Tanzania na siasa: Lugha ya kutumia Kiswahili au Kiingereza, Tatizo lipo wapi?

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
25,260
Reaction score
7,204
Nimesikia ktk ITV leo na hata katika mijadala mbalimbalia kuhusu uimara wa kiswahili na tatizo linalosababishwa na Kiswahili.

katika akufuatilia nimeona tatizo si Lugha na hata kama lingekuwa lugha bado hatutakiwi kataa lugha.Wenzetu wanchi kubwa ambao lugha yao ni ya kimataifa ila si kiingereza, wanajipanulia nafasi kwa kujifunza lugha nyingi sana kwa gharama kubwa sana ili waweze jipanulia wigo ktk maisha.Mfano Ujerumani nchi yenye uchumi mkubwa wa kubeba ulaya.Pamoja na kwamba wanathamini sana lugha yao ktk nchi yao,bado hawaoni haja ya kupambana na kiigereza duniani.sabau ikiwa ni kwmaba tayari kiingereza kimesambaa sana na vi vyea kutumia hiyo platform.

Nikiangalia kwa makini nimekuja gundua kuwa si watanzania wengi wanaweza jieleza kwa ufasaha kwa lugh ayoyote waliyowahi jifunza.Hii inaonyesha tatizo lipo ktk walimu zaidi, pamoja na kukosa kuwa makini ktk mambo yetu.

katik amjadala wa leo waongeaji wengi walikuw awakifuata mkumbo kwa majibu mepesi sana ya kutaka kiswahili,kikishika hatamu.Wao wenyewe wanatumia vijineno vya kiingereza kibovu ili kusisitiza hoja zao nyepesi.

Ninachoweza tahadharisha watu hapa ni kuhusu kuw amaini sana na huu ushabiki wa kutaka kiswahili kishike hatamu.nadhani tunahitaji kwenda hivihivi.Ufundishaji ukiwa na umakini tunaweza toa wanafunzi makini wenye kujua lugha zote kwa umakini na wenye kuwez kieleza vyema.Ipo siku tutakuja juta kama tunavyojuta kwa maamuzi ya kichaa Mungai kufuta technical subject, kukusanya masomo yote ya sayansi ktk somo moja .Na kuondoa michezo.leo tuna wasomi wasiojua science nyepesi kwa maisha,wanafikia mahali pa kunshidwa elewa mazungumzo mepesi tuu toka kwa wasomi wa fani nyingine.Tuna vihiyo kila mahali, tuna watu wanaoongoza watalii waliokimbia somo ya Biology au agriculture sekondari na primary kwa miaka yote halafu waksiahfeli wanakuja soma kozi ya miezi mitatu halafu wanakwenda ongoza watalii wengine ni maprofessor wa zoology.

Kwanza hiyo miaka ya kusoma kiingereza tokea darasa la 3 hadi chuo kikuu ni miaka mingi sana,kila mtu angepaswa kuelewa lugha zaidi ya moja.Inakuweje wanaokwedna soma uchina na urusi,a unchi nyingine wanapotakiwa soma kugha kw akipindi kifupi na kuanza soma fani husika?

Tunapata shida elewa mikataba inayohusu sayansi na mengine kwa vile tuna wansheria wasio hata na basi knowledge ktk fani husika.

Huku tunajidanganya kuwa sijui spain,german, sijui russia, sijui japan etc kuwa wanatumia lugha zao kutatusaidia nini?Hizo nchi zina watu wapo very competetent ktk lugh za kigeni kwa fani zote za kielimu na utamaduni.wana uwezo mkubwa wa kutafsiri taaluma mbalimbalia kwa watu wa ndani na kwa usahihi mkubwa.sisi hata watu watukta hawajaweza tupa maneno sahihi kwa maeneo ya tehcnologia ya computer, madawa, na hata mambo yahusuyo riwaya tuu.

Ipo siku tunajuta kw akukiweka kizazi kizima ktk shimo wasiloweza toka na hivyo nchi kuwa na kizazi kizima hakina mtu wakutumia kwa maendeleo ya nchi.Hadi sasa hivi kuna walimu wengi tuu hawawezi fundisha somo kwa ufasaha kwa Kiswahili peke yake.

Kiswahili kinakosa sana uwezo wa kuelezea fikra na vitu vingine visivyoshikika amabvyo ni msingi wa sayansi.
 
Mfano.

Nimepewa deal la kutafsiri kitabu cha Brian Green cha Fizikia kwenda kwenye Kiswahili.

Kabla sijakubali, inabidi nijue jinsi ya kutafsiri misamiati.

Niambie neno "quantum" kiswahili chake ni nini?
 
-vipi kuhusu forge-ahead, maneuverability, polarized,cross over, multiplexing, artificial,unicode, sopersonic, traces,rudder,aerodyanamics, magnetron ,Teleporting,impedance, black hole, synchronize,randomize,blackmailing,anti-matter etc.Ni nadra kuweza tafsiri haya maneno bila kuishia kuyaelezea, ukijipa tafsiri ambayo si rasmi halafu muda si mrefu msomaji akashindwa jua lipi afuate.
 
Mfano.

Nimepewa deal la kutafsiri kitabu cha Brian Green cha Fizikia kwenda kwenye Kiswahili.

Kabla sijakubali, inabidi nijue jinsi ya kutafsiri misamiati.

Niambie neno "quantum" kiswahili chake ni nini?

Hapa ndo tatizo letu linapoanzia, kwa nini tutafsiri vitatabu vya watu wengine? Kama tunataka vitabu vilivyoandikwa kiswahili kwa nini tusitunge vya kwetu? Nimesoma Ujerumani, hakuna kitabu cha kiingereza kinachotafsiriwa, wanatumia vitabu vyao walivyoandika wenyewe kwa Kijerumani, vitabu vilivyoandikwa kwa kiingereza vinatumika mashuleni vikiwa hivyo hivyo, labrary za vyuo vikuu huko zina vitabu vingi tu viliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza na vinatumika vikiwa hivyohivyo.

Point yangu hapa ni kumsapoti mleta maada, watu wamekariri kwamba nchi zilizoendelea hazithamini Kiingereza, HIYO NI NOTION YA UONGO. Huwa wanakikomalia hasa kuhakikisha mtoto anayemaliza shule anajuwa kuongea Kiingereza, mtoto aliyemaliza sekondari Ujerumani anaongea kingereza vizuri huwezi kabisa kulinganisha na anayemaliza sekondari Tanzania.

Mfano tu ni kwamba wajerumani pamoja na kuwa wanapenda lugha yao, lakini TV yao ya DW ina channel inayotangaza duniani kwa kiingereza. Academic journals nyingi ziaandikwa kwa English, zikiwemo nyingi zinazoandikwa na kumilikiwa na wajerumani, au hata mataifa mengine ambayo lugha zao za asili si Kiingereza.

Tutaendelea kukaa na kujifariji na umaimuna wetu eti tukipotezee kingereza, lakini hiyo haitabadilisha umuhimu wa English katika kuleta maendeleo kwenye dunia ya leo. Ni wajinga kama sisi tu tunaoweza kudhani tutaendelea kama tutakipotezea kiingereza.
 
vipi smart phones, Tablet,PC, Touch screen, threading,superlative, supernatural,flirt?
 
Hapa ndo tatizo letu linapoanzia, kwa nini tutafsiri vitatabu vya watu wengine? Kamwa tunataka vitabu vilivyoandikwa kiswahili kwa nini tusitunge vya kwetu? Nimesoma Ujerumani, hakuna kitabu cha kiingereza kinachotafsiriwa, wanatumia vitabu vyao walivyoandika wenyewe kwa Kijerumani, vitabu vilivyoandikwa kwa kiingereza vinatumika mashuleni vikiwa hivyo hivyo, labrary za vyuo vikuu huko zina vitabu vingi tu viliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza na vinatumika vikiwa hivyohivyo.

Wajerumani kidogo ni tofauti na wengine kwani kwa kiasi fulani wanakijua kiingereza safi na wana ugonjwa wa kujua lugha nyingi.Na walishagive up battle ya kutaka kueneza kijerumani kwa nguvu duniani.USA na Ujerumani tayari muamko upo kwa lugha za mataifa,kwao lengo ni kuweza wasoma na kujiweka sehemu ya kiushindani.Wanatafsiri baadhi ya vitu vya kitechnologia huku wakiwapa watu wao original zake, ili kuwaacha wakiwa competitive duniani.Mimi sijui kama tukijifunza kiswahili pekee kama tutaweza chomoka kwenye ujinga.

Sasa hivi hata nchi za Kifaransa na kihispania zinafanya juhudi kubwa ya kuingiza kiingereza ktk list.

Point yangu hapa ni kumsapoti mleta maada, watu wamekariri kwamba nchi zilizoendelea hazithamini Kiingereza, HIYO NI NOTION YA OUNGO. Huwa wanakikomalia hasa kuhakikisha mtoto anayemaliza shule anajuwa kuongea Kiingereza, mtoto aliyemaliza sekondari Ujerumani anaongea kingereza vizuri huwezi kabisa kulinganisha na anayemaliza sekondari Tanzania.

Mfano tu ni kwamba wajerumani pamoja na kuwa wanapenda lugha yao, lakini TV yao ya DW ina channel inayotangaza duniani kwa kiingereza. Academic journals nyingi ziaandikwa kwa English, zikiwemo nyingi zinazoandikwa na kumilikiwa na wajerumani, au hata mataifa mengine ambayo lugha zao za asili si Kiingereza.

Tutaendelea kukaa na kujifariji na umaimuna wetu eti tukipotezee kingereza, lakini hiyo haitabadilisha umuhimu wa English katika kuleta maendeleo kwenye dunia ya leo. Ni wajinga kama sisi tu tunaoweza kudhani tutaendelea kama tutakipotezea kiingereza.

Kiswahili kinatakiwa kiende parallel na kiingereza na lugha nyingine, hapa tuu kuna shida ya kazi ndani ya nchi yetu kwa vile kiingereza ni kibovu.Mbaya zaidi hata ukisamehe ubovu wa kiingereza bado kuwakilisha kitu kwa kiswahili kwa usahihi unaohitajika ni shughuli sana.

Ukibahatika kusikiliza na kuona mahojiano ktk TV au radio kwa watanzania wa sehemu yoyo ktk jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Utaona jinsi watu wasivyojua jieleza,wasivyotoa sababu za msingi za majibu wanayoyatoa.Yaani watu hawajui vitu,hawajui lugha, na hawajui maneno sahihi yanayosema kitu sahihi.Hii power inatakiwa ipatikane ktk kuongea kwanza kwani kuandika ni kipaji.

Watu wanatumia maneno too general ktk mazungumzo ili wakibanwa wabadili,ila yanawafanya kuwa dhaifu sana.
 
Historia ya lugha ya kiingereza imegawanyika mara tatu kuna old english (ambayo unless you're a linguistic you have no chance of deciphering it), middle english (again today unless you're an english scholar, apart from that no chance many of us can read it) na modern english (ambayo hata hiyo old modern yale yale kuilewa kwa watu kama mimi).

Na kote huko kumetokana na influence nyingi ambazo ziliambatana na kutawaliwa lakini major influence ya modern english ni germany ambayo ina maneno mengi na latin (to be specific the french version), hizo ndizo lugha ambazo zimetawala lugha ya kiingereza leo.

Worst of lugha inazungumzwa kwa namna nyingi sana leo kwenye jamii ya waingereza, lugha ya uswahilini kuna watu wa juu hawailewi na lugha ya msomi wa daraja la juu mzungu wa chini inakuwa ngumu kuielewa. Kwani lugha ya juu imetawalia na misamiati na ufahamu to precise descriptions, kuna watu kwenye media wakisikika ni kama drama kwa maongezi yao tu.

Get a chance to listen to this guy they call 'Stephen Fry' utaelewa ninacho ongela hapa in terms of proper usage of English, they call him an artist just because of his choices of words and his elaboration, that skills comes with a vast knowledge of things and their jargon's.
 
Pia tukumbuke Kiingereza pia kimeazima maneno ya kisayansi/kihisabati kutoka Uarabuni kama hili hapa:

algebra |ˈaljəbrə|nounthe part of mathematics in which letters and other general symbols are used to represent numbers and quantities in formulae and equations.• a system of this based on given axioms.DERIVATIVESalgebraist |-ˌbrā-ist| nounORIGIN late Middle English : from Italian, Spanish, and medieval Latin, from Arabic al-jabr ‘the reunion of broken parts,' ‘bone setting,' from jabara ‘reunite, restore.' The original sense, [the surgical treatment of fractures,] probably came via Spanish, in which it survives; the mathematical sense comes from the title of a book, עilm al-jabr wa'l-muḳābala ‘the science of restoring what is missing and equating like with like,' by the mathematician al- K wārizmī (seealgorithm ).
 
Mfano.

Nimepewa deal la kutafsiri kitabu cha Brian Green cha Fizikia kwenda kwenye Kiswahili.

Kabla sijakubali, inabidi nijue jinsi ya kutafsiri misamiati.

Niambie neno "quantum" kiswahili chake ni nini?

Niliishi Ulaya kwenye nchi zenye watu 2Milioni wenye lugha yao na kufundisha kwa kutumia lugha mpaka PhD. Nilichojifunza ni kuwa vocabularies nyingi wamehamisha kutoka kwenye Latin na kuzifanyia pronunciation zao.

Kwa mfano:

quadratic = Kvadratic
Equvailent = Ekvalencia
Quantum = Kvantum
Simulation = Simulacia
Function = Funkcia

Kiswahili kilifuata mfumo huu-huu wakati kinakuwa bila kutumia wataalamu

Kwa mfano:

shock absorber = shokomzoba
Check Line = Chekeleni
Sharia = Sheria
Ilmu = Elimu
Safr = Safari

Tatizo lililopo sasa ni kuwa wataalamu wa kiswahili wanatunga misamiati. Misamiati mingine ni vurugu tupu tuchukua mfano:

Mkokotoo - wakati kuna neno fanksheni linalotumika
Luninga - Wakati televisheni ingetosha kabisa
 
Kwa mantiki hiyo hiyo neno algorithm ambalo kina Kiranga na Bluray wanalitumia nalo asili yake sio Kiingereza:

algorithm |ˈalgəˌriðəm|nouna process or set of rules to be followed in calculations or other problem-solving operations, esp. by a computer : a basic algorithm for division.DERIVATIVESalgorithmic |ˌalgəˈriðmik| adjectivealgorithmically |ˌalgəˈriðmik(&#601😉lē| adverbORIGIN late 17th cent.: variant (influenced by Greek arithmos‘number' ) of Middle English algorism, via Old French from medieval Latin algorismus. The Arabic source, al- K wārizmī ‘the man of Kwārizm' (now Khiva), was the cognomen of the 9th-cent. mathematician Abū Ja‛far Muhammad ibn Mūsa.
 
Mkuu umeanza vizuri umehitimisha vibaya (umebolonga, to use your word) - lugha inayokuwa lazima iwe na visawe (synonyms); cheki:

Visawe Vipya Virasimishwe

Yuthi Visheni asante kwa kuendeleza dibeti hii. Hiyo hasa ndio misheni ya makala yangu ya wazi, yaani, kuendelea kuchochea mjadala wa kisera ila katika namna ambayo utaliangalia upya - kwa mtazamo wa Kiswanglishi - suala la lugha ya kufundishia ambalo linarudisha sana nyuma maendeleo yetu.

Kwenye Kiswahili kuna maneno yanaitwa 'Visawe'. Katika Kiingereza maneno haya yanaitwa 'Synonyms'. Kwa ufupi, visawe/synonyms ni maneno yenye maana sawa au maana zinazokaribiana sana. Lugha yoyote inayokua haijifungi kuwa na neno moja linalowakilisha kitu fulani. Hivyo unakuta lugha kama Kiingereza ina maneno kama (1) eat (2) consume (3) munch ambayo yote yana maana sawa au zinazokaribiana na yanaweza kutumika kuelezea tukio hilo hilo moja,yaani 'kula'. Kama unatumia Microsoft Word njia rahisi ya kuziona hizi synonyms ni kukliki/kubonyeza kitufe cha kulia cha mausi/mouse yako kwenye neno husika na utaona chaguo la 'synonyms' na ukilibofya hilo utapata hayo maneno mengine yenye maana sawa na hilo neno.

Matumizi haya ya visawe/synonyms utaona yanaonesha kuwa hoja yako hapo chini haikubaliani na hali halisi ya ukuaji wa lugha ya Kiswahili na matumizi yake la kila siku. Kiswahili unachokiongelea hapo chini, ambacho mimi nakiita 'Kiswanglishi' kinachochanganya maneno kukitofautisha na 'Kiswanglish' kinachochanganya lugha, kina visawe vingi tu. Hapa nina 'Kamusi ya Visawe: Swahili Dicitionary of Synonyms' iliyotungwa na Mohamed A. Mohamed & Said A. Mohamed na kuchapishwa hapa Afrika Mashariki na East African Educational Publishers. Kwa mujibu wa Dibaji yake, Kamusi hii ina visawe visivyopungua 71,000. Maneno ya Kiswahili yanayotupa hivi visawe ndio maneno hayo hayo tuliyochukua kwenye lugha za Kiarabu, Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi na kwenye lugha mbalimbali za Kiafrika. Ila kama nilivyosisitiza kwenye makala yangu ya wazi, kwa sasa tunachukua maneno mengi zaidi kutoka kwenye Kiingereza. Hivyo basi, sioni kwa nini tusitumie maneno hayo, yakiwemo ambayo ni visawe kama hivyo ulivyovitaja hapo chini, na kuvirasimisha ili tuvitumie kama sehemu ya lugha yetu ambayo kwa sasa inazidi kuwa Kiswanglishi kuliko ilivyo 'Kiswarabu'.

Nahitimisha hoja yangu kwa kutoa mifano kadhaa ya visawe na tofauti kati ya 'Kiswanglishi = Kiswahili' na 'Kiswanglish = Anglo-Kiswahili':

- Kiswanglish: Nakwenda kula chakula then I'll go to town alafu nitarudi kazini, of course I will see you there (Sentensi hii imechanganya lugha mbili)
- Kiswanglishi: Nakwenda kupata menu kisha nitaenda tauni alafu nitarudi jobu, naam tutaonana hapo (Sentensi hii inanyambulika Kibantu/Kiswahili)
- Visawe vya Kiswarabu: salimu,amkia, amkua sabahi, lahiki (maneno yote haya yana maana sawa na hutumika kwa kubadilishana)
- Visawe vya Kiswanglishi: televisheni, runinga, tivii (maneno yote haya yana maana sawa na huweza kutumika kwa kubadilishana)

CHANZO: UDADISI: Rethinking in Action: Kiswanglishi kiwe Lugha Rasmi ya Taifa

Mfano.

Nimepewa deal la kutafsiri kitabu cha Brian Green cha Fizikia kwenda kwenye Kiswahili.

Kabla sijakubali, inabidi nijue jinsi ya kutafsiri misamiati.

Niambie neno "quantum" kiswahili chake ni nini?

Kumbe hata hilo neno Kiingereza kimeazima kwenye Kilatini:

quantum |ˈkwäntəm|noun ( pl. -ta |-tə|)1 Physics a discrete quantity of energy proportional in magnitude to the frequency of the radiation it represents.• an analogous discrete amount of any other physical quantity, such as momentum or electric charge.• Physiology the unit quantity of acetylcholine released at a neuromuscular junction by a single synaptic vesicle, contributing a discrete small voltage to the measured end-plate potential.2 a required or allowed amount, esp. an amount of money legally payable in damages.• a share or portion : each man has only a quantum of compassion.ORIGIN mid 16th cent. (in the general sense [quantity] ): from Latin, neuter of quantus (see quantity ). Sense 1 dates from the early 20th cent.
 
Kwa mantiki hiyo hiyo neno algorithm ambalo kina Kiranga na Bluray wanalitumia nalo asili yake sio Kiingereza:

algorithm |ˈalgəˌriðəm|nouna process or set of rules to be followed in calculations or other problem-solving operations, esp. by a computer : a basic algorithm for division.DERIVATIVESalgorithmic |ˌalgəˈriðmik| adjectivealgorithmically |ˌalgəˈriðmik(&#601😉lē| adverbORIGIN late 17th cent.: variant (influenced by Greek arithmos‘number' ) of Middle English algorism, via Old French from medieval Latin algorismus. The Arabic source, al- K wārizmī ‘the man of Kwārizm' (now Khiva), was the cognomen of the 9th-cent. mathematician Abū Ja‛far Muhammad ibn Mūsa.

Companero

Miaka 200 au 300 kulikuwa hakuna mashule ulaya ya kufundisha kwa lugha za wazawa. Shule zilikuwa za makanisa na lugha iliyotumika ilikuwa Latin.
 
Naam sasa kama Kiingereza na lugha zingine zinafanya hivyo kwa nini sisi tuone kasumba kutofanya hivyo kwenye Kiswahili? Kwa nini tushindwe kusema kwantamu, astronomi,aljebra, algorizimu n.k? Tuache utumwa wa fikra!
 
Mkuu umeanza vizuri umehitimisha vibaya (umebolonga, to use your word) - lugha inayokuwa lazima iwe na visawe (synonyms); cheki:

Visawe Vipya Virasimishwe

Yuthi Visheni asante kwa kuendeleza dibeti hii. Hiyo hasa ndio misheni ya makala yangu ya wazi, yaani, kuendelea kuchochea mjadala wa kisera ila katika namna ambayo utaliangalia upya - kwa mtazamo wa Kiswanglishi - suala la lugha ya kufundishia ambalo linarudisha sana nyuma maendeleo yetu.

Kwenye Kiswahili kuna maneno yanaitwa 'Visawe'. Katika Kiingereza maneno haya yanaitwa 'Synonyms'. Kwa ufupi, visawe/synonyms ni maneno yenye maana sawa au maana zinazokaribiana sana. Lugha yoyote inayokua haijifungi kuwa na neno moja linalowakilisha kitu fulani. Hivyo unakuta lugha kama Kiingereza ina maneno kama (1) eat (2) consume (3) munch ambayo yote yana maana sawa au zinazokaribiana na yanaweza kutumika kuelezea tukio hilo hilo moja,yaani 'kula'. Kama unatumia Microsoft Word njia rahisi ya kuziona hizi synonyms ni kukliki/kubonyeza kitufe cha kulia cha mausi/mouse yako kwenye neno husika na utaona chaguo la 'synonyms' na ukilibofya hilo utapata hayo maneno mengine yenye maana sawa na hilo neno.

Matumizi haya ya visawe/synonyms utaona yanaonesha kuwa hoja yako hapo chini haikubaliani na hali halisi ya ukuaji wa lugha ya Kiswahili na matumizi yake la kila siku. Kiswahili unachokiongelea hapo chini, ambacho mimi nakiita 'Kiswanglishi' kinachochanganya maneno kukitofautisha na 'Kiswanglish' kinachochanganya lugha, kina visawe vingi tu. Hapa nina 'Kamusi ya Visawe: Swahili Dicitionary of Synonyms' iliyotungwa na Mohamed A. Mohamed & Said A. Mohamed na kuchapishwa hapa Afrika Mashariki na East African Educational Publishers. Kwa mujibu wa Dibaji yake, Kamusi hii ina visawe visivyopungua 71,000. Maneno ya Kiswahili yanayotupa hivi visawe ndio maneno hayo hayo tuliyochukua kwenye lugha za Kiarabu, Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi na kwenye lugha mbalimbali za Kiafrika. Ila kama nilivyosisitiza kwenye makala yangu ya wazi, kwa sasa tunachukua maneno mengi zaidi kutoka kwenye Kiingereza. Hivyo basi, sioni kwa nini tusitumie maneno hayo, yakiwemo ambayo ni visawe kama hivyo ulivyovitaja hapo chini, na kuvirasimisha ili tuvitumie kama sehemu ya lugha yetu ambayo kwa sasa inazidi kuwa Kiswanglishi kuliko ilivyo 'Kiswarabu'.

Nahitimisha hoja yangu kwa kutoa mifano kadhaa ya visawe na tofauti kati ya 'Kiswanglishi = Kiswahili' na 'Kiswanglish = Anglo-Kiswahili':

- Kiswanglish: Nakwenda kula chakula then I'll go to town alafu nitarudi kazini, of course I will see you there (Sentensi hii imechanganya lugha mbili)
- Kiswanglishi: Nakwenda kupata menu kisha nitaenda tauni alafu nitarudi jobu, naam tutaonana hapo (Sentensi hii inanyambulika Kibantu/Kiswahili)
- Visawe vya Kiswarabu: salimu,amkia, amkua sabahi, lahiki (maneno yote haya yana maana sawa na hutumika kwa kubadilishana)
- Visawe vya Kiswanglishi: televisheni, runinga, tivii (maneno yote haya yana maana sawa na huweza kutumika kwa kubadilishana)

CHANZO: UDADISI: Rethinking in Action: Kiswanglishi kiwe Lugha Rasmi ya Taifa

Wewe uchelewi kuboronga na kutupeka kwenye blog yako. Waswahili wanatumia neno fanksheni (function). Hakuna sababu ya mtaalamu wa kiswahili kupoteza muda kutuletea neno mkokotoo au mashine ya matendo.
 
Inabidi mimi na wewe tuanze. Nilijaribu hiyo project na watanzania fulani lakini baada ya muda nilibaki peke yangu.
 
Wewe uchelewi kuboronga na kutupeka kwenye blog yako. Waswahili wanatumia neno fanksheni (function). Hakuna sababu ya mtaalamu wa kiswahili kupoteza muda kutuletea neno mkokotoo au mashine ya matendo.

visawe ni muhimu, vinapanua wigo wa fikra na ubunifu - ukiwa na istilahi/misamiati mingi inakusaidia kupanuka kimawazo na kimtazamo
 
Mkuu umeanza vizuri umehitimisha vibaya (umebolonga, to use your word) - lugha inayokuwa lazima iwe na visawe (synonyms); cheki:

Visawe Vipya Virasimishwe

Yuthi Visheni asante kwa kuendeleza dibeti hii. Hiyo hasa ndio misheni ya makala yangu ya wazi, yaani, kuendelea kuchochea mjadala wa kisera ila katika namna ambayo utaliangalia upya - kwa mtazamo wa Kiswanglishi - suala la lugha ya kufundishia ambalo linarudisha sana nyuma maendeleo yetu.

Kwenye Kiswahili kuna maneno yanaitwa 'Visawe'. Katika Kiingereza maneno haya yanaitwa 'Synonyms'. Kwa ufupi, visawe/synonyms ni maneno yenye maana sawa au maana zinazokaribiana sana. Lugha yoyote inayokua haijifungi kuwa na neno moja linalowakilisha kitu fulani. Hivyo unakuta lugha kama Kiingereza ina maneno kama (1) eat (2) consume (3) munch ambayo yote yana maana sawa au zinazokaribiana na yanaweza kutumika kuelezea tukio hilo hilo moja,yaani 'kula'. Kama unatumia Microsoft Word njia rahisi ya kuziona hizi synonyms ni kukliki/kubonyeza kitufe cha kulia cha mausi/mouse yako kwenye neno husika na utaona chaguo la 'synonyms' na ukilibofya hilo utapata hayo maneno mengine yenye maana sawa na hilo neno.

Matumizi haya ya visawe/synonyms utaona yanaonesha kuwa hoja yako hapo chini haikubaliani na hali halisi ya ukuaji wa lugha ya Kiswahili na matumizi yake la kila siku. Kiswahili unachokiongelea hapo chini, ambacho mimi nakiita 'Kiswanglishi' kinachochanganya maneno kukitofautisha na 'Kiswanglish' kinachochanganya lugha, kina visawe vingi tu. Hapa nina 'Kamusi ya Visawe: Swahili Dicitionary of Synonyms' iliyotungwa na Mohamed A. Mohamed & Said A. Mohamed na kuchapishwa hapa Afrika Mashariki na East African Educational Publishers. Kwa mujibu wa Dibaji yake, Kamusi hii ina visawe visivyopungua 71,000. Maneno ya Kiswahili yanayotupa hivi visawe ndio maneno hayo hayo tuliyochukua kwenye lugha za Kiarabu, Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi na kwenye lugha mbalimbali za Kiafrika. Ila kama nilivyosisitiza kwenye makala yangu ya wazi, kwa sasa tunachukua maneno mengi zaidi kutoka kwenye Kiingereza. Hivyo basi, sioni kwa nini tusitumie maneno hayo, yakiwemo ambayo ni visawe kama hivyo ulivyovitaja hapo chini, na kuvirasimisha ili tuvitumie kama sehemu ya lugha yetu ambayo kwa sasa inazidi kuwa Kiswanglishi kuliko ilivyo 'Kiswarabu'.

Nahitimisha hoja yangu kwa kutoa mifano kadhaa ya visawe na tofauti kati ya 'Kiswanglishi = Kiswahili' na 'Kiswanglish = Anglo-Kiswahili':

- Kiswanglish: Nakwenda kula chakula then I'll go to town alafu nitarudi kazini, of course I will see you there (Sentensi hii imechanganya lugha mbili)
- Kiswanglishi: Nakwenda kupata menu kisha nitaenda tauni alafu nitarudi jobu, naam tutaonana hapo (Sentensi hii inanyambulika Kibantu/Kiswahili)
- Visawe vya Kiswarabu: salimu,amkia, amkua sabahi, lahiki (maneno yote haya yana maana sawa na hutumika kwa kubadilishana)
- Visawe vya Kiswanglishi: televisheni, runinga, tivii (maneno yote haya yana maana sawa na huweza kutumika kwa kubadilishana)

CHANZO: UDADISI: Rethinking in Action: Kiswanglishi kiwe Lugha Rasmi ya Taifa

Mkuu ingawa si mtaalamu wa lugha na sina hiyo nafasi ya kutafuta hata nyenzo kwa hapa (online) kwakuwa makarabasha husika ya kunipleka on point hayapo, hila huyo jamaa anachanganya maana ya visawe (as in synonyms).

Anachozungumzia yeye hiyo ni assimilation ya lugha into the current language, kwakuwa hayo maneno bado hayapo kwenye kamusi ya kiswahili na bado kutambulika kama maneno ya kiswahili that is referred as an assimilation process. Synonyms ni maneno ambayo yapo tayari kwenye lugha and they are universally used na pengine wengi hata hawajui asili yake na si yote lazima yawe ya kigeni mengine ni kwa sababu ya maana zake tu kwenye kuelezea vitu vingine.

Lugha yetu inahitaji serious scholars kuipekuwa na kujua vyanzo vyake na uzuri wake tuna lugha nyingi za kibantu ambazo bado zipo hai kuweza kutusaidia hivyo kuanzia Tanzania mpaka Zimbabwe.
 
Back
Top Bottom