mzamifu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2010
- 6,400
- 3,853
wanaotetea kufundisha kwa kiswahili wanasema wanafunzi wataelewa zaidi kuliko kwa kiingereza wengine wanasema ni kuenzi utamaduni. hilo la kwanza sidhani kama ni sahihi maana kwa miaka yote watanzania wamekuwa wakipata elimu kwa kiingereza hapa nchini na nje ya nchi na wengi wanatenda kazi vizuri tu. tatizo la sasa la kiingereza linatokana na mfumo mbaya uliobomoa si kiingereza tu bali elimu kwa ujumla. hilo la utamaduni ni finyu maana karibu kila kitu tunachotumia hakina asili yetu; mavazi, vyombo vya usafiri, tv, redio hata elimu yenyewe sasa na hivi tuviache?. wakati dunia inazidi kuwa moja ni makosa kufikiri kuwa kiingereza si sehemu ya utamaduni wa dunia kwa sasa ambamo tumo.
kinachotakiwa kuondoa ni zile sababu zilizofanya kiingereza kishuke na elimu itetereke kama wingi wawanafunzi darasani, uandaaji mbovu wa walimu, uhaba wa vifaa n.k Angalia Rwanda imeamua kutumia kiingereza katika elimu na wanaenda vizuri sisi tunacho tayari lakini tunataka kukitupa eti ndipo tutapata kukielewa zaidi hizo ni ndoto za mchana. wanaotaka kufundisha kwa kiswahili waanzishe shule zao waanze kama majaribio. tena tukiamua kufundisha kwa kiswahili ndipo shule za English medium zitazidi kuongezeka na wanaoshabikia watawapeleka watoto wao huko. taifa litazidi kuparaganyika kwa matabaka.