Gentlemen_
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 4,431
- 13,876
KURASA 1: UTANGULIZI
Maono ya Serikali hivi karibuni yameonyesha ni jinsi gani imepania kufanya mapinduzi ya sekta ya nishati hapa nchini, rejea maagizo ya viongozi wetu wa juu hasa Mheshimiwa RaisChanzo: Mwananchi
Pia, Rais Samia hakuishia hapo alitoa agizo kwa mheshimiwa Waziri Dkt. Seleman Jafo
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
NINI KIFANYIKE?
Nigusie kidogo aina mbili ambazo ningependekeza zitumike kulingana na aina ya mazingira tuliyonayo, ubora wa teknolojia pia utaalamu tulionao kama nchi.Compressed Natural Gas (CNG): Ni gesi ambayo haina harufu kali, haina ladha na haina sumu, gesi hii imeundwa na takribani asilimia 90% ya methane, naitrojeni, karbondayoksaidi, propeni na viambata vidogo mno vya etheni. Inatambulika kwa ubora wake wa kutunza mazingira kutokana na hilo basi inatambulika kuwa best alternative fuel type.
LNG fuel au Liquefied Natural Gas (LNG): Ni gesi asilia ambayo imebadilishwa kwenda kwenye hali ya kimiminika (Liquefied) baada ya kupitia mchakato maalumu wa Liquefaction. Katika mchakato huo gesi asilia inapoozwa kwenda katika viwango vidogo vya hali joto mpaka pale gesi hiyo kubadirika na kuwa kimiminika na uwingi wa gesi unashushwa kwa karibu mara mia sita!
Ikumbukwe LNG haina viambata vya sumu vya kuharibu (non-toxic & corrosive) pia LNG ikiwa imebanwa (compressed) ina uwiano wa 1/600 ukilinganisha na gesi asilia kabla haijafanyiwa mchakato, hali hii inafanya iwe gharama nafuu pia utunzaji wake kuwa rahisi na usafirishaji wake kuwa rafiki.
CNG na LNG ni sawa kwa kila kitu kasoro usafirishaji na utunzaji wake, pia uandaaji wa LNG ni gharama zaidi kulinganisha na CNG.
Kuielezea kwa ukubwa hatutamaliza leo, ingawa kitu cha msingi ni kukumbusha kuwa CNG ni rahisi kuiongeza (refuel) kuliko LNG ambayo inahitaji utaalamu na vifaa bora. Pia LNG inaweza kubadirishwa na kuwa CNG.
Inafahamika katika nchi zilizoendelea wanapenda kutumia LNG katika magari yao hasa ya mizigo/masafa marefu kutokana na uzito wa nguvu unaoweza kulinganishwa na dizeli.
MAPENDEKEZO1. Kuundwa/Kuboreshwa kwa tume/chombo cha kusimamia gesi asilia
Tume hii itatumika kuratibu, kuendesha na kusimamia shughuli zote za ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa nishati hii kutoka sehemu A kwenda sehemu B kwa ubora na usalama wa hali ya juu.2. Kupanga gesi asilia katika matumizi ya makundi makuu matatu
Kundi A: Majumbani na maeneo ya biashara ya kipato cha chini;Kundi B: Viwandani, Mashuleni, Mahospitalini Mahotelini n.k;
Kundi C: Stesheni za nishati na Karakana za Magari.
Chanzo: Alternative Fuels Data Center
3. Kuandaa magari maalumu ya kusambaza gesi
Gari hizi zitatengenezwa au kuagizwa kwa matakwa maalumu ya nchi (Special Order)Chanzo: Slideserve
Chanzo: OpenPR
A - Kuacha Tenki katika eneo maalumu
Chanzo: Auyan company
B - Kujaza (Re-filling) gesi kama vile gari za maji inavyojaza katika matenki ya watumiaji mitaani.
Chanzo: Tianjin Sino Gas
4. Rasilimali watu makini
Hapa nashauri Serikali kuwekeza katika wataalamu wapya na kuwatumia vizuri wataalamu waliopo. Huu mradi unapaswa kusimamiwa na watu walio na uzoefu, “exposure” na uzalendo wa hali ya juu.Katika uchambuzi wa rasilimali watu hao pia kuwepo na timu maalumu ya ukaguzi ndani ya chombo husika hasa kuhakikisha swala zima la Usalama wa mifumo, matenki na matumizi ya nishati hii, ili kuepusha na majanga ambayo yanaweza kuepukika.
KURASA 2: JINSI MFUMO UTAKAVYOFANYA KAZI
1. Usalama:
Jambo la kwanza ni kuhakikisha mfumo huu ni salama kwa watumiaji wake, nimependekeza uchimbiwaji wa matenki ya gesi chini ya ardhi kwa urefu utakaonekana unafaa ft 6+ kulingana na ukubwa wa tenki. Kwanini?- Jua halitaathiri kwa kuongeza joto katika tenki hili
- Mvua na hali zote za hewa hazitaathiri tenki hili
- Halitafikiwa na vitu vya kuweza kulidhuru kirahisi mfano MOTO
- Ni salama kwa watoto na watu mbalimbali wenye changamoto za akili n.k
- Ni salama endapo kutatokea changamoto ya kuripuka.
Chanzo: Shandong Luen Auto
2. Mfumo wa malipo na kuanzisha huduma (Activation Scheme):
a. Tokeni maalumu:Itaandaliwa system itakayoweza kupokea tokeni ili kuanzisha huduma ya gesi hiyo kwa kiwango fulani kulingana na tokeni husika kutoka katika tenki hilo lililopandikizwa ardhini, hili tenki linakuwa limewekwa na tume bila maombi ya moja kwa moja kutoka kwa mwananchi;
b. Bando kwa Kilogramu:
Gesi hii pia itajazwa kulingana na manunuzi ya mteja husika, ambapo itategemea na kilogramu ngapi kanunua zikiisha basi itahitajika gari lije kujaza upya, hili tenki linakuwa ni la mwananchi ambae ataamua alitumie kwa muda gani bila kuathiri usalama wake na watu wengine;
c. Jamii husika kuchangia gharama na kutumia kwa pamoja:
Hii inafaa hasa katika miji mipya ambapo tume itaweka ujenzi wa stesheni ya gesi asilia ambapo mifumo ya usambazaji itafanyika kutoka katika stesheni hiyo kwenda katika nyumba za jamii hiyo itakayoamua kujiunga kwa njia hiyo. Huduma hii inapendeza katika kota au nyumba zilizopangwa kimpangilio maalumu.
Hii stesheni inakuwa ni mali ya tume, na bili za matumizi zitakuwa zinatumwa kwa jamii hiyo ambayo italipa kwa pamoja, ingawa kutawekwa pia mita ndogo ndogo kubaini na kugundua ni Kaya, Familia ipi iliyotumia gesi nyingi zaidi hivyo kulipa maradufu kulingana na matumizi yake.
Chanzo: Natural Gas
KURASA 3: MATOKEO CHANYA
1- Utunzaji bora wa Mazingira2- Kukuza uchumi
3- Kwenda sambamba na kasi ya sayansi na teknolojia
4- Kuchochea uvumbuzi na ubunifu zaidi
5- Chachu ya ajira kwa Watanzania
6- Gharama za maisha kupungua
NAWASILISHA
Upvote
11