Tanzania na Maendeleo ya Wajinga - What did Nyerere do?

Tanzania na Maendeleo ya Wajinga - What did Nyerere do?

I think we should blame 1985 when Mwinyi adopted SAP from IMF/World Bank. One of the condition was to cut the subsidy on education sector. This is one of the effect of ERP I which cost Tanzania not only on education, but health was another victim because we were not supposed to fund even education against HIV. In 1996 IMF/WB found that ERP I was a failure and they adopt ERPII which allow our government to fund education. That was when Mkapa announced that primary education will be free, but elimu ya watu wazima remained in shambo.

It 's sad to see in 2009 we're still fighting to eradicate ujinga.... what a shame, instead of injecting money on the other sector.... IMF/WB trap..... Juzi wametupa 350 billion wait and you will see.
 
Kuna kusoma na kuandika. Na kuna kuelimika.

Wasomi tunao wengi sana. Walioelimika tunao kiduchu. And this has been the case miaka yote from wakati wa uhuru mpaka leo hii.

To me, this is the crux of the problem.
 
Mtanganyika,
In 1996 IMF/WB found that ERP I was a failure and they adopt ERPII which allow our government to fund education. That was when Mkapa announced that primary education will be free, but elimu ya watu wazima remained in shambo.
..
Nakumbuka Mkapa aliondoa ada na michango ya shule za msingi mwaka 2002 sio 1996.. hii ni baada ya wananchi wengi kupiga kelele..
Ukweli ni kwamba mwaka 1997 serikali ya Mkapa iliongeza ada kutoka 1,000 hadi 2,000, shilingi 40,000 badala ya 30,000 kwa shule za sekondari za kutwa na 70,000 badala ya 45,000 kwa shule za bweni
 
Zakumi,
Mkandara:

China imejiunga na World Bank na IMF 1980. Hivyo vitu vingi walivifanya wanafanya wenyewe kwa kujitegemea.

1980 Tanzania ilikuwa imejaza mabakuri ya kuomba sadaka kila kona. Na bado bila aibu unalinganisha China na Tanzania.
Mkuu labda bado hujanipata kabisa.. maendeleo ya Bakhresa hayawezi kuwa sawa na yangu, nachozungumzia ni kwamba mwaka 1975 alikuwa mshona viatu na mimi mbangaizaji tu mtaani. Vipi kaweza kufanikiwa wakati mimi bado muobaji!..
Swala sio mimi kuwa sawa na Bakhresa isipokuwa niwe na maendeleo ya aina fulni ambayo yanaweza kulingana na jitihada zangu hata kama ningekuwa Daktari ingetosha kuonyesha nakwenda mbele..
Sasa ukianza na hizo habari za IMF na Word Bank unaipa excuse Tanzania kwa nini hatukufanikiwa..Ukianza kutumia sababu za China kwamba wao walikuwa na ujuzi miaka 100 kabla yetu ni another excuse kwa Tanzania.. jambo ambalo mimi nalikataa na kusema tuna mapungufu ktk kupanga priorities zetu na ndio maana tupo nyuma kam nchi nyinginezo iwe Egypt ambao waliakuwa na utaalam wa kufua vyuma na dhahabu toka enzi za Biblia acha hiyo China..
Sijui tumeelewana hakuna excuse isipokuwa tuna matatizo na hatuwezi kufikiria Ujamaa na siasa za mwalimu kuwa sababu kwani China na Russia walikuwa sio tu wajamaa bali Wakomunist wa kutupa na wamefanikiwa ktk mengi ikiwa ni pamoja na kuboresha elimu ya wananchi wake badala ya kufundisha siasa za Kikomunist..
 
Kulikuwa hakuna ujamaa Tanzania wala ubepari. Watu walikuwa wanafanya na mpaka sasa wanafanya sera kwa kutegemea sana mhisani atatoa kitu.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo ni masikini toka imepata uhuru, iliwezaje kufuta ujinga katika kipindi cha miaka chini ya mitano?

Ukweli wa mambo ni lazima tuwe realistic. Tanzania haikufikisha literacy rate ya 90%.
 
Na kama ilifikisha, ubora wa hiyo literacy ulikuwaje?
 
Kikojozi,

Na kama ilifikisha, ubora wa hiyo literacy ulikuwaje?
..
Nitakusaidia hapa.. moja ya sababu ilikuwa ni ada.. soma kipande hiki cha UNICEF na unaweza kusoma mengi zaidi hapa

The School Fee Abolition Initiative (SFAI) seeks to accelerate progress toward quality education for all children by supporting policies that remove cost barriers, preventing parents from enrolling
and maintaining their children at school. As explained further in the preface to this book, SFAI was launched by the United Nations Children's Fund (UNICEF) and the World Bank in 2005 as an instrument to ensure that existing Education for All (EFA) commitments were met.

Its main objective is to provide guidance and support to countries planning to abolish school fees with respect to the development and implementation of such policies. SFAI helps countries answer the following two questions: What are the challenges faced when school fees are discontinued, and what are the options for overcoming these challenges in a sustainable manner, especially in low-income countries? In many countries, recent efforts to reduce or abolish school fees are, in fact, second attempts. The first efforts were initiated many decades earlier but were abandoned or reversed under pressure of economic crises.

In Ghana, for instance, primary school fees were first abolished in 1961; while in Kenya and Tanzania, fee abolition policies were introduced in 1974. These policies had a significant impact on enrollment and resulted in rapid gains toward the goal of universal primary education (UPE). Over time, however, the policies were largely abandoned, and many of the early
gains reversed.
 
Bob mimi nadhani ...wote tunaongelea kitu kile kile..hakuna tofauti kubwa. NA UMETOA MFANO MARIDADI. KAMA WEWE NA BAKHRESA MLIKUWA MASIKINI MWAKA 1975..LEO HII YEYE ANAMILIKI SIZABLE SHARE YA GDP NA WEWE BADO UNASHONA VIATU, SURELY, LAZIMA UJIULIZE NI WAPI ALIKUACHA NYUMA.

Zakumi anahoji hizo statistics za 90%. LAKINI ndugu yetu huyu anasahau kwamba takwimu zote za dunia ya tatu tunazipokea toka huko majuu..infact tumefika hata level tumeshindwa hata kujihesabu..wengine wanaamini takwimu za CIA kuliko za serikali yetu. Partly kwa sababu takwimu nyingi za banana republic zinakuwa inflated kwa political motives. Hivi leo serikali inakwambia eti unemployment ni 30% hivi kweli hata kama wewe ni lord lofa utawaamini? si unaona ni mchanga tuu?..Mimi hata leo unavyoniambia eti uchumi wa TANZANIA unakua kwa 7% naona ni uwongo tuu..maana hakuna mabadiliko yoyote on the ground. Kifupi swala la takwimu...ni secondary, maana haya matatizo huhitaji kuambiwa..maana tunayaona. Mimi leo nahangaika kutuma karo kwa ndugu kijijini...sasa leo kweli uanze kunipa hadithi eti uchumi unakuwa? wakati sioni mabadiliko yoyote katika jitihada za hawa wakubwa? Kila nikienda village hali nakuta imekuwa ngumu kuliko nilivyoiacha..na hapa siyo mimi tuu..tuko wengi ambao we have to struggle on both fronts.

Mimi nimefika point naamini kabisa..Tanzania sisi ni masikini than we are willing to admit. Ni mpaka pale tutakapokubali ukweli, tutakapozinduka. Hili swala la maendeleo ni chimera ya mchana kabisa.

Perhaps, idea ya maendeleo tuiache kwanza, tupambane tupate mazingira ya kutuwezesha kutafuta hayo maendeleo (HAPA NAONGELEA VITU KAMA UFISADI, UZEMBE, UBADHIRIFU WA MALI YA UMMA, NEPOTISM ZA AKINA SALVA NK AMBAVYO VINAFANYA MAENDELEO KUPATIKANA IWE NDOTO). Kwa sababu sasa hivi tunapigania maendeleo wakati mazingira hayaturuhusu. END RESULTS..MAZINGIRA YANAZIDI KUWA MAGUMU NA MAENDELEO HATUYAPATI!
 
Zakumi,
Kulikuwa hakuna ujamaa Tanzania wala ubepari. Watu walikuwa wanafanya na mpaka sasa wanafanya sera kwa kutegemea sana mhisani atatoa kitu.
Mkuu wangu vipi tena ni wewe unayedai hapa kuhusiana na Nyerere na Ujamaa wake, kisha tena unarudi na kusema Tanzania kulikuwa hakuna Ujamaa..Nani kasema kulikuwa na Ujamaa!..bila shaka tunachozungumzia hapa ni Siasa ya ujamaa kama mwongozo wa maendeleo ya Watanzania..
Kumbuka maneno ya mwalimu alipotoa mfano wa Ukristu..kuwa unaweza kwenda kanisani ukakuta hesabu ndogo sana ya wakristu wanaosali, hii haina maana hakuna hesabu kubwa ya wakristu nchini isipokuwa wengi hawa practice Ukristu....

Mimi nitaongezea tu kwamba na Biblia ni mwongozo wao ambao kama kuna matatizo yatokanayo na mwongozo wa Biblia ndilo liwe somo, sio mahudhurio ya wakristu kanisani kuwa mfano wa hoja ya kuwepo Ukristu nchini.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo ni masikini toka imepata uhuru, iliwezaje kufuta ujinga katika kipindi cha miaka chini ya mitano?
Ukweli wa mambo ni lazima tuwe realistic. Tanzania haikufikisha literacy rate ya 90%.
Hizi dataz unazipata wapi?.. Tumepata Uhuru mwaka 1961 hayo mafanikio chini ya miaka mitano, hata kama tukichukulia mwaka 1967 kweli kulikuwepo na mafanikio ya aina hiyo!..
Mkuu wangu Literacy ni neno pana sana inabidi uelewe kinachozungumziwa.. Kifupi hadi leo mimi bado mjinga, nazidi kujifunza toka kwenu.. Elimu haina mwisho!
 
Masanja,
Mkuu wangu haya ndio maneno... maneno yanayojenga na kutuweka hapa ili tupate kufikiria suluhu ya kutokana na umaskini wetu..Tutazungumza na kulaumu hata Mungu na Malaika wake kwa sababu tunashindwa kujitazama sisi wenyewe kwa aibu kubwa ya tupu zetu..
Kifupi Tanzania leo inatembea uchi wa mnyama tukidai kuwa ndio maendeleo, ati mbona wazungu wanafanya hayo kumbe sisi tumeshindwa kwa sababu hatuna uwezo ikichangiwa na Ulimbukeni (kuiga) wakati wenzetu Wazungu wanafanya hivyo ili kupata suntan..
 
Masanja,Zakumi,Mkandara,...

..maendeleo lazima yawe sustainable.

..wengine wanadai maendeleo ya kufuta ujinga hayakuwa sustainable kutokana na mipango ya IMF na WB ya SAP.

..tunapaswa kujiuliza kwanini tulitafuta msaada wa IMF na WB na matokeo yake tukaingizwa kwenye mpanga SAP?

..je, tusingetafuta msaada IMF na WB tungeweza ku-sustain na kuyalinda mafanikio tuliyoyapata ktk kufuta ujinga?

..kwa hapa tulipofikia/tulipo ni kitu gani kinatuzuia kuanza ku-invest tena ktk elimu na kufuta ujinga?

..je, tutumie mbinu gani kuhakikisha kwamba, iwapo tuta-invest ktk elimu, basi tutaweza kulinda/ku-sustain mafanikio tutakayoyapata.
 
Last edited:
Hapa wengi tunafunika vichwa kwenye mchanga kwa kujaribu kujificha kwenye ukoloni, IMF/WB, ujamaa; kila kitu kitalaumiwa.

Ukweli ni kuwa tuna matatizo ya kutojua nini kama taifa inatakiwa tukifanye. Mapato ya kodi za watanzania yanakwenda wapi?

1/Kwenye mikutano ya kila siku isiyo na tija na malipo manono manono ya sitting allowances

2/Kwenye semina na makongamano ambayo mengi hayana tija pamoja na subsistence allowances pamoja na full board hotel accomodations zinazolipwa kwa maofisa wetu

3/Kwenye kumaintain maelfu ya mashingingi na kuyatia mafuta kwa ajili ya kufanya safari zisizo na tija

4/Kwenye rushwa za kisiasa kuhakikisha tunabaki madarakani daima dawamu

5/Malipo ya bidhaa hewa ambazo kila siku serikali inasingiziwa kuzinunua kwa bei zilizopandishwa mno

Tukishatumia fedha hizo zimekwisha, tunaenda world bank kukopa. Huko tunakoenda kukopa wanaotupa hiyo mikopo wanatamani nao wangekuwa na magari ya fahari kama tunayotumia sisi. Wanashangaa, halafu wanatukong'oli kwa masharti ambayo yanahakikisha mikopo yote asilimia 50 inarudi kwao. Halafu lazima tutalipa mikopo yote na riba juu.

Tutaondokana na hayo matatizo ya kushuka literacy rate na kuongezeka umaskini siku tutakapo;

1/Jua kusimamia hazina yetu ya taifa na kuhakikisha kuwa kilichokusanywa huko kinarudi kwa wazalishaji.

2/Matumizi yetu makubwa yanaelekezwa katika kuwaandaa watu wetu kujiletea maendeleo kwa kuwapa elimu bora na ya kutosha. Matumizi yaelekezwe katika kuandaa walimu bora na wa kutosha, kuhakikisha shule zetu zinavyo vifaa bora na vya kutosha, kusimamia mitaala na kuhakikisha haichezewi na wachuuzi

3/Kuwawezesha walipa kodi watanzania kwa kuwapa vivutio vitakavyo wawezesha kuanzisha na kukuza biashara zao ili kuumiliki uchumi

4/Kusambaratisha magenge ya wezi na wanyang'anyi waliojazana katika mfumo wa utawala na vyama vya kibangaizaji vinavyoitwa vya siasa

5/Kujenga miundo mbinu kama barabara na madaraja na njia za kisasa za mawasiliano zitakazowezesha kukua kwa biashara kati ya watu wa nchi hii

Fedha inayopatikana inatosha kufanya yote hayo ila inaelekezwa kusikofaa.
 
Huu ni uthibitisho mwingine kwamba walioingia madarakani kuanzia awamu ya pili hadi ya nne wamezembea na kuachia mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa Nyerere kwa kujua kusoma na kuandika kupitia elimu ya watu wazima yapotee bure sasa hivi tumerudi nyuma zaidi kuliko hata tulipokuwa 1970.

Hii ni sera maalum kati ya sera zilizofichika kuwa kuwaelimisha watanzania ni kujinyima kura wakati wa uchaguzi. Ni rahisi sana kuwarubuni wasiojua kusoma kwa wali na nyama wakakupa kura kuliko wasomi.

"Mustakabali wa nchi utakuwa mashakani kuwa na watu wengi wenye degree bila ya kuwa na kazi"- Mohammed Seif Khatibu (alipokuwa waziri wa habari, akitoa ufafanuzi wa kuzuia taasisi nyingi kugeuzwa Universities)
 
Bob mimi nadhani ...wote tunaongelea kitu kile kile..hakuna tofauti kubwa. NA UMETOA MFANO MARIDADI. KAMA WEWE NA BAKHRESA MLIKUWA MASIKINI MWAKA 1975..LEO HII YEYE ANAMILIKI SIZABLE SHARE YA GDP NA WEWE BADO UNASHONA VIATU, SURELY, LAZIMA UJIULIZE NI WAPI ALIKUACHA NYUMA.

Zakumi anahoji hizo statistics za 90%. LAKINI ndugu yetu huyu anasahau kwamba takwimu zote za dunia ya tatu tunazipokea toka huko majuu..infact tumefika hata level tumeshindwa hata kujihesabu..wengine wanaamini takwimu za CIA kuliko za serikali yetu. Partly kwa sababu takwimu nyingi za banana republic zinakuwa inflated kwa political motives. Hivi leo serikali inakwambia eti unemployment ni 30% hivi kweli hata kama wewe ni lord lofa utawaamini? si unaona ni mchanga tuu?..Mimi hata leo unavyoniambia eti uchumi wa TANZANIA unakua kwa 7% naona ni uwongo tuu..maana hakuna mabadiliko yoyote on the ground. Kifupi swala la takwimu...ni secondary, maana haya matatizo huhitaji kuambiwa..maana tunayaona. Mimi leo nahangaika kutuma karo kwa ndugu kijijini...sasa leo kweli uanze kunipa hadithi eti uchumi unakuwa? wakati sioni mabadiliko yoyote katika jitihada za hawa wakubwa? Kila nikienda village hali nakuta imekuwa ngumu kuliko nilivyoiacha..na hapa siyo mimi tuu..tuko wengi ambao we have to struggle on both fronts.

Mimi nimefika point naamini kabisa..Tanzania sisi ni masikini than we are willing to admit. Ni mpaka pale tutakapokubali ukweli, tutakapozinduka. Hili swala la maendeleo ni chimera ya mchana kabisa.

Perhaps, idea ya maendeleo tuiache kwanza, tupambane tupate mazingira ya kutuwezesha kutafuta hayo maendeleo (HAPA NAONGELEA VITU KAMA UFISADI, UZEMBE, UBADHIRIFU WA MALI YA UMMA, NEPOTISM ZA AKINA SALVA NK AMBAVYO VINAFANYA MAENDELEO KUPATIKANA IWE NDOTO). Kwa sababu sasa hivi tunapigania maendeleo wakati mazingira hayaturuhusu. END RESULTS..MAZINGIRA YANAZIDI KUWA MAGUMU NA MAENDELEO HATUYAPATI!

Masanja:

Naona umenipata. Katika nchi kama ya kwetu, ambayo kiongozi anatoa amri kwa mkuu wa wilaya kuwa usipojenga shule 50, utafukuzwa kazi. Ni lazima uanze kujiuliza. Je kama mkuu wa wilaya hana resources za kujenga shule hizo, atakubali kibarua chake kiote nyasi.

Hakuna atakayekubali. Na matokeo yake zitajengwa shule za mabox na baada ya miaka mitatu shule zimebomoka.

Hakuna Ofisa elimu ambaye hakutaka kupanda cheo. Hivyo ukimwambia afisa elimu kuwa tunataka watu wote wajue kusoma na kuandika katika kipindi cha miaka mitano. Atakuletea ripoti ya kuonyesha juhudi zake.

Mfano mmoja: Kabla ya 1985, nilikuwa nasoma mkoani Mwanza. Na afisa elimu alitakiwa kutoa ripoti ya wanaojua kusoma na kuandika. Alichofanya afisa elimu ni kuja shuleni kwetu na kuchukua wanafunzi wa darasa la tano, sita na la saba kumsaidia kuhesabu kura za uchaguzi za mwaka 1975 na 1980.

Hivyo kura ya mpiga dole gumba ni ya asiyejua kusoma na kura yenye jina ni kura ya anayejua kusoma.

Mwaka 1985, kwa sababu ya ukosefu wa wasimamizi wa uchaguzi, nilisimamia uchaguzi wa rais na wabunge japokuwa umri wangu ulikuwa chini ya umri wa wapiga kura. Katika kijiji nilichosimamia, ukiondoa mwenyekiti wa kijiji, hakuna aliyeweza kutia sahihi. Kila mtu alitia dole gumba.

Siwezi kuziita hizi episodes mbili kama ni data. Lakini zimenishawishi mimi siku zote ku-question muundo mzima wa serikali yetu ambayo viongozi wa juu wanapanga mipango na kuwasukumia viongozi wa ngazi za chini kutekeleza na wao kusubiri matokeo ya utekelezaji wa mipango hiyo.
 
Jokakuu,
Mimi binafsi nakubaliana kabisa na mchango wa IMF na Wolrd Bank umetupotosha zaidi ktk yale ambayo ni asili ya jamii hii...Nakumbuka kati ya masharti magumu tuliyokutana nayo ilikuwa ni pamoja na kupunguza mfuko wa social expenditure, kuondoa subsidies ktk chakula, devalue currency yetu na kibaya zaidi introduction of user fees for education and health care.. ktk nchi ambayo asilimia 90 ni maskini wasiojiweza. Sasa vitu kama hivi huhitaji kuwa scientist kuelewa kwamba ktk mazingira yetu utaua kabisa standard of living kutokana na kipato cha wananchi wahusika..
Leo hii nina hakika sio elimu tu hata health ya wananchi wetu imeshuka kiasi kwamba yawezekana kabisa kuwa zaidi ya wanawake 10,000 wanakufa kila mwaka kutokana na pregnancy-related complications na sababu kubwa ni kukata matumizi ktk sehemu hizo muhimu ktk jamii yetu..kuna report moja niliiona ikisema kwamba watoto wanaozaliwa ni kati ya aslimia 20 hufariki kabla ya mwaka mmoja na zaidi ya asilimia 50 hufa kabla ya miaka mitano!..Jamani hii sio disaster!..

Mishahara pamoja na kupanda kwa namba bado kabisa huwezi kulinganisha na cost of living ilivyonda na nachelea kusema watu waliishi vizuri (afford necessities of life) kwa mishahara wakati wa mwalimu kuliko leo hii..Tulikosa wakati ule ni upatikanaji wa vitu hivyo kwa hiyo kilichotakiwa zaidi ni kubadilisha mfumo wa kiuchumi ktk uzalishaji na usambazaji zaidi kwani tayari kilimo kilikuwa kimeshapewa kipaumbele..

Hakuna zuri lolote linalotokana na SAP kwa nchi yetu zaidi ya kufuata wazungu wanasema nini, tulikuwa na uwezo wa kukataa badhii ya masharti na tungefanikiwa kwani leo hii tumeshindwa hata kurudi nyuma kutazama wapi tulikosea kwa sababu hatuna jawabu.. Na sababu kubwa kwa nini hatuna jawabu tunajaribu kutazama wazungu au vitabu vinasema nini!..
Ndio Ugonvi wangu mkubwa na ELIMU inayotolewa siku hizi.. Ikiwa Elimu waliyopata hawa viongozi wetu imeshindwa kuwa applied ktk mazingira yetu na kuleta maendeleo acha mbali sustainable bado tutegemea punda aliyechoka?..
Mkuu wangu IMF na World bank ni biashara kwanza hilo lazima tulifahamu.. Ni sawa na benki zote za ukopeshaji duniani kutoa huduma zao ni part ya biashara yao hivyo riba ni lazima wabvute ili wao waweze kuwa sustainable as bank..Kila unavyozidi kuwa na matatizo ndivyo ukakavyokuja kuomba msaada na haya mashirika mawili yapo kwa sababu ya matatizo..Ikiwa nchi zote maskini zitaondokana na Umaskini hawa jama wakakuwa hawana biashara..Nakumbuka tulipoanza kukorofishana nao Mtei (Mtazamia)alikuwa akifanya kazi IMF na tulishindwa kufikia makubaliano na chombo hicho tukiwa na ndugu yetu ndani..
 
Zakumi,
Mfano mmoja: Kabla ya 1985, nilikuwa nasoma mkoani Mwanza. Na afisa elimu alitakiwa kutoa ripoti ya wanaojua kusoma na kuandika. Alichofanya afisa elimu ni kuja shuleni kwetu na kuchukua wanafunzi wa darasa la tano, sita na la saba kumsaidia kuhesabu kura za uchaguzi za mwaka 1975 na 1980.
Hivyo kura ya mpiga dole gumba ni ya asiyejua kusoma na kura yenye jina ni kura ya anayejua kusoma.
Mwaka 1985, kwa sababu ya ukosefu wa wasimamizi wa uchaguzi, nilisimamia uchaguzi wa rais na wabunge japokuwa umri wangu ulikuwa chini ya umri wa wapiga kura. Katika kijiji nilichosimamia, ukiondoa mwenyekiti wa kijiji, hakuna aliyeweza kutia sahihi. Kila mtu alitia dole gumba.
Mkuu wangu pengine hufahamu juhudi alizofanya mwalimu miaka ya 70 ktk shule za msingi na Elimu ya watu wazima.. unafanya kusimuliwa uliza sisi tuliokuwepona akili timamu yaani watu wazima tayari..utafahamishwa vizuri..
Katika Uchaguzi kuweka dole hata Marekani wanafanya hivyo sio kwa sababu watu hawawezi wekeka sahihi zao isipokuwa ni uthibitisho mzuri wa kura ya mtu..Hakuna kitu rahisi kama sahihi unaweza andikia madudu yoyote na mtu asikuulize.. kwani hakuna record ya sahihi za watu mahala popote..
Finger print ni utaalam uliokuwepo toka zamani sana haina maana anayeweka dole hajui kusoma na kuandika.
 
Masanja,Zakumi,Mkandara,...

..maendeleo lazima yawe sustainable.

..wengine wanadai maendeleo ya kufuta ujinga hayakuwa sustainable kutokana na mipango ya IMF na WB ya SAP.

..tunapaswa kujiuliza kwanini tulitafuta msaada wa IMF na WB na matokeo yake tukaingizwa kwenye mpanga SAP?

..je, tusingetafuta msaada IMF na WB tungeweza ku-sustain na kuyalinda mafanikio tuliyoyapata ktk kufuta ujinga?

..kwa hapa tulipofikia/tulipo ni kitu gani kinatuzuia kuanza ku-invest tena ktk elimu na kufuta ujinga?

..je, tutumie mbinu gani kuhakikisha kwamba, iwapo tuta-invest ktk elimu, basi tutaweza kulinda/ku-sustain mafanikio tutakayoyapata.

Sitohi lawama yoyote kwa WB na IMF. Kwa maoni yangu, we are so luck kwa vyombo hivi ku-exist.

Kuna viwanda na miradi kibao imefunguliwa kwa misaada au grants za hivyo vyombo.

Mmoja wa mradi ujenzi wa kisasa wa kiwanda cha viatu Morogoro ambacho mpaka wakati kinafungwa, uzalishajiwa wake ulikuwa chini ya 4%.

Sijamuona mtanzania yoyote anayeandamana kuunga mkono misaada ya WB. Lakini pale tunapopata matatizo na kupewa tiba na WB, tupo rahisi kulalamika.

Sasa tukirudi kwenye mada. Bila SAPs literacy rate yetu ingeporomoka zaidi kufika 40% au 50%. Ni uchumi wa nchi unao-sustain huduma za jamii na sio vinginevyo.

Kuhusu ku-invest tena katika elimu, kwa maoni yangu imefika wakati tujiulize swali moja tu. Hivi kwa idadi ya wasomi waliopo, wanaomaliza shule kila mwaka na taasisi zetu za elimu, je tunaweza kuendesha maendeleo yanayojitegemea?

Kama tunaweza, tuanze hayo maendeleo na mambo mengine yataji-sort yenyewe.

Literacy rate ni indicator tu. Na kama watu kazi wanazozifanya ni kuokota kuni, kulima robo heka ya mpunga literacy rate ni indicator isiyo na maana yoyote.
 
Zakumi,
Mkuu vipi tena!.. kwani kiwanda cha viatu Morogoro kilijengwa kutokana na msaada wa program ya SAP?.. mbona hatuelewani!
 
Zakumi,

Mkuu wangu pengine hufahamu juhudi alizofanya mwalimu miaka ya 70 ktk shule za msingi na Elimu ya watu wazima.. unafanya kusimuliwa uliza sisi tuliokuwepona akili timamu yaani watu wazima tayari..utafahamishwa vizuri..
Katika Uchaguzi kuweka dole hata Marekani wanafanya hivyo sio kwa sababu watu hawawezi wekeka sahihi zao isipokuwa ni uthibitisho mzuri wa kura ya mtu..Hakuna kitu rahisi kama sahihi unaweza andikia madudu yoyote na mtu asikuulize.. kwani hakuna record ya sahihi za watu mahala popote..
Finger print ni utaalam uliokuwepo toka zamani sana haina maana anayeweka dole hajui kusoma na kuandika.

Mkandara:

I said what I had seen.
 
Zakumi,
Mkuu vipi tena!.. kwani kiwanda cha viatu Morogoro kilijengwa kutokana na msaada wa program ya SAP?.. mbona hatuelewani!

I am not sure if you understood me. Nimetoa mfano kuonyesha kuwa WB na IMF sio wa kulaumiwa. Kwa sababu kabla ya SAPs kuanza in full swing, walishasaidia sana modernity yetu.
 
Back
Top Bottom