π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” 𝗑𝗔 π—”π—‘π—šπ—’π—Ÿπ—” π—­π—”π—¦π—”π—œπ—‘π—œ π— π—”π—žπ—¨π—•π—”π—Ÿπ—œπ—”π—‘π—’ π— π—”π—‘π—‘π—˜ 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—œπ— π—”π—₯π—œπ—¦π—›π—” π—¨π—¦π—›π—œπ—₯π—œπ—žπ—œπ—”π—‘π—’

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” 𝗑𝗔 π—”π—‘π—šπ—’π—Ÿπ—” π—­π—”π—¦π—”π—œπ—‘π—œ π— π—”π—žπ—¨π—•π—”π—Ÿπ—œπ—”π—‘π—’ π— π—”π—‘π—‘π—˜ 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—œπ— π—”π—₯π—œπ—¦π—›π—” π—¨π—¦π—›π—œπ—₯π—œπ—žπ—œπ—”π—‘π—’

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola zimesaini mikataba na Hati za Makubaliano manne ya ushirikiano katika sekta za sheria na haki, usafiri wa anga, teknolojia ya habari na mawasiliano, pamoja na sayansi ya vipimo. Utiaji saini huo umefanyika wakati wa Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Angola, Mhe. JoΓ£o Manuel GonΓ§alves LourenΓ§o, nchini Tanzania, tarehe 29 na 30 Oktoba 2026.

Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kupanua ushirikiano katika sekta muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi, kuimarisha taasisi na kukuza mahusiano kati ya wananchi wa Tanzania na Angola.

Mkataba wa Uhamishaji wa Wafungwa Waliotiwa Hatiani unaweka utaratibu wa kuhamisha wafungwa wanaokidhi vigezo kutoka nchi moja kwenda nyingine, kwa kuzingatia masharti ya mkataba huo na taratibu za sheria zinazotumika. Ushirikiano huo unalenga kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo katika masuala ya haki jinai.

Kwa upande wa usafiri wa anga, Mkataba wa Huduma za Usafiri wa Anga kati ya Nchi hizo (BASA) unaweka msingi wa ushirikiano katika sekta hiyo, kwa lengo la kuboresha muunganiko wa usafiri wa anga na kutoa fursa zaidi za kukuza biashara, utalii, uwekezaji na shughuli nyingine za kiuchumi.

Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inalenga kukuza ubadilishanaji wa maarifa na utaalamu, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika maendeleo ya teknolojia za kidijitali.

Aidha, Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Sayansi ya Vipimo inaweka msingi wa ushirikiano katika masuala ya upimaji, viwango vya vipimo na maeneo mengine ya kitaalamu yanayohusiana na sayansi hiyo.

Kwa upande wa Tanzania, mikataba na Hati hizo za Makubaliano zimesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Benedict Chang’a.

Kwa upande wa Angola, zilizosainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. TΓ©te AntΓ³nio, Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika, Mashariki ya Kati na Mashirika ya Kikanda, Balozi Jorge Catarino Cardoso, pamoja na Mhe. Mario Augusto da Silva Oliveira.

Utiaji saini wa mikataba na Hati hizo za Makubaliano unaonesha dhamira ya Tanzania na Angola ya kuendeleza vipaumbele vya pamoja vya maendeleo, kupanua maeneo ya ushirikiano na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
 
Attachments

  • Tanzania, Angola Sign Four Agreements to Strengthen Bilateral CooperationThe United Republic o...jpg
    Tanzania, Angola Sign Four Agreements to Strengthen Bilateral CooperationThe United Republic o...jpg
    1 MB · Views: 2

    1 MB · Views: 1

    969.2 KB · Views: 1

    941.1 KB · Views: 1

    1.1 MB · Views: 1

  • Tanzania, Angola Sign Four Agreements to Strengthen Bilateral CooperationThe United Republic of .jpg
    Tanzania, Angola Sign Four Agreements to Strengthen Bilateral CooperationThe United Republic of .jpg
    903 KB · Views: 1
Back
Top Bottom