Tanzania na Saudi Arabia kushirikiana kudhibiti Uhalifu Mtandaoni

Tanzania na Saudi Arabia kushirikiana kudhibiti Uhalifu Mtandaoni


Serikali za Tanzania na Saudi Arabia zimeingia makubaliano ya kusaidiana katika kukabiliana na uhalifu ikiwemo uhalifu wa mitandaoni.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano huo kwa upande wa Tanzania jijini Riyadh, Saudi Arabia.


Akibainisha maeneo mengine ya ushirikiano huo, Waziri Masauni amesema pia makubaliano hayo yatahusisha namna ya kukabiliana na majanga ya moto, ajali za barabarani na ajali za majini.

Hati za makubalino hayo kwa upande wa SaudI Arabia zimetiwa saini na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudia, Mwanamfalme Abdul Aziz Bin Saud Al Saudi.

Waziri Masauni yuko nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi.

Akina mkojani wamewai kuweza nini

Hao zaidi ya kugawa kondoo na kugawa nyamaaa .

Nina uhakikaa kuna mradi unanukia
 
Awamu hii mtasumulishwa bila kujielewa😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭.
 
Tungeanza kudhibiti uhalifu wa kutekana kwa ground kabla ya hayo ya mtandaoni 🐒
 
Kwanini tudhibiti kutekana?
Kwa sababu kuna genge la uhalifu linafarakanisha taifa kwa utekaji

1000012681.jpg
 
Genge lolote linalohusika na utekaji lidhibitiwe ili kuepusha mifarakano kwenye taifa
Wakiruhusu bangi itakua hakuna magenge. Bangi za kujificha na kuvutia chooni zina madhara.
 
Back
Top Bottom