Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani kama TRA Dodoma unaenda ofisini kwao kulipa kodi wanajizungusha wee hadi ugombane nao ndio wanaanza kushughulikia suala lako.Mtu anatakiwa alipe Kodi akiwa amelala sio kwenda kupanga foleni na ujinga wa control number
Hapana Mkuu, ukitaka kwenda kulipa kodi TRA au kupata leseni ya biashara Halmashauri, kama ni mfanyakazi omba kabisa ruhusa kazini. Maana inachukua Siku 1 au 2 kushughulikia masuala hayo.Hata kuwe na mfumo gani bila kujituma na kuwajibika vema TRA itachukiwa siku zote. Watanzania tumezoea kufanya vitu siku ya deadline na hilo ndio linawagharimu watu sana
Unapitia njia gani kuipata mwenyewe?Control number unaweza toa mwenyewe mbona.
Kwani Mwigulu Mchemba na Mama Samia hawajaliona hilo tatizo.?Hapana Mkuu, ukitaka kwenda kulipa kodi TRA au kupata leseni ya biashara Halmashauri, kama ni mfanyakazi omba kabisa ruhusa kazini. Maana inachukua Siku 1 au 2 kushughulikia masuala hayo.
System yao ni mbovu na nahisi hawaitengenezi ili waendelee kupiga hela za faini kwa kuchelewesha kufanya returns za mwezi. Brela nao system yao ya annual fee payment ni majanga matupuuNimesoma quote ya mtu mmoja hapa jf, imenifurahisha sana. Ni kuhusu sakata la Diamond na TRA. Ni ukweli usiopingika mfumo wa ulipaji Kodi Tanzania bado ni changamoto. Hii efilling system ina watesa sana watu. Nashauri TRA wakae chini walitafakari hili, na kuja na mfumo rahisi na wezeshi kwa kulipa Kodi
Nawasilisha