Tanzania na siasa: Lugha ya kutumia Kiswahili au Kiingereza, Tatizo lipo wapi?

Tanzania na siasa: Lugha ya kutumia Kiswahili au Kiingereza, Tatizo lipo wapi?

Kwa sababu mpaka leo hatuna maandiko yetu. Unaandika kwa kutumia alphabet ya warumi.

Kwa sababu hatuna umeme tuliovumbua, unatumia umeme kwa hisani ya Wamarekani.

Kwa sababu hatuna internet yetu, hapo unapojitutumua na kudai tuandike vitabu vyetu unasema hivyo kwa kutumia herufi za Warumi, umeme wa Wamarekani, Kompyuta sijui ya watu gani lakini si yetu, inernet mostly ya Wamarekani.

Bora hao Wajerumani wenye lugha yao na kumthamini Goethe. Sie leo mtoto anamaliza Chuo Kikuu hajui sio tu Kiingerea, bali hata Kiswahili.

Na "Usilogwe kumuuliza kama kashawahi kusikia kitu kinaitwa "Maisha Yangu Baada Ya Miaka Hamsini".

Huyo baba wa Taifa aliyejua umuhimu wa utaifa kabla ya kuwepo kwa taifa, na kulijenga taifa kutoka makabila, na kuchukia ukoloni, na kujua umuhimu wa Kiswahili katika yote haya, bado alitafsiri "Mabepari wa Venisi". Bado unasema kutafsiri vitabu vya lugha nyingine kwenda kwenye Kiswahili hakuhitajiki?

Umesoma historia ya China na kujua kisa kilichofanya China iliyokuwa imeendelea kisayansi kuliko Ulaya ipitwe na Ulaya kimaendeleo ni kitu gani?

Unajua tofauti ya usomi uliofunguka na ujivuni majununi?

Nikikusoma tena naona post yako inavyoanza na inavyoisha inajipinga yenyewe.

Incoherence.

Hujui unkwenda au unarudi. Napata shaka kuelewa kama kweli unamuunga mkono mleta mada au la. Kwa sababu sina hakika unajua uko wapi wewe mwenyewe.

Hata maswali yako uliyoanza nayo hayaeleweki kama ni rhetoric au la!

Point yangu ni kwamba ingawa Ujerumani wanatumia Kijerumani kama medium of instruction lakini Kiingereza pia kinatumika indirectly kama medium of instruction, kwa sababu wanafunzi wanasoma pia vitabu vilivyoandikwa kiingereza ili kujibu mtihani. Na mimelisema hilo kuonyesha nafasi ambayo kingereza kinapewa kwenye education systems za nchi ambazo watu wamekariri zimeendelea na haziweki msisitizo kwenye Kiingereza.

Mtoa maada ametahadhalisha kwamba swala la kusisitiza kiswahili kishike hatamu bila kuweka mikakati ya watu kuweza kumudu English pia itatufisha sipo. Na ndicho nilichosapoti, na ili tuweze kujua kiingereza vizuri, lazima tuwe na program zinazoendeshwa kwa kiingereza katika elimu na maisha kwa ujumla, hiyo siyo ulimbukeni, nchi nyingi zinafanya hivyo, ikiwa ni pamoja na hizo mnazozisema zimeendelea bila kiingereza.

Kwa mfano huwa najiuliza, kwa nini TV zetu hamna inayorudia taarifa ya habari kwa kiingereza, ITV walikuwa wanafanya hivyo wakaacha. Najua watu mtasema ni ulimbukeni, lakini nchi nyingi huwa wanafanya hivyo. Ni vizuri kuenzi kiswahili chetu, lakini hiyo haimaanishi tusiweke juhudi za kujua kiingereza.

Na nikuulize swali, tumetumia kiswahili kama lugha ya kufundishia kwenye shule za msingi kwa miaka 40 au 50 sasa, unafikiri wahitimu wetu wa shule ya msingi wanakuwa na uelewa mkubwa wa mambo kuliko wa Kenya ambao wanatumia Kiingereza?
 
Maelezo yako yamenigusa sana, yaani kila nikisoma Wimbo Ulio Bora, Mhubiri na Mithali za Sulemani mwenye Hekima zilivyotafsiriwa kwa umakini wa hali ya juu nashindwa kuelewa Wamishonari waliwezaje kuwa na upeo mubwa wa lugha yetu kiasi hicho, naishia kujiambia kuwa labda ulikuwa ni Uvuvio tu!

1 Wimbo ulio bora, wa Sulemani.
2 Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai;
3 Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda.
4 Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutazinena pambaja zako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.
5 Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.
6 Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
7 Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa kidoto, Karibu na makundi ya wenzako?
8 Usipojua, wewe uliye mzuri katika wanawake, Shika njia uzifuate nyayo za kondoo, Na kuwalisha wana-mbuzi wako Karibu na hema za wachungaji.
9 Mpenzi wangu, nimekulinganisha Na farasi katika magari ya Farao.
10 Mashavu yako ni mazuri kwa mashada, Shingo yako kwa mikufu ya vito.
11 Tutakufanyizia mashada ya dhahabu, Yenye vifungo vya fedha.
12 Muda mfalme alipoketi juu ya matakia, Nardo yangu ilitoa harufu yake.
13 Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemane Ukilazwa usiku maziwani mwangu.
14 Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina, Katika mizabibu huko Engedi.
15 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua.
16 Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;
17 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi.
 
Wanasema mjerumani alichukua mtaala wake wa ujerumani na kuufundisha kwa kiswahili. Na kwa muda mfupi native walifanya kazi zote stadi.
 
Inaonekana tunakubaliana, ila una incoherence tu inayosababishwa na maswali uliyoanza nayo kwenye previous post, ambayo hujajibu swali langu bado kwamba yalikuwa rhetorical or not kwa sababu yanapinga habari yako ya kutaka jitihada za kukuza Kiswahili ziende sambamba na jitihada za kukuza Kiingereza, kitu ambacho nakubaliana nacho.

Nisichoelewa ni kwa nini mtu mwenye maoni haya apinge kutafsiri vitabu kutoka Kiingereza kwenda kwenye Kiswahili.

Mie mwenyewe nilivyokuwa mdogo nilitamani sana kuwepo na vitabu vingi vilivyotafsiriwa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, partly kwa sababu nilikuwa najifunza kiingereza mwenyewe kwa kulinganisha maneno kati ya kitabu cha kiingereza na tafsiri yake ya Kiswahili, hivyo kujenga msamiati. Kwa hiyo naelewa umuhimu wa tafsiri from personal experience, na najua kuna watoto wengi walio katika ile stage niliyokuwapo ambao wangeweza kufaidika sana na tafsiri zaidi, sio tu kujifunza kiingereza, bali pia hata kujifunza kiswahili na kujifunza kuangalia jambo moja kwa lugha mbili tofauti.

Sijaelewa kwa nini umeliwekea maswali hili jambo la kutafsiri vitabu bado.

Halafu hujanijibu swali langu la kwamba, kama hutaki kutafsiri vitabu vya wengine, unataka tutunge vyetu kila kitu, kwa nini unatumia herufi za wengine, internet ya wengine, umeme wa wengine etc?

You seem to be holding two distinct positions at the same time. One allowing for a multicultural/ multilingual tradition where you attempt some semblance of upholding the importance of learning english, and another, at the same time and contradictory, introvertly closed to translating english books into swahili. You can't eat your cake and have it too.

Unless you are operating in the quantum world.

Which brings me back to the question by the way.

What is quantum in Swahili?
 
Sir, I am not going to come here and claim to be an expert in particle physics, you are telling us now about quantum ideas yet you asked for the translation of the word quantum in Swahili if it existed.

Which is which, my answer was based on the closest translation the word quantum could be translated into Swahili. Hayo ya ma-wave simo sio kwamba siyataki hila siyajui huo ndio ukweli wenyewe.

Habari ndo hiyo, kama unayajua, huyajui, unayajua na huyajui, unayajua au huyajui, au hata kama hujui kama unayajua au huyajui.
 
Tatizo la elimu yetu siyo lugha ni mfumo wa elimu wenye kuaandaa walimu kwa kauli mbiu hii: 'umekosa hata pointi 28 za kukuwezesha hata kwenda ualimu?', walimu wetu wengi ni div. IV ni mara chache sana kukutana na mwalimu aliyepata div. I kidato cha nne, hapa inaonekana jinsi ambavyo serikali haijali elimu yetu.

Maoni yangu: fani ya ualimu ipewe uzito wake, walimu taraja wawe ni wale wenye pass za juu kama vyuo vikuu, mishahara iboreshwe, elimu yetu itaimarika kwa kutumia Kiswahili na English kama ilivyo sasa.
 
hayo mawili wawindaji lazima wana maneno yao na hilo la mwisho lazima walevi wana maneno yake

yeah,ila yatakuwa ktk mainstream language?Wawindani hutumia neno lolote linaloanzishwa na mwenzao, wale professionals wengi hutumia lugha za wageni wanaoshiriki nao ktk uwindaji husika kufanikisha uwindaji huo.Hata walevi wana misemo yao kutokana na circle yao.
 
Maelezo yako yamenigusa sana, yaani kila nikisoma Wimbo Ulio Bora, Mhubiri na Mithali za Sulemani mwenye Hekima zilivyotafsiriwa kwa umakini wa hali ya juu nashindwa kuelewa Wamishonari waliwezaje kuwa na upeo mubwa wa lugha yetu kiasi hicho, naishia kujiambia kuwa labda ulikuwa ni Uvuvio tu!

1 Wimbo ulio bora, wa Sulemani.
2 Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai;
3 Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda.
4 Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutazinena pambaja zako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.
5 Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.
6 Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
7 Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa kidoto, Karibu na makundi ya wenzako?
8 Usipojua, wewe uliye mzuri katika wanawake, Shika njia uzifuate nyayo za kondoo, Na kuwalisha wana-mbuzi wako Karibu na hema za wachungaji.
9 Mpenzi wangu, nimekulinganisha Na farasi katika magari ya Farao.
10 Mashavu yako ni mazuri kwa mashada, Shingo yako kwa mikufu ya vito.
11 Tutakufanyizia mashada ya dhahabu, Yenye vifungo vya fedha.
12 Muda mfalme alipoketi juu ya matakia, Nardo yangu ilitoa harufu yake.
13 Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemane Ukilazwa usiku maziwani mwangu.
14 Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina, Katika mizabibu huko Engedi.
15 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua.
16 Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;
17 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi.
Inafurahisha na inatia moyo na fahari sana kupata watu wasomi kama nyinyi.Kwanza mawazo yako kuwa na sehemu nyingi za kuona mafanikio ya lugha ni mfano mwema kuwa unasoma na kulinganisha mambo mengi na hivyo akili yako ina maeneno mengi ya kupitia kabla hujatoa maamuzi.

Watu wengi wasingeona ustadi wa tafsiri ya Biblia ,pamoja na maeneo ya kisayansi ulitopitia hapo juu.

NImependa hapo juu nilipoweka nyekundu.Sijui alikuwa mnubi wa sudan au ethiopia enzi hizo.Inatia moyo kuwa watu weusi pia walipata positivie remarks,ingawa inaelekea kulikuwa na watu waliotazama tofauti.ndio maan hiyo aya ikawa inasisitiza.

Wajerumani ndio walikichukua kiswahili kwenda kwenda kwenye level nyingine.Walikirekebisha na kukijenge tarakimu,otherwise kingeweza tumia tarakimu za kiarabu.Au kila mtu angeandika kivyake.Historia inatueleza wajerumani walijikutaw akitumia kiswahili kuwasilina na watu wa makabila mengi, na mara nyingine kuwasiliana na wakoloni wengine wanaozungumza lugha nyingine.
 
Hii inadhihirisha tu usemi kwamba sisi Waafrika hakuna kitu tunaweza kufanya, nakuhakikishia kama Tanzania ingekuwa bado inatawaliwa na Wazungu (Wajerumani) ambao ndio walileta mfumo wa kutumia Kiswahili mashuleni (sio sisi) leo hii tungekuwa tunatumia Kiswahili kuanzia chekechea mpaka Elimu ya juu, lakini kwa bahati mbaya Mungu hakutupenda sana wakaondoka mapema bila kuendelea kutuelimisha kwa Lugha yetu wenyewe leo hii zaidi ya miaka 100 baadaye tunapinga kwa nguvu zote Lugha (yetu wenyewe na hii utaiona Afrika tu) iliyotufundisha Neno La Mungu!

Wajerumani waliweza kwa vile kijerumani kinachoongelewa leo si natural sana, kwa kiasi fulani ni lugha artificial,iliyotengenezwa na wasanii na wataalamu wa literature.

Hawa jamaa wana masomo fulani la lugha na tamaduni yanayopata support ya mbinu za kisayansi.Na hivyo kuwasaidia sana kukuza lugha yao ambayo inajitahidi kwenda sambamba namabadiliko ya dunia.Kwetu wengi wa wataalamu wa kiswahili hawakupenda sana kuwa na fani nyingine ambayo ingewasaidia sana katika maeneo fulani ya lugha na tafiti.

Kwa ujumla sijapenda sana Dinosours wote kuitwa "mijusi" kibaiologia si kweli, kwani kuna wengine walikuwa wakipaa, wengine wakiwa na tabia zinazoambatana na wanyama na viumbe wengi tuu.
Na mwisho kuna nchi nyingi sana za Kiafrika zinatumia Kiingereza kabisa, Je hali yao ya kimaendeleo ikoje? kama hali yao ni bora sana kuliko yetu nikimaanisha kwamba hawaibiwi kwenye Mikataba kama sisi au hawauzi rasilimali zao kama sisi kwa kuwa wanatumia Kiingereza na hivyo kuelewa kilichoandikwa kwenye mikataba, basi hoja yako inaweza kuwa na maana kidogo lakini SI KWELI Nigeria bado wanaibiwa ingawaje wanatumia kiingereza Ghana bado wanaibiwa rasilimali ingawaje wanatumia iingereza, Uganda bado, Kenya bado n.k HIVYO TATIZO SIO KISWAHILI

kauli yako ina mantiki ila imekuwa ya jumla sana.Ktk mikataba mibovu kuna factor nyingi sana kama ilivyo kwa mchezaji na mafanikio yake uwanjani na nje ya uwanja.

Kuna masuala mengine yanayoweza changia kuharibu mikataba.Watu kuna kufanya makosa makusudi n akuna kufanya makosa kwa kutokujua kabisa, na kuna makosa yatokanayo na kutojua vya kutosha kuweza push mambo zaidi ili kupata kadiri iwezekanavyo.Huko kwa makusudi kunaweza sababishwa na rushwa,kuwa ktk hali mbaya kiuchumi na kiushindani na hivyo kila dili inayokuja ni dili angalau kupata quick fix,hata kama kwa muda mrefu ni hasara.

Tanzania inaweza kuwa ina matatizo hayohayo ila udhaifu wa kusoma kwa umakini mikataba au hata kutokuwa na weledi wa lugha kiasi cha kustushwa na baahi ya vipengele ni tatizo kubwa.Pia ubabaishaji ktk mambo yetu nis shida.Hembu sikiliza habari ya Wahadhiri wa vyuo wanaosema "mwana chuo hana shida mfundisha, mpe zoezi na references halafu mtangazie test "

Kama kiingereza ni maendeleo nchi kama Jamaika na nyinginezo wote 100% wanatumia Kiingereza lakini bado ndio wa mwisho kwa Umaskini katika bara la Marekani na wanapitwa na nchi ambazo watu wao hawajuia kiingeza kabisa kama Venezuela, Brazilii ambayo wanatumia Kireno, sasa sijui hoja yako iko wapi?
Jamaica imeharibiwa sana na kujisahahu ktk movements za black people hata baada ya mambo kubadilika, social structure ya jamaica na Haiti haikuwa nzuri kama ilivyo Zenj leo.Ni ngumu sana kuwa na common platform ambayo itakuwa base ya kujenga maendeleo.

Brazil na venezuela imekuzwa na mabepari, waliokuwa na mitaji kwa miaka mingi, pamoja na kuibuka kwa masoko ktk rasilimali za nchi mafuta, misitu, kilimo na watu wa kufanya tafiri ktk maeneo ya afya na kilimo.N akireno si lugha dhaifu.Kireno tayari kilikuwa ktk maandiko ya tafiti,literature, culture etc, hata manuals za machine ambazo ureno walikuwa walitengeneza.

Tofauti na Kiswahili ambacho kimejikita kataka maeneo fulani ya utamaduni, na elimu.
Labda tunahitaji wazungu waje tena na sijui safari hii watatumia mbinu gani kuja kutuelimisha na kutuambia kwamba tunaweza kutumia Kiswahili na tukaendelea lakini kwa bahati mbaya bahati haiji mara mbili tuliipata mara ya kwanza toka kwa Wamisionari.
Sasa hivi dunia inakimbia sana, mabadiliko ya dunia yanafanya lugha nyingine kuwa muhimu leo, kesho si muhimu.Kila nchi inahitaji kuwa na flexibility ya kutumia faida za muda zitokanazo na hayo maendeleo.Nchi ziongeavo lugha mbili kama cameroun, swiss etc huwa wananchi wake wanajikuta kila mara lugha fulani inakuwa si kipaumbele.Supporse sasa hivi umuhimu wa kichina unaanza onekana,taifa haliwezi puuza hayo.Na hii si kudhalilisha Kiswahili bali ni kuliweka taifa ktk mazingira ya kukama kila fursa inayopatikana.Sasa hivi wamarekani wanahimiza watu wao kujua kichina,hii ni kwa sababu wanajua uchumi wa china sasa hivi ni muhimu kuliko Ulaya yote,na kusitawi kwao kunategemea sana jinsi watakavyoilewa china,jinsi watakavyotumia kila nafasi.Hasa kufanya kila thamani yao kuwa diplomasia.Tanzania hatujafikia huko kwani hatuna sera ya kitaifa,hatuna raisa wanaowajibika ktk nchi popote walipo.hakuna watu wenye kufanya mambo yanayofanya kiswahili kuwa silaha yetu.

Suala la kupata fursa na kuzitumia kikamilifu kabla hazitoweka au hata kuweza ziongeza inategemea na jinsi nchi inaweza kuwa na upana ktk kujua tamaduni za nchi husika ambazo kwa kiasi fulani zinabebwa na lugha.

English ni kama njia panda ambapo ni mahali sahihi pa kusubiri watu wanaotoka njia nyingi ambazo hujui ni ipi atatoka.Uwezekano wa vitu muhimu kupata tafsiri ya mwanzo kwenda kiingereza ni mkubwa sana.

Believe me ktk kichagga kuna maneno ambayo kiswahil hakina,ingawa nao wachaga wamedrop maneno mengi na kuingiza ya kiswahili, hivyo kufanya lugha ianze fanana na kiswahili.
 
Tatizo la elimu yetu siyo lugha ni mfumo wa elimu wenye kuaandaa walimu kwa kauli mbiu hii: 'umekosa hata pointi 28 za kukuwezesha hata kwenda ualimu?', walimu wetu wengi ni div. IV ni mara chache sana kukutana na mwalimu aliyepata div. I kidato cha nne, hapa inaonekana jinsi ambavyo serikali haijali elimu yetu.

Maoni yangu: fani ya ualimu ipewe uzito wake, walimu taraja wawe ni wale wenye pass za juu kama vyuo vikuu, mishahara iboreshwe, elimu yetu itaimarika kwa kutumia Kiswahili na English kama ilivyo sasa.

Pia Tatizo ni kwamba hatufanyi vitu muhimu katika maisha with passion,passion inaongeza curiousity, na willingness ya kutafuta the best way tunaweza present tunachokijua na kuweza tafuta feedback ya mafanikio ya tulichofanya.Mwalimu anayo nafasi kubwa sana ya kufanikiwa ktk uandishi, ktk taaluma na kazi nyingine za kijamii kama atawezekeza ktk fani yake vyema na mwishowe kufanikiw asana kiuchumi.Ila kwa sasa wanataka waboreshewe Mishahara bila wao kuwa tayari kuboresha mbinu zao za ufundishaji, utendaji wao kazini.sasa sijui kama wao hawataki kuwa wa kwanza nani atakuwa wa kwanza?Kwanza hadi sasa ukiangalia wanacholipwa na wanachoweka katika kazi wengi ni wezi wa mali za umma.

haina tofauti na wachezaji wa Tanzania wanodai kuwa malipo yao sijui yaboreshwe wanagomea mazoezi bila jijua kuwa wanajizua kuenda mbali ktk soko la soka wakidhani kuwa wana komoa timu zao.Kumbe wanapoteza muda na kujifelisha kwenda walipo akina Messi.NI kama kupoteza muda kubishania mambo ktk nyumba ya kupanga.
 
Sir, I am not going to come here and claim to be an expert in particle physics, you are telling us now about quantum ideas yet you asked for the translation of the word quantum in Swahili if it existed.

Which is which, my answer was based on the closest translation the word quantum could be translated into Swahili. Hayo ya ma-wave simo sio kwamba siyataki hila siyajui huo ndio ukweli wenyewe.

Nadhadhani translation ni vizuri ikapunguza kuwa description kadiri iwezekanavyo,nadhania ndicho unamaanisha?Hata mimi nimekuwa na shida sana na kiswahili,pengine ni kwa vile nilishaachana na kufuatilia sana misamiati yake.Ila mara nyingi translation ya maneno ya kiingereza au kisayansi kuja kiswahili in maelezo ya kitu na si mapping ya neno kwa neno.
 
uwezekano wa Kiswahili kufanikiwa hapa ni mdogo sana kutokana na jinsi tunavyoendesha mambo. Ni lazima tuwe na unique products au technology au kitu chochote ambacho dunia ikiwa inajitahidi kukitafuta ilazimike kujifunza lugha yetu
Juzi nimeona bungeni wanaongelea masuala ya kamisheni ya kiswahili na wabunge wetu wanachekelea kuwa sasa zitapatikana nafasi za watanzania kwenda kuwafundisha kiswahili wengine huko nje. Wakati wakiongea bungeni wakenya tayari wameshasambaa dunia nzima na 'tuisheni' zao za kiswahili wakisubiria kivi- legalize kupitia hii sheria tunayotunga sasa. Sababu kubwa hapa ni kuwa huwezi kumfundisha mtu kiswahili bila uelewa wa lugha ya 'mwanafunzi' (ambayo mara nying ni English)
Kweli Tanzania tuna matatizo mengi, fikiria haya"

  • Jina Tanzania sio jina halisi la nchi bali lilibuniwa kutoka kusikojulikana
  • Mipaka yetu haijulikani vizuri - Kenya wanataka Kilimanjaro, Uganda - eneo la mutukula, Malawi - ziwa nyasa nk
  • Kiswahili chenyewe - 40% Arabic, 20% Kijerumani, 20% Kiingereza, 10% Makabila ya kibantu
yaani taabu tu
 
Mfano.

Nimepewa deal la kutafsiri kitabu cha Brian Green cha Fizikia kwenda kwenye Kiswahili.

Kabla sijakubali, inabidi nijue jinsi ya kutafsiri misamiati.

Niambie neno "quantum" kiswahili chake ni nini?

Katika lugha ni rukhsa kuazima maneno kutoka lugha moja kwenda nyengine na kuyaandika kwa kutumia lugha yenu. Mfano neno "schule" kwa Kijerumani maana yake ni "shule" kwa Kiswahili. Sasa kwa nini quantum isiwe kwantum(u)?
 
Kwa sababu Kiswahili kina sifa ya kuwa phonetic, na kwantam ni phonetic zaidi.

We make this as we go along, sijaona neno rasmi bado.
 
Mfano.

Nimepewa deal la kutafsiri kitabu cha Brian Green cha Fizikia kwenda kwenye Kiswahili.

Kabla sijakubali, inabidi nijue jinsi ya kutafsiri misamiati.

Niambie neno "quantum" kiswahili chake ni nini?

Unaadika Qwantam, unakopa kidogo. teh teh...............
 
Kwa sababu Kiswahili kina sifa ya kuwa phonetic, na kwantam ni phonetic zaidi.

We make this as we go along, sijaona neno rasmi bado.

There is nothing wrong with making it as we go along. Kiswahili bado ni lugha changa na yenye nafasi kubwa ya kukua. Kama physics ni fizikia basi sioni kwa nini iwe shida kwa quantum kuwa kwantum au kwantam kama ulivyoiweka. Ngoja nifungue TUKI yangu hapa nione wao wametafsiri vipi.
 
Inaonekana tunakubaliana, ila una incoherence tu inayosababishwa na maswali uliyoanza nayo kwenye previous post, ambayo hujajibu swali langu bado kwamba yalikuwa rhetorical or not kwa sababu yanapinga habari yako ya kutaka jitihada za kukuza Kiswahili ziende sambamba na jitihada za kukuza Kiingereza, kitu ambacho nakubaliana nacho.

Nisichoelewa ni kwa nini mtu mwenye maoni haya apinge kutafsiri vitabu kutoka Kiingereza kwenda kwenye Kiswahili.

Mie mwenyewe nilivyokuwa mdogo nilitamani sana kuwepo na vitabu vingi vilivyotafsiriwa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, partly kwa sababu nilikuwa najifunza kiingereza mwenyewe kwa kulinganisha maneno kati ya kitabu cha kiingereza na tafsiri yake ya Kiswahili, hivyo kujenga msamiati. Kwa hiyo naelewa umuhimu wa tafsiri from personal experience, na najua kuna watoto wengi walio katika ile stage niliyokuwapo ambao wangeweza kufaidika sana na tafsiri zaidi, sio tu kujifunza kiingereza, bali pia hata kujifunza kiswahili na kujifunza kuangalia jambo moja kwa lugha mbili tofauti.

Sijaelewa kwa nini umeliwekea maswali hili jambo la kutafsiri vitabu bado.

Halafu hujanijibu swali langu la kwamba, kama hutaki kutafsiri vitabu vya wengine, unataka tutunge vyetu kila kitu, kwa nini unatumia herufi za wengine, internet ya wengine, umeme wa wengine etc?

You seem to be holding two distinct positions at the same time. One allowing for a multicultural/ multilingual tradition where you attempt some semblance of upholding the importance of learning english, and another, at the same time and contradictory, introvertly closed to translating english books into swahili. You can't eat your cake and have it too.

Unless you are operating in the quantum world.

Which brings me back to the question by the way.

What is quantum in Swahili?

Tunatumia herufi za kirumi kama ulivyosema, hatukuzibadlisha, ziko vilevile, tufanye hivyohivyo kwenye vitabu vilivyoandikwa kwa kiingereza, tuvitumie vikiwa hivyo hivyo. Swala hapa sipingi kutumika kwa vitabu na tekinolojia za watu wengine. Tusipende miteremko na shortcuts, kutaka vitabu vilivyoandikwa kwa kiswahili ni jambo jema, tutunge vya kwetu.

Hiyo point unayosema ya kujifunza kiingereza kwa kukaa na vitabu viwili (kilichoandikwa kwa kiswahili na kilichoandikwa kwa kiingereza) ni irrelevant, hiyo ni the most ineffective way ya kujifunza lugha, lugha huwa haifundishwi kwa kufanya direct translation kutoka lugha unayojifunza kwenda lugha unayoijua. Ndiyo maana mwalimu anayefundisha English au French huwa haruhusiwi kutumia lugha nyingine darasani zaidi ya hiyo anayoifundisha. Kama unataka kujifunza kwa direct translation si uchukie English-Swahili dictionary tu.

Kuhusu swali lako la what is quntum in Kiswahili, mimi sijui, tuna balaza la kiswahili Tanzania (BAKITA) ambayo ni taasisi iliyoundwa kukuza kiswahili, kama neno quantum halina kiswahili ni jukumu lao kulitengenezea neno la kiswahili.
 
Kwanza nikupe heko mtoa mada. Mojawapo ya matatizo makubwa tuliyonayo Tanzania ni kutafuta njia rahisi kutatua matatizo magumu. Kiukweli wengi wetu lugha hizi zote mbili hatuzifahamu ipasavyo, yaani tunababia babia tu iwe kisw au kiing. Na matokeo yake ndio kuchanganya lugha kusiko na maana. Tutatue kwanza tatizo hili jamani. Kiingereza hatuwezi kukiepuka hata kidogo kama tunataka kasi ya maendeleo yetu iwe ya maana. na hatuwezi kufikia huko kama tunaridhika tu kukariri misamiati michache ya kiingereza na kuitupia tupia tu kwenye mazungumzo ili kuwatisha watu! Na kwa vile lugha zote hatuzijui kikamilifu, ndio maana tunatafuta nafuu katika kuondoa moja au sijui kufanya nini. Tufikirie vizuri, turekebishe mitaala yetu na hapo ndio tutakuwa kwenye mstari safi wa kutatua tatizo hili.
 
Back
Top Bottom