Mzee Kipara
Member
- Jan 3, 2011
- 83
- 43
Kwa sababu mpaka leo hatuna maandiko yetu. Unaandika kwa kutumia alphabet ya warumi.
Kwa sababu hatuna umeme tuliovumbua, unatumia umeme kwa hisani ya Wamarekani.
Kwa sababu hatuna internet yetu, hapo unapojitutumua na kudai tuandike vitabu vyetu unasema hivyo kwa kutumia herufi za Warumi, umeme wa Wamarekani, Kompyuta sijui ya watu gani lakini si yetu, inernet mostly ya Wamarekani.
Bora hao Wajerumani wenye lugha yao na kumthamini Goethe. Sie leo mtoto anamaliza Chuo Kikuu hajui sio tu Kiingerea, bali hata Kiswahili.
Na "Usilogwe kumuuliza kama kashawahi kusikia kitu kinaitwa "Maisha Yangu Baada Ya Miaka Hamsini".
Huyo baba wa Taifa aliyejua umuhimu wa utaifa kabla ya kuwepo kwa taifa, na kulijenga taifa kutoka makabila, na kuchukia ukoloni, na kujua umuhimu wa Kiswahili katika yote haya, bado alitafsiri "Mabepari wa Venisi". Bado unasema kutafsiri vitabu vya lugha nyingine kwenda kwenye Kiswahili hakuhitajiki?
Umesoma historia ya China na kujua kisa kilichofanya China iliyokuwa imeendelea kisayansi kuliko Ulaya ipitwe na Ulaya kimaendeleo ni kitu gani?
Unajua tofauti ya usomi uliofunguka na ujivuni majununi?
Nikikusoma tena naona post yako inavyoanza na inavyoisha inajipinga yenyewe.
Incoherence.
Hujui unkwenda au unarudi. Napata shaka kuelewa kama kweli unamuunga mkono mleta mada au la. Kwa sababu sina hakika unajua uko wapi wewe mwenyewe.
Hata maswali yako uliyoanza nayo hayaeleweki kama ni rhetoric au la!
Point yangu ni kwamba ingawa Ujerumani wanatumia Kijerumani kama medium of instruction lakini Kiingereza pia kinatumika indirectly kama medium of instruction, kwa sababu wanafunzi wanasoma pia vitabu vilivyoandikwa kiingereza ili kujibu mtihani. Na mimelisema hilo kuonyesha nafasi ambayo kingereza kinapewa kwenye education systems za nchi ambazo watu wamekariri zimeendelea na haziweki msisitizo kwenye Kiingereza.
Mtoa maada ametahadhalisha kwamba swala la kusisitiza kiswahili kishike hatamu bila kuweka mikakati ya watu kuweza kumudu English pia itatufisha sipo. Na ndicho nilichosapoti, na ili tuweze kujua kiingereza vizuri, lazima tuwe na program zinazoendeshwa kwa kiingereza katika elimu na maisha kwa ujumla, hiyo siyo ulimbukeni, nchi nyingi zinafanya hivyo, ikiwa ni pamoja na hizo mnazozisema zimeendelea bila kiingereza.
Kwa mfano huwa najiuliza, kwa nini TV zetu hamna inayorudia taarifa ya habari kwa kiingereza, ITV walikuwa wanafanya hivyo wakaacha. Najua watu mtasema ni ulimbukeni, lakini nchi nyingi huwa wanafanya hivyo. Ni vizuri kuenzi kiswahili chetu, lakini hiyo haimaanishi tusiweke juhudi za kujua kiingereza.
Na nikuulize swali, tumetumia kiswahili kama lugha ya kufundishia kwenye shule za msingi kwa miaka 40 au 50 sasa, unafikiri wahitimu wetu wa shule ya msingi wanakuwa na uelewa mkubwa wa mambo kuliko wa Kenya ambao wanatumia Kiingereza?