Tanzania na Saudi Arabia kushirikiana kudhibiti Uhalifu Mtandaoni

Tanzania na Saudi Arabia kushirikiana kudhibiti Uhalifu Mtandaoni


Serikali za Tanzania na Saudi Arabia zimeingia makubaliano ya kusaidiana katika kukabiliana na uhalifu ikiwemo uhalifu wa mitandaoni.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano huo kwa upande wa Tanzania jijini Riyadh, Saudi Arabia.


Akibainisha maeneo mengine ya ushirikiano huo, Waziri Masauni amesema pia makubaliano hayo yatahusisha namna ya kukabiliana na majanga ya moto, ajali za barabarani na ajali za majini.

Hati za makubalino hayo kwa upande wa SaudI Arabia zimetiwa saini na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudia, Mwanamfalme Abdul Aziz Bin Saud Al Saudi.

Waziri Masauni yuko nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi.

Wacha weeeeee wacha tuone
 
Riyadh, September 19, 2024, SPA --


Minister of Interior Prince Abdulaziz bin Saud bin Naif bin Abdulaziz received Minister of Home Affairs of the United Republic of Tanzania Eng. Hamad Yussuf Masauni at the ministry headquarters in Riyadh today.

During the meeting, the two sides discussed ways to enhance security cooperation between the two countries and addressed several issues of mutual interest.

Following the reception, Prince Abdulaziz and Masauni signed a security cooperation agreement, and a memorandum of understanding for cooperation in civil defense and protection between the governments of Saudi Arabia and Tanzania.
Source --SPA
 
Riyadh, Saudi Arabia

TANZANIA NA SAUDIA ZATIA SAINI MAKUBALIANO YA UOKOZI NA ULINZI DHIDI YA MAJANGA

1726914346540.png


Waziri wa Mambo ya Ndani Prince Abdulaziz bin Saud bin Naif bin Abdulaziz akimpokea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Eng. Hamad Yussuf Masauni katika makao makuu ya wizara mjini Riyadh leo.

Katika mkutano huo, pande hizo mbili zilijadili njia za kuimarisha ushirikiano wa kiusalama kati ya nchi hizo mbili na kushughulikia masuala kadhaa yenye maslahi kwa pande zote mbili.

Kufuatia mapokezi hayo, Prince Abdulaziz na Masauni walitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kiusalama, na hati ya makubaliano ya ushirikiano katika usalama na ulinzi wa raia dhidi ya majanga na utayari wa uokozi wa raia kati ya serikali ya Saudi Arabia na Tanzania.
Chanzo --SPA
 
How ?

Ni kama watu mna njaa na hamna chakula alafu msimamizi wa mirathi anahangaika kutafuta mbinu za kuwawezesha kwenda Holiday.....; Na katika utafutaji wa mbinu anatumia kahifadhi kenu kadogo...
 
Back
Top Bottom