Tanzania na siasa: Lugha ya kutumia Kiswahili au Kiingereza, Tatizo lipo wapi?

Inabidi mimi na wewe tuanze. Nilijaribu hiyo project na watanzania fulani lakini baada ya muda nilibaki peke yangu.

Mimi nimeshaanza na hoja hii japo hupendi dondoo za bloguni:

[h=3]KISWANGLISHI KIWE LUGHA RASMI YA TAIFA[/h]Sikuplani kuandika makala hii wiki hii. Sikupanga kufanya hivyo hasa ukizingatia kuwa juma hili kuna ishu nyingi zinazochukua taimu yetu sana. Suala la mafisadi papa ni mojawapo ya hayo masuala yanayochukua muda wetu mwingi.

Nilichenji, yaani nilibadili, mawazo yangu baada kusikiliza kipindi cha Redio Wani. Katika programu hiyo watalaamu walikuwa wakidibeti, yaani wakijadiliana, kuhusu matumizi ya lugha ya kufundishia. Hoja iliyonitachi, yaani iliyonigusa, sana ni ile inayosema kuwa matumizi ya lugha ya Inglishi, yaani Kiingereza, kufundishia yanasababisha wanafunzi wengi wasipate elimu.

Hakika ni jambo lisilopingika kuwa maticha, yaani walimu, wengi hawajui kufundisha kwa lugha hii kwa namna inayowafanya madenti, yaani wanafunzi, waelewe wanachofundishwa. Risechi, yaani tafiti, nyingi zimefanywa na watafiti wa ndani na nje ya nchi yetu kuonesha kuwa kutumia lugha isiyoeleweka vizuri kufundishia kunasababisha wanafunzi wasielewe vizuri somo.

Lakini pamoja na ukweli huo bado tunang'ang'ania kutumia Kiingereza kufundishia kuanzia Skuli, yaani Shule, za Sekondari hadi kwenye Vyuo Vikuu. Wengine tumeamua kabisa kuwa na shule za msingi zinazotumia Kiingereza kufundishia. Eti hatutaki watoto wetu wakose chansi, yaani fursa, ya kujua lugha ya globalaizisheni, yaani utandawazi, kana kwamba lugha yetu ya Kiswahili yenye maneno lukuki ya Kiarabu, Kiingereza na Kireno nayo sio lugha ya utandawazi!

Ni kweli kabisa kuwa sisi na watoto wetu tunapaswa kuijua lugha ya Kiingereza. Lakini njia ya kujifunza Kiingereza kizuri cha kuongea na kuandika sio kwa kukitumia kama lugha ya kufundishia katika jamii ambayo haikijui vyema. Ndio maana watoto wetu na hata viongozi wetu wanachanganya sana Kiingereza na Kiswahili wanapozungumza. Sasa hicho ni Kiingereza gani?

Wapo wanaokiita Kiswanglishi. Lakini, je, ni Kiswanglishi kweli? Hapana! Hicho ni Kiswahili kinachobadilika ghafla katikati ya sentensi au mazungumzo na kuwa Kiingereza au Kiingereza kinachobadilika ghafla na kuwa Kiswahili. Naam ni ‘Kiswahili English' au ‘English Kiswahili.' Wataalamu wa lugha wanauita mtindo huo ‘code switching' yaani kubadilibadili lugha katikati.

Kiswanglishi nachotaka kiwe lugha ya Taifa ni kipi basi? Ni hicho ambacho kimetumika katika sentensi za mwanzo za makala hii. Hiyo ni lugha ambayo Watanzania wengi, waliopo mijini na vijijini, wanakitumia. Kwa mfano, Bibi yangu amewahi kuniambia "ukifanya hivyo utadedi" akimaanisha ‘ukifanya hivyo utakufa.' Hicho ndio Kiswanglishi halisi maana ni Kiswahili kilichokopa neno ‘dead' kutoka kwenye ‘English' na kulifanya liwe neno ‘dedi' la Kiswahili.

Mifano ya jinsi tunavyotumia Kiswanglishi cha aina hii katika maandishi na mazungumzo yetu ya kila siku ni mingi. Hii ni baadhi tu: "nakwenda jobu kisha naenda shoping' tauni"; "najiandaa na pepa kisha naenda kupata menu"; "yule sista/braza atakupa data zote unazohitaji." Hiki ndicho Kiswanglishi kinachopaswa kuwa lugha ya Taifa maana ndicho Kiswahili chenyewe.

Hakika "Kiswahili sio Kreoli wala Pijini". Sentensi hii imeganda kichwani kwangu toka Mwalimu wangu wa Kiswahili alipoitamka na kuiandika ubaoni nilipokuwa Sekondari. Kwa ufupi, alikuwa ana maana kuwa pamoja na kwamba Kiswahili kimeazima maneno kutoka lugha nyingine - kama vile Gari na Duka kutoka kwenye Kihindi, Mvinyo na Meza kutoka kwenye Kireno, Malaika na Shetani kutoka kwenye Kiarabu, Skuli na Hela kutoka kwenye Kijerumani - bado ni lugha kamili inayofuata mnyambuliko wake wenyewe wa maneno wa Kibantu.

Hivyo Kiswanglishi cha kweli ni Kiswahili cha Utandawazi - kinachokopa na kukopesha sana maneno. Ni Kiswahili kinachokubali kuchukua ama kukopa maneno mapya ya Kiingereza na kuyafanya yawe ya Kiswahili cha Kibantu na yaweze kutumika katika sentensi ya Kiswahili cha Kibantu. Kwa mfano, Kiingereza kikitumia ‘dead' kinasema ‘s/he is dead', ‘s/he will die' na ‘s/he is dying' lakini Kiswahili kikilikopa neno hilo kitasema ‘amededi', ‘atadedi' na ‘anadedi.'

Kwa kukonkludi, yaani kuhitimisha, napenda kutoa wito kuwa tuidhinishe Kiswanglishi, kama kilivyotafsiriwa katika makala hii, kitumike kama lugha rasmi hasa shuleni na vyuoni. Tukifanya hivyo tutashangaa kuona lugha yetu inakua, elimu yetu inapanuka na jamii yetu inapata maendeleo maana lugha ya mawasiliano ni chachu ya kuongeza ujuzi, maarifa na uelewa mpana.

Naam Kiswahili na kiendelee kutandawaa kwa kasi katika zama hizi za utandawazi kama kilivyotamalaki enzi zile tulipofanya biashara zenye tija na Waaajemi, Waarabu na Wachina bila kutegemea lugha zao. BAKITA na TUKI mpo? Kubalini yaishe: 'Kiswahili = Kiswanglishi'!
 

Umeelewa kweli maana ya kichwa cha habari hapo juu? Kinasema vilivyo vipya virasimishwe!
 

Kiingereza na kilatini ni sawa na Kiswahili na Kiarabu.

Swali linabaki, hata kama tunatohoa kutoka Kiarabu, Kilatini, Kihaya n.k.

Quantum kwa Kiswahili ni nini?

Mie bado kidogo nianze kutunga maneno yangu kwa kukosa muongozo hapa.
 
Nukta (wild guess)

Nukta = point.
Nukta = full stop.

The quantum idea evades a point since it revolves around a probabilistic wave particle duality through Heisenberg's Uncertainty Principle, it is neither a wave, nor a particle crystallized in space-time as a point.
 
inaelekea watu wana misamiati ,jamani nani anajua maana aya maneno disguise, camouflage,sober,nasi tuelimike
 

Point taken lakini kwenye uelewaji wangu dhaifu wa lugha hayo maneno mekundu are not recognised na wataalamu wa lugha ya kiswahili kama ni maneno ya kiswahili. Kwa maana hiyo my argument still remains their on the assimilation process. Hayo maneno niliyo ya highlight kwa nyekundu ingawa they are widely used terms in every day language they are not yet recognised by swahili scholars as being official swahili words.

That defines those words as just being slang tofauti na neno ishu ingawa linahistoria ya kizungu lakini limekubalika ni kama neno la kiswahili na kamusi inatambua hivyo, kwa maana hiyo yaho maneno mengine hayawezi kutambulika kama visawe kwa sasa mpaka wataalamu wayakubali kama maneno ya kiswahili.
 

Kwa sababu mpaka leo hatuna maandiko yetu. Unaandika kwa kutumia alphabet ya warumi.

Kwa sababu hatuna umeme tuliovumbua, unatumia umeme kwa hisani ya Wamarekani.

Kwa sababu hatuna internet yetu, hapo unapojitutumua na kudai tuandike vitabu vyetu unasema hivyo kwa kutumia herufi za Warumi, umeme wa Wamarekani, Kompyuta sijui ya watu gani lakini si yetu, inernet mostly ya Wamarekani.

Bora hao Wajerumani wenye lugha yao na kumthamini Goethe. Sie leo mtoto anamaliza Chuo Kikuu hajui sio tu Kiingerea, bali hata Kiswahili.

Na usilogwe kumuuliza kama kashawahi kusikia kitu kinaitwa "Maisha Yangu Baada Ya Miaka Hamsini".

Huyo baba wa Taifa aliyejua umuhimu wa utaifa kabla ya kuwepo kwa taifa, na kulijenga taifa kutoka makabila, na kuchukia ukoloni, na kujua umuhimu wa Kiswahili katika yote haya, bado alitafsiri "Mabepari wa Venisi". Bado unasema kutafsiri vitabu vya lugha nyingine kwenda kwenye Kiswahili hakuhitajiki?

Umesoma historia ya China na kujua kisa kilichofanya China iliyokuwa imeendelea kisayansi kuliko Ulaya ipitwe na Ulaya kimaendeleo ni kitu gani?

Unajua tofauti ya usomi uliofunguka na ujivuni majununi?

Nikikusoma tena naona post yako inavyoanza na inavyoisha inajipinga yenyewe.

Incoherence.

Hujui unkwenda au unarudi. Napata shaka kuelewa kama kweli unamuunga mkono mleta mada au la. Kwa sababu sina hakika unajua uko wapi wewe mwenyewe.

Hata maswali yako uliyoanza nayo hayaeleweki kama ni rhetoric au la!
 
Nukta = point.
Nukta = full stop.

The quantum idea evades a point since it revolves around a probabilistic wave particle duality through Heisenberg's Uncertainty Principle, it is neither a wave, nor a particle crystallized in space-time as a point.
Sir, I am not going to come here and claim to be an expert in particle physics, you are telling us now about quantum ideas yet you asked for the translation of the word quantum in Swahili if it existed.

Which is which, my answer was based on the closest translation the word quantum could be translated into Swahili. Hayo ya ma-wave simo sio kwamba siyataki hila siyajui huo ndio ukweli wenyewe.
 

Naona umeelewa nilichotaka kulonga. Nilipata bahati ya kusoma isimu ya lugha. Katika isimu, sifa ya lugha ni lazima ijikamilishe katika mazingira yake. Ikiwa na maana kuwa vitu vyote vinavyojulikana ni lazima viwe na misamiati.

Walipokuja wageni na vitu vipya, kiswahili kama lugha zingine kikakopa misamiati na kuitamka kibantu. Katika miaka ya hivi karibuni utaratibu wa kukopa maneno na kuyatamka kibantu umeachwa na tunajaribu kugundua misamiati mipya kabisa.

Wakati mwingine tunavumbua neno jipya wakati tayari mitaani watu wanao msamiati wa neno hilo.
 
inaelekea watu wana misamiati ,jamani nani anajua maana aya maneno disguise, camouflage,sober,nasi tuelimike

hayo mawili wawindaji lazima wana maneno yao na hilo la mwisho lazima walevi wana maneno yake
 

yaani unasoma isimu halafu bado unataka lugha iwe na neno moja tu? kama waingereza wangetosheka na neno 'peradventure' basi wasingeongeza maneno haya: 'perhaps', 'possibly', na 'probably'!
 

Companero,

Ukiwa hujui tatizo lako utashindwa kulitatua. Tatizo la Tanzania ni waalimu. Masaa ya kiingereza ya primary school yangetosha kukuza lugha hiyo kama waalimu wangekuwepo. English ni lugha ya pili. Lakini tunasoma kama lugha ya kwanza.
 

I dont get the meaning of the word 'Isimu' to the extent lakini the whole point is understood. Ndio maana kwa waingereza sasa wanajua kuna maneno yataingia kwenye lugha yao, lakini linguist wako very keen on preserving their english language.

Na wao wana measure english kutokana na accepted standard za English (which is the accepted English in work places, education institution and expected to be used in mainstream media for the large part).

That is not to say estuary English does not permeate other parts of the northern country nor the cockney accent is not traveling, but it is just not the accepted standard of English nor will it ever give its imitators pass marks in the exams.

Kikubwa ni wanaijua lugha yao kutokana na historia yao mabadiliko yake and so forth and they know the plan is to preserve it from outside influence.

Huko kwetu i dont know companero na wenzake wana plan gani.
 
yaani unasoma isimu halafu bado unataka lugha iwe na neno moja tu? kama waingereza wangetosheka na neno 'peradventure' basi wasingeongeza maneno haya: 'perhaps', 'possibly', na 'probably'!

Nilisoma isimu kimakosa tu. Kutafuta unga.
 

Isimu ni sayansi ya lugha kama bado kumbukumbu zipo sahihi (linguistic). America English inasambaa haraka sana. Kwa hiyo hata kama waingereza watafanya juhudi za kuzuia, long time no see you itaendelea ku-influence the World.
 

Baada ya kusoma post yako naweza kusema kwamba nafikiri kama ungekuwepo (Mungu saidia haukuwepo) wakati Wamisionari (ambao walikuwa Wazungu) wanatafsiri biblia enzi hizo ungepiganiana kuwashawishi wasitafsiri Biblia Kiswahili kwa maana "Kiswahili kinakosa uwezo wa kuelezea fikra", lakini Wazungu walifanya pamoja na kuwa Biblia ni moja ya vitabu vigumu sana, lakini walifanya na leo hii Watanzania wengi tunanufaika kwa kazi kubwa iliyofanywa ya kuifanya liturjia kuwa kwa Kiswahili (Wazungu walifanya), sasa kama waliweza Biblia kwa nini ishindikane Fizikia au Kemia au Hisabati?

Hii inadhihirisha tu usemi kwamba sisi Waafrika hakuna kitu tunaweza kufanya, nakuhakikishia kama Tanzania ingekuwa bado inatawaliwa na Wazungu (Wajerumani) ambao ndio walileta mfumo wa kutumia Kiswahili mashuleni (sio sisi) leo hii tungekuwa tunatumia Kiswahili kuanzia chekechea mpaka Elimu ya juu, lakini kwa bahati mbaya Mungu hakutupenda sana wakaondoka mapema bila kuendelea kutuelimisha kwa Lugha yetu wenyewe leo hii zaidi ya miaka 100 baadaye tunapinga kwa nguvu zote Lugha (yetu wenyewe na hii utaiona Afrika tu) iliyotufundisha Neno La Mungu!

Na mwisho kuna nchi nyingi sana za Kiafrika zinatumia Kiingereza kabisa, Je hali yao ya kimaendeleo ikoje? kama hali yao ni bora sana kuliko yetu nikimaanisha kwamba hawaibiwi kwenye Mikataba kama sisi au hawauzi rasilimali zao kama sisi kwa kuwa wanatumia Kiingereza na hivyo kuelewa kilichoandikwa kwenye mikataba, basi hoja yako inaweza kuwa na maana kidogo lakini SI KWELI Nigeria bado wanaibiwa ingawaje wanatumia kiingereza Ghana bado wanaibiwa rasilimali ingawaje wanatumia iingereza, Uganda bado, Kenya bado n.k HIVYO TATIZO SIO KISWAHILI

Kama kiingereza ni maendeleo nchi kama Jamaika na nyinginezo wote 100% wanatumia Kiingereza lakini bado ndio wa mwisho kwa Umaskini katika bara la Marekani na wanapitwa na nchi ambazo watu wao hawajuia kiingeza kabisa kama Venezuela, Brazilii ambayo wanatumia Kireno, sasa sijui hoja yako iko wapi?

Labda tunahitaji wazungu waje tena na sijui safari hii watatumia mbinu gani kuja kutuelimisha na kutuambia kwamba tunaweza kutumia Kiswahili na tukaendelea lakini kwa bahati mbaya bahati haiji mara mbili tuliipata mara ya kwanza toka kwa Wamisionari.
 

Katika nchi zote zilizoendelea hakuna nchi isiyotumia lugha yake.
 
Isimu ni sayansi ya lugha kama bado kumbukumbu zipo sahihi (linguistic). America English inasambaa haraka sana. Kwa hiyo hata kama waingereza watafanya juhudi za kuzuia, long time no see you itaendelea ku-influence the World.

Ushasema the world lakini sio kwa waingereza wala many ueropean states. Unajua kwanini, wenzako wana limit the amount of media saturation from the US, mfano ufaransa najua redio aziruhusiwi kupiga more than forty percent of external language musics per day and there people whose jobs is just to monitor that. Hata waingereza najua wana limitations on the amount of media coverage from the US (including mass media).

Na ukija kwenye mitihani ambayo inatungwa kwao, they dont compromise on their standard English nor languages. Since these societies are widely of 40:30:30 societies it tells you who is controlling who and who is influencing who.

Usiku mwema, usingizi tena.
 

Najiulizaga Tanzania twajipambanua kwamba Kiswahili ni chetu! Jiulize kwa nn maprofesa wengi na wakubwa idara za lugha Ulaya na amerika sio WaTanzania? Ni WaKenya na WaGanda! Watangazaji Idhaa za Kiswahili America, Ujerumani na uingereza vivyo hivyo!

Juzi hapa huko bungeni kuna kuna maprofesa wametolewa kijasho wameandaa nondo zao kwa kiingereza, Mch. Msigwa akasema wamesaini Swahili protocol watumie kiswahili kitumike!

Mch. Msigwa sio padri wa Kikatoliki! Naamini ameoa na watoto! Tuwe wakweli watoto wake anawasomesha shule za kata ambako ni Kiswahili mwanzo mwisho au any public school?

Tumekuwa wanafikiki sana! Mtu km Msigwa a wenzie sio km hawajui ulichoandika MM Ila ni unafiki na dynastic agenda! if u r poor.......... the poverty vicious cycle should continue! Poors should depend on chances!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…