais Samia hakuishia hapo alitoa agizo kwa mheshimiwa Waziri Dkt. Seleman Jafo

Mwananchi - katazo.JPG

Chanzo: Mwananchi
Maoni ya Mdau baada ya agizo hilo:

Mwananchi - Mdau.JPG

Chanzo: Mwananchi

NINI KIFANYIKE?

Nigusie kidogo aina mbili ambazo ningependekeza zitumike kulingana na aina ya mazingira tuliyonayo, ubora wa teknolojia pia utaalamu tulionao kama nchi.

Compressed Natural Gas (CNG)
: Ni gesi ambayo haina harufu kali, haina ladha na haina sumu, gesi hii imeundwa na takribani asilimia 90% ya methane, naitrojeni, karbondayoksaidi, propeni na viambata vidogo mno vya etheni. Inatambulika kwa ubora wake wa kutunza mazingira kutokana na hilo basi inatambulika kuwa best alternative fuel type.

LNG fuel au Liquefied Natural Gas (LNG): Ni gesi asilia ambayo imebadilishwa kwenda kwenye hali ya kimiminika (Liquefied) baada ya kupitia mchakato maalumu wa Liquefaction. Katika mchakato huo gesi asilia inapoozwa kwenda katika viwango vidogo vya hali joto mpaka pale gesi hiyo kubadirika na kuwa kimiminika na uwingi wa gesi unashushwa kwa karibu mara mia sita!

Ikumbukwe LNG haina viambata vya sumu vya kuharibu (non-toxic & corrosive) pia LNG ikiwa imebanwa (compressed) ina uwiano wa 1/600 ukilinganisha na gesi asilia kabla haijafanyiwa mchakato, hali hii inafanya iwe gharama nafuu pia utunzaji wake kuwa rahisi na usafirishaji wake kuwa rafiki.

CNG na LNG ni sawa kwa kila kitu kasoro usafirishaji na utunzaji wake, pia uandaaji wa LNG ni gharama zaidi kulinganisha na CNG.

Kuielezea kwa ukubwa hatutamaliza leo, ingawa kitu cha msingi ni kukumbusha kuwa CNG ni rahisi kuiongeza (refuel) kuliko LNG ambayo inahitaji utaalamu na vifaa bora. Pia LNG inaweza kubadirishwa na kuwa CNG.

Inafahamika katika nchi zilizoendelea wanapenda kutumia LNG katika magari yao hasa ya mizigo/masafa marefu kutokana na uzito wa nguvu unaoweza kulinganishwa na dizeli.
MAPENDEKEZO

1. Kuundwa/Kuboreshwa kwa tume/chombo cha kusimamia gesi asilia

Tume hii itatumika kuratibu, kuendesha na kusimamia shughuli zote za ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa nishati hii kutoka sehemu A kwenda sehemu B kwa ubora na usalama wa hali ya juu.

2. Kupanga gesi asilia katika matumizi ya makundi makuu matatu

Kundi A: Majumbani na maeneo ya biashara ya kipato cha chini;

Kundi B: Viwandani, Mashuleni, Mahospitalini Mahotelini n.k;

Kundi C: Stesheni za nishati na Karakana za Magari.

Alternative Fuels Data Center.jpg

Chanzo: Alternative Fuels Data Center

3. Kuandaa magari maalumu ya kusambaza gesi

Gari hizi zitatengenezwa au kuagizwa kwa matakwa maalumu ya nchi (Special Order)

slideserve.jpg

Chanzo: Slideserve

Screenshot_23-5-2024_142253_www.google.co.tz.jpeg

Chanzo: OpenPR
Gari hizi zitasambaza kwa njia mbili kama ifuatavyo:-
A - Kuacha Tenki katika eneo maalumu

Screenshot_23-5-2024_142555_www.google.co.tz.jpeg

Chanzo: Auyan company

B - Kujaza (Re-filling) gesi kama vile gari za maji inavyojaza katika matenki ya watumiaji mitaani.

Tianjin Sinogas.jpg

Chanzo: Tianjin Sino Gas

4. Rasilimali watu makini

Hapa nashauri Serikali kuwekeza katika wataalamu wapya na kuwatumia vizuri wataalamu waliopo. Huu mradi unapaswa kusimamiwa na watu walio na uzoefu, “exposure” na uzalendo wa hali ya juu.

Katika uchambuzi wa rasilimali watu hao pia kuwepo na timu maalumu ya ukaguzi ndani ya chombo husika hasa kuhakikisha swala zima la Usalama wa mifumo, matenki na matumizi ya nishati hii, ili kuepusha na majanga ambayo yanaweza kuepukika.

KURASA 2: JINSI MFUMO UTAKAVYOFANYA KAZI

1. Usalama:

Jambo la kwanza ni kuhakikisha mfumo huu ni salama kwa watumiaji wake, nimependekeza uchimbiwaji wa matenki ya gesi chini ya ardhi kwa urefu utakaonekana unafaa ft 6+ kulingana na ukubwa wa tenki. Kwanini?
  • Jua halitaathiri kwa kuongeza joto katika tenki hili
  • Mvua na hali zote za hewa hazitaathiri tenki hili
  • Halitafikiwa na vitu vya kuweza kulidhuru kirahisi mfano MOTO
  • Ni salama kwa watoto na watu mbalimbali wenye changamoto za akili n.k
  • Ni salama endapo kutatokea changamoto ya kuripuka.
Angalizo: Mfumo huu utakuwa na uwezo wa kubaini na kuzuia hali mbalimbali za hatari mfano ‘ gas leakage ‘ , itakuwa na mfumo wa kuhisi joto kupitiliza hivyo koki kuu itajizima na kutuma taarifa kwa msimamizi (operator) mkuu wa hilo tenki. Mambo ni mengi nimeandaa MANUAL kuhusu mfumo huu.. naomba tuendelee mbele.

Shandong luen auto 2.jpg

Chanzo: Shandong Luen Auto

2. Mfumo wa malipo na kuanzisha huduma (Activation Scheme):

a. Tokeni maalumu:
Itaandaliwa system itakayoweza kupokea tokeni ili kuanzisha huduma ya gesi hiyo kwa kiwango fulani kulingana na tokeni husika kutoka katika tenki hilo lililopandikizwa ardhini, hili tenki linakuwa limewekwa na tume bila maombi ya moja kwa moja kutoka kwa mwananchi;

b. Bando kwa Kilogramu:
Gesi hii pia itajazwa kulingana na manunuzi ya mteja husika, ambapo itategemea na kilogramu ngapi kanunua zikiisha basi itahitajika gari lije kujaza upya, hili tenki linakuwa ni la mwananchi ambae ataamua alitumie kwa muda gani bila kuathiri usalama wake na watu wengine;

c. Jamii husika kuchangia gharama na kutumia kwa pamoja:
Hii inafaa hasa katika miji mipya ambapo tume itaweka ujenzi wa stesheni ya gesi asilia ambapo mifumo ya usambazaji itafanyika kutoka katika stesheni hiyo kwenda katika nyumba za jamii hiyo itakayoamua kujiunga kwa njia hiyo. Huduma hii inapendeza katika kota au nyumba zilizopangwa kimpangilio maalumu.

Hii stesheni inakuwa ni mali ya tume, na bili za matumizi zitakuwa zinatumwa kwa jamii hiyo ambayo italipa kwa pamoja, ingawa kutawekwa pia mita ndogo ndogo kubaini na kugundua ni Kaya, Familia ipi iliyotumia gesi nyingi zaidi hivyo kulipa maradufu kulingana na matumizi yake.

Natural Gas.jpg

Chanzo: Natural Gas

KURASA 3: MATOKEO CHANYA

1- Utunzaji bora wa Mazingira
2- Kukuza uchumi

3- Kwenda sambamba na kasi ya sayansi na teknolojia
4- Kuchochea uvumbuzi na ubunifu zaidi

5- Chachu ya ajira kwa Watanzania
6- Gharama za maisha kupungua

NAWASILISHA
 
Upvote 11

Nimeipenda hii, unajua Ulaya walishafanyaga zamaaaaaani kisa tu wao wanaitumia hadi kuchemshia nyumba zao.

Sema wasiwasi wangu tu ni 'maintenance' hapo ndipo mtiti ulipo. Nauliza je, kwa hali hii ya sasa ambapo mtaani kuna bomba nyingi tu zinavujisha maji zimepasuka na hazijarekebishwa kwa wakati. Vipi itakuwa kwa hayo mabomba ya gesi????.

Huduma hii inapendeza katika kota au nyumba zilizopangwa kimpangilio maalumu.
KWa kweli, ni katika maeneo ya kisasa zaidi. Hawa wengine asee tuwaache wanunue mitungi midogomidogo.

NAWASILISHA
Ahsante tumepokea🙏
 
KURASA 1: UTANGULIZI

Maono ya Serikali hivi karibuni yameonyesha ni jinsi gani imepania kufanya mapinduzi ya sekta ya nishati hapa nchini, rejea maagizo ya viongozi wetu wa juu hasa Mheshimiwa Rais
View attachment 2998022
Chanzo: Mwananchi

Pia, Rais Samia hakuishia hapo alitoa agizo kwa mheshimiwa Waziri Dkt. Seleman Jafo

View attachment 2998024
Chanzo: Mwananchi
Maoni ya Mdau baada ya agizo hilo:

View attachment 2998025
Chanzo: Mwananchi

NINI KIFANYIKE?

Nigusie kidogo aina mbili ambazo ningependekeza zitumike kulingana na aina ya mazingira tuliyonayo, ubora wa teknolojia pia utaalamu tulionao kama nchi.

Compressed Natural Gas (CNG)
: Ni gesi ambayo haina harufu kali, haina ladha na haina sumu, gesi hii imeundwa ka takribani asilimia 90% ya methane, naitrojeni, karbondayoksaidi, propeni na viambata vidogo mno vya etheni. Inatambulika kwa ubora wake wa kutunza mazingira kutokana na hilo basi inatambulika kuwa best alternative fuel type.

LNG fuel au Liquefied Natural Gas (LNG): Ni gesi asilia ambayo imebadirishwa kwenda kwenye hali ya kimiminika (Liquefied) baada ya kupitia mchakato maalumu wa Liquefaction. Katika mchakato huo gesi asilia inapoozwa kwenda katika viwango vidogo vya hali joto mpaka pale gesi hiyo kubadirika na kuwa kimiminika na uwingi wa gesi unashushwa kwa karibu mara mia sita!

Ikumbukwe LNG haina viambata vya sumu vya kuharibu (non-toxic & corrosive) pia LNG ikiwa imebanwa (compressed) ina uwiano wa 1/600 ukilinganisha na gesi asilia kabla haijafanyiwa mchakato, hali hii inafanya iwe gharama nafuu pia utunzaji wake kuwa rahisi na usafirishaji wake kuwa rafiki.

CNG na LNG ni sawa kwa kila kitu kasoro usafirishaji na utunzaji wake, pia uandaaji wa LNG ni gharama zaidi kulinganisha na CNG.

Kuielezea kwa ukubwa hatutamaliza leo, ingawa kitu cha msingi ni kukumbusha kuwa CNG ni rahisi kuiongeza (refuel) kuliko LNG ambayo inahitaji utaalamu na vifaa bora. Pia LNG inaweza kubadirishwa na kuwa CNG.

Inafahamika katika nchi zilizoendelea wanapenda kutumia LNG katika magari yao hasa ya mizigo/masafa marefu kutokana na uzito wa nguvu unaoweza kulinganishwa na dizeli.
MAPENDEKEZO

1. Kuundwa/Kuboreshwa kwa tume/chombo cha kusimamia gesi asilia

Tume hii itatumika kuratibu, kuendesha na kusimamia shughuli zote za ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa nishati hii kutoka sehemu A kwenda sehemu B kwa ubora na usalama wa hali ya juu.

2. Kupanga gesi asilia katika matumizi ya makundi makuu matatu

Kundi A: Majumbani na maeneo ya biashara ya kipato cha chini;

Kundi B: Viwandani, Mashuleni, Mahospitalini Mahotelini n.k;

Kundi C: Stesheni za nishati na Karakana za Magari.

View attachment 2998030
Chanzo: Alternative Fuels Data Center

3. Kuandaa magari maalumu ya kusambaza gesi

Gari hizi zitatengenezwa au kuagizwa kwa matakwa maalumu ya nchi (Special Order)

View attachment 2998034
Chanzo: Slideserve

View attachment 2998037

Chanzo: OpenPR
Gari hizi zitasambaza kwa njia mbili kama ifuatavyo:-
A - Kuacha Tenki katika eneo maalumu

View attachment 2998038
Chanzo: Auyan company

B - Kujaza (Re-filling) gesi kama vile gari za maji inavyojaza katika matenki ya watumiaji mitaani.

View attachment 2998041
Chanzo: Tianjin Sino Gas

4. Rasilimali watu makini

Hapa nashauri Serikali kuwekeza katika wataalamu wapya na kuwatumia vizuri wataalamu waliopo. Huu mradi unapaswa kusimamiwa na watu walio na uzoefu, “exposure” na uzalendo wa hali ya juu.

Katika uchambuzi wa rasilimali watu hao pia kuwepo na timu maalumu ya ukaguzi ndani ya chombo husika hasa kuhakikisha swala zima la Usalama wa mifumo, matenki na matumizi ya nishati hii, ili kuepusha na majanga ambayo yanaweza kuepukika.

KURASA 2: JINSI MFUMO UTAKAVYOFANYA KAZI

1. Usalama:

Jambo la kwanza ni kuhakikisha mfumo huu ni salama kwa watumiaji wake, nimependekeza uchimbiwaji wa matenki ya gesi chini ya ardhi kwa urefu utakaonekana unafaa ft 6+ kulingana na ukubwa wa tenki. Kwanini?
  • Jua halitaathiri kwa kuongeza joto katika tenki hili
  • Mvua na hali zote za hewa hazitaathiri tenki hili
  • Halitafikiwa na vitu vya kuweza kulidhuru kirahisi mfano MOTO
  • Ni salama kwa watoto na watu mbalimbali wenye changamoto za akili n.k
  • Ni salama endapo kutatokea changamoto ya kuripuka.
Angalizo: Mfumo huu utakuwa na uwezo wa kubaini na kuzuia hali mbalimbali za hatari mfano ‘ gas leakage ‘ , itakuwa na mfumo wa kuhisi joto kupitiliza hivyo koki kuu itajizima na kutuma taarifa kwa msimamizi (operator) mkuu wa hilo tenki. Mambo ni mengi nimeandaa MANUAL kuhusu mfumo huu.. naomba tuendelee mbele.

View attachment 2998047
Chanzo: Shandong Luen Auto

2. Mfumo wa malipo na kuanzisha huduma (Activation Scheme):

a. Tokeni maalumu:
Itaandaliwa system itakayoweza kupokea tokeni ili kuanzisha huduma ya gesi hiyo kwa kiwango fulani kulingana na tokeni husika kutoka katika tenki hilo lililopandikizwa ardhini, hili tenki linakuwa limewekwa na tume bila maombi ya moja kwa moja kutoka kwa mwananchi;

b. Bando kwa Kilogramu:
Gesi hii pia itajazwa kulingana na manunuzi ya mteja husika, ambapo itategemea na kilogramu ngapi kanunua zikiisha basi itahitajika gari lije kujaza upya, hili tenki linakuwa ni la mwananchi ambae ataamua alitumie kwa muda gani bila kuathiri usalama wake na watu wengine;

c. Jamii husika kuchangia gharama na kutumia kwa pamoja:
Hii inafaa hasa katika miji mipya ambapo tume itaweka ujenzi wa stesheni ya gesi asilia ambapo mifumo ya usambazaji itafanyika kutoka katika stesheni hiyo kwenda katika nyumba za jamii hiyo itakayoamua kujiunga kwa njia hiyo. Huduma hii inapendeza katika kota au nyumba zilizopangwa kimpangilio maalumu.

Hii stesheni inakuwa ni mali ya tume, na bili za matumizi zitakuwa zinatumwa kwa jamii hiyo ambayo italipa kwa pamoja, ingawa kutawekwa pia mita ndogo ndogo kubaini na kugundua ni Kaya, Familia ipi iliyotumia gesi nyingi zaidi hivyo kulipa maradufu kulingana na matumizi yake.

View attachment 2998049
Chanzo: Natural Gas

KURASA 3: MATOKEO CHANYA

1- Utunzaji bora wa Mazingira
2- Kukuza uchumi

3- Kwenda sambamba na kasi ya sayansi na teknolojia
4- Kuchochea uvumbuzi na ubunifu zaidi

5- Chachu ya ajira kwa Watanzania
6- Gharama za maisha kupungua

NAWASILISHA
Kijana naona umepania kubeba hela za JF..

Swali langu je Nchi ina uwezo wa kutimiza hayo hasa kifedha.. (Bajeti)?
 
Sema wasiwasi wangu tu ni 'maintenance' hapo ndipo mtiti ulipo. Nauliza je, kwa hali hii ya sasa ambapo mtaani kuna bomba nyingi tu zinavujisha maji zimepasuka na hazijarekebishwa kwa wakati. Vipi itakuwa kwa hayo mabomba ya gesi????.

Ahsante sana... kwa mchango wako na swali zuri.

Ukisoma vizuri kuna kipengele cha RASILIMALI WATU ambapo niliandika hivi:

"Katika uchambuzi wa rasilimali watu hao pia kuwepo na timu maalumu ya ukaguzi ndani ya chombo husika hasa kuhakikisha swala zima la Usalama wa mifumo, matenki na matumizi ya nishati hii, ili kuepusha na majanga ambayo yanaweza kuepukika"

Nilifikiria hiyo changamoto mwanzo pia nilitoa pendekezo la kuwa na TUME ambayo itakuwa serious na hili swala.
 
Kijana naona umepania kubeba hela za JF..

Swali langu je Nchi ina uwezo wa kutimiza hayo hasa kifedha.. (Bajeti)?
Hapana.. sijapania nina mawazo tu mengi.. nikitulia nakuja na BANDIKO jingine... stay tune.

Kuhusu swala la bajeti. Dunia ya sasa imebadirika sana.. nchi nyingi zinaingia ubia ambao utanufaisha pande zote.

Ndio maana Mheshimiwa Rais anakwenda huku na huko kutafuta wawekezaji nchini.. moja ya sehemu ya kuwekeza ni hapa katika GESI ASILIA au NISHATI kwa ujumla.

Pia serikali ina mtindo wa kuweka vipaumbele.. hili jambo likiwa ni kipaumbele basi litafanikiwa kwa haraka sana.. nchi inajiweza.
 
Inafahamika katika nchi zilizoendelea wanapenda kutumia LNG katika magari yao hasa ya mizigo/masafa marefu kutokana na uzito wa nguvu unaoweza kulinganishwa na dizeli.
Nadhani unamaanisha CNG na sio LNG..., Ni kwamba gesi asilia ni gesi (methane) na kama gesi nyingine gesi ina mtindo wa kuchukua eneo kubwa sana (Volume) sasa ukiweza kuigandamiza hio gesi na mpaka kuwa kimiminika unahitaji pressure kubwa sana na ukifanya hivyo utakuwa umeweka gesi nyingi sana kwenye eneo dogo....; chukulia hii equation.....

PV = nRT, where P is the pressure of the gas, V is its volume, n is the number of moles of the gas, T is its kelvin temperature, and R is the ideal (universal) gas constant

Ukipunguza Temperature pia hauhitaji pressure kubwa..., Propane ambayo ndio gesi ya majumbani inachukua pressure ndogo sana at room temperature kuwa kimiminika kuliko Gesi asilia..., kwahio kupata ujazo uleule wa propane utahitaji mitungi imara zaidi, pressure kubwa zaidi na ku maintain ubaridi (hizi zote ni nishati)...

Ndio maana wanaobadilisha kuwa LNG wanafanya hivyo na kuweka gesi hii kwenye matanker makubwa kwenye maintained temperature na kuyapeleka kwenye uhitaji wa nishati ili ikifika huko wairudishe katika gesi asilia na itumike huko...

Kwa sisi matumizi ya ndani hatuhitaji kuibadilisha kuwa LNG na cheapest way ingekuwa ni kuipeleka directly kwenye mabomba kama maji mpaka kwenye matumizi yake (na tufanye hivyo kuipeleka kwenye masheli) ingawa majumbani miundo mbinu itakuwa gharama.....
 
Nadhani unamaanisha CNG na sio LNG...,
LNG ref.JPG

Ahsante kwa mchango wako Mkuu...., tafadhali pitia hapo... nilikuwa namaanisha LNG na si CNG ndio maana mwisho kabisa nikasema LNG wanaitumia kama substitute ya DIESEL.

CNG inatumika pia hasa katika magari madogo.. huko ndio unakutana na nishati zingine kama vile LPG hasa ktk magari ambayo ni hybrid.. etc etc...

Karibu.
 
View attachment 2998427

Hii LNG inafaa tu kama unapeleka nishati nchi ambazo hazina nishati kwa matumizi ya ndani kuna better option yaani hata ku-maintain ibaki katika liquid form kwenye pressure practical unahitaji temperature ndogo kwenye -83 au zaidi ya hapo

The common characteristic of LNG Storage tanks is the ability to store LNG at the very low temperature of -162 °C (-260 °F). LNG storage tanks have double containers, where the inner contains LNG and the outer container contains insulation materials.

sasa utaona practicability ya hili jambo ni non starter and there are better options kwenye magari
 
Well, refer maelezo yangu ktk hili bandiko..

Kuna sehemu niliandika kuwa LNG inaweza kuwa compressed na kupata ratio ya 1/600.

Point ya pili ni kwamba ndani ya LNG unaweza pata CNG kuna procedures za kufanya uipate CNG.

so tunakuja kuona kuwa LNG kama tatizo si gharama na utaalamu wa kuichakata basi ni best option so far..

CNG ni light compared to LNG kwa matumizi ya majumbani (kupikia) ipo more recommended...

Main point ni kujua GAS ipi utaitumia wapi.. that's it..

Ukipitia vzr bandiko nimegawanya aina ya Matumizi ya GAS hizi...

Karibu...
 
Mkuu LNG ni Natural Gas ambayo imekuwa compresed hadi kuwa kimiminika (kwahio in short LNG, CNG, Biogas zote hizo ni Methane ... CNG ni kwamba imekuwa compressed kidogo na LNG imekuwa compressed under higher pressure na lower temperature mpaka kuwa Liquid (Kimiminika) kwahio ukiondoa ile pressure / temperature LNG itarudia kuwa gesi sababu naturally ni gesi...

Ni kama tu ilivyo mitungi ya gesi majumbani ile ni propane imekuwa compressed na kuwa LPG Liquid Petroleum Gas..., tofauti ni kwamba its easier kwa propane kubadilika na kuwa Kimiminika kuliko natural gas i.e. methane....

Na compression inafanyika ili kuweza kusafirisha / kutunza more in less space
 
Back
Top Bottom