Kuna video, Watanzania wanachekelea na kuisambaza kwenye mitandao ya mdada anayesemekana ni Mkenya aliyetelekezwa na wenzake baada ya kuonekana na dalili za Corona. Nawashangaa sana Watanzania wanaojifanya kutokujua nini kinaendelea.
Leo hii Tanzania na Burundi ukanda huu ndio wanapima watu wachache sana kwa siku, hii imepelekea wao kuonekana kana kwamba kirusi cha Corona hakipo sana kwao, ukizingatia pia haya mataifa mawili ndio bado hayajafunga mipaka na mpaka sasa kwao kila kitu ruksa, hamna tahadhari wala nini, full mibanano kwenye madaladala na kote kote.
Hata juzi mwanahabari nguli na mwana JF ndugu
Pascal Mayalla alianzisha uzi unaomtaja rais Magufuli kama nabii kisa kuna Mkenya kaandika kumsifia huyo rais wao kwa kutofunga mipaka wala kubana chochote au mizunguko ya watu, ambapo inategemewa rais Uhuru aige pia kwa kulegeza.
Mataifa mengine yanayopima watu wengi ili kupata uhalsia wa hali ilivyo mtaani, yameamua hamna haja ya kupima watu wachache na kuishia kuweka taswira inayopotosha kwamba hauna waathirika au kila kitu shwari, mataifa yanayopima sana yamelazimika kufunga mipaka na kuingia kwenye lockdowns na wengine curfews (Kenya).
Hizi lockdowns na curfews ni balaa, zinatesa, tunaopitia hii hali tunaweza tukawaambia ilivyo, na inapelekea wote tunaishia kuona Tanzania kama nchi ya asali na maziwa, kwamba wamebarikiwa sana kiasi cha wao kuachiwa wafanye watakavyo bila kuzuiwa sehemu yoyote na maambukizi kwao ni machache, na rais wao alishatangaza kwamba hafungi mipaka, hivyo Watanzania msikae mkishangaa kwanini majirani wanakimbilia kuja kwenu huko, mtaenedelea kuibukiwa na watu wanaokohoa kohoa.
Mpaka sasa idadi ya vipimo kwa siku
Rwanda wanapima 842 kwa siku na wapo kwenye lockdown
Kenya juzi tulipima 766 kwa siku na tupo kwenye curfew
Uganda wanapima 555 kwa siku na wapo kwenye lockdown
Tanzania nahisi wanapima 10 kwa siku maana tangu waanze kupima sijui hata kama wamefikisha jumla ya 500
Burundi ndio hata sijui wanachokifanya
Huyo mdada Mkenya anayeumwa dalili za Corona nimejaribu kujiuliza nini kinaweza kikasababisha Mkenya kwa akili zake ajue anaumwa Corona, aamue kusafiri kutokea Nairobi mpaka kwenda Tanzania, hapo kuna mawili:
- Aidha itakuwa kuna waganga wa Tanzania ambao labda wanajinadi kisiri kwamba wanatibu Corona, na ndio maana mpaka sasa maambukizi yametajwa machache huko, labda wanasema yote ni kwa ajili ya dawa zao wanazowapa Watanzania, hili linawezekana ukizingatia hiyo Tanzania ndio nchi ya yule babu aliyeidhinishwa na serikali kupokeza kikombe chake cha miujiza, watu walitokea mataifa hadi ya Ulaya, wengine walikua wanatua hata kwa helikopta.
- Sababu nyingine, inawezekana labda watu wameaminishwa kwamba hewa ya Tanzania inatibu kiasi kwamba muathirika ukifika Tanzania kirusi kinakukimbia, na ndio maana huko watu wanaendelea na shughuli wakifanya kila kitu bila kudhibitiwa.
Sasa hapo ndiyo msishangae kuendelea kuibukiwa na watu wanaofuata hiyo miujiza yenu, hata walioelimika watakuja tu maana mtu ukiumwa, elimu hukutokea maskioni na puani unabaki mtupu na tayari kufanya chochote.