Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Tanzania na Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), zimetiliana saini mkataba wa msaada wa Yen za Japan bilioni 1.527 sawa na shilingi bilioni 27.3 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini.
Mkataba huo umesainiwa katika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hitoshi Ara, kwa niaba ya Serikali ya Japan.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto.
Dkt. Mwamba alisema kuwa, ufadhili huo muhimu unaendana na Mpango wa sasa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao pamoja na masuala mengine, unalenga kutatua changamoto za ubora katika utoaji huduma za afya nchini.
“Ufadhili huu unaunga mkono juhudi za Serikali kwenye sekta ya afya, zinazolenga kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wakati kwenye jamii,” alisema Dkt Mwamba.
Tusubirie kampeni zianze tupate kusema kuwa maendeleo yote yaliyotokea Tanzania ni juhudi na nguvu za Mama Samia. Ila asanteni sana Wajapani maana kwenye miaka zaidi ya 60 ya uhuru bado watanzania tuna shida kwenye miundombinu ya afya haswa katika kipengele cha afya ya Mama na mtoto. Hakika Mama anaupiga mwingi sana.