Tanzania na Uganda zapigwa marufuku na Ulaya kuendeleza Miradi ya Mafuta na Gesi

Japokuwa hiyo sababu haina mashiko lakini bora tusitishe tu utafiti.Maana kizazi cha kutumia rasilimali zetu inavyotakiwa hakijazaliwa.wenye akili ndogo wanapanga mipango ambayo inakuwa ni hasara kwa taifa zaidi kunufaisha wawekezaji wa nje.Ili tunufaike,mafuta yanatakiwa yachakatwe hapahapa nyumbani na tutumie sisi na ziada tupeleke ubeberuni,hivyohivyo na gesi yetu ya mtwara.Lakini kwa kuwa sisi wazalendo tukitaka tupewe nafasi tunanyimwa na badala yake wanapewa kwa kujuana basi nchi itaendelea kuporomoka na kuongezeka kwa tozo zinazobuniwa na wenye akili ndogo
 
hata wao walianzia huko huko, hata sisi tutafika walipo. watuache tuanze.
 
Mh Lissu ameeleza katiba inasema nini ili Raia awe mbunge. Kigezo ninlujua kutambua a e i o u. Hao ndo tunaowatarajia wachallenge wenzao wa E U na kututungia mikataba
Tena Bunge la mwendazake😅
 
Hawa wazungu washenzi na huwenda ndio waandaa mipango ya kumwondoa JPM

Africa ili ikomboke kiuchumi, tunawahitaji viongozi wenye mitizamo kama kina hayati JPM, watu ambao wako tayari kufa Kwa ajiri ya nchi zao na rasilimali zake, na endapo hatutawahitaji kabisa viongozi dizaini ya kima Magufuli, maendeleo tutayasikia tu
 
Aisee.
Kiwango cha juu cha kudharauliwa
 
Hio diplomasia ilisaidia nini toka kuanza kwa taifa hili. Watu mnahubiri diplomasia ili muendelee kuliibia taifa na kuhujumu watanzania wenzenu kwa amani. Mi naona kuheshimiana ni muhimu kuliko amani ya kijinga
 
Kama hii habari ni kweli basi wazungu bado wana mkakati wa muda mrefu wa kumdumaza mwafrika kwa malengo yao.

Kama ni uharibifu wa mazingira, mbona kuna mabomba(mengi) yanayotoka Urusi kwenda ulaya kwa umbali mrefu kuliko huu wa kwetu na hatuoni huo uharibifu wa mazingira!?
 
Mradi utayeyuka na utafiti mpya utaonesha hakuna mafuta yoyote hapo walikuwa wanatania tu, ndipo stori itageuka historia kama gesi ya Mtwara.
Kweli mkuu umenikumbusha gas ya MTR. Ubeberu si mchezo
Mpeni kibajaji achambue hoja hapo!
Unaweza kuchaguliwa kimichongo ukateseka sana kama ni mstaarabu lakini
 
Kwani sasa hauna vikwazo vya kuingia huko kama Mtanzania? Enzi zetu, tuliosafiri zamani tulikuwa tunaenda nchi takriban zote Ulaya bila visa, leo yanawezekana hayo kwa PP ya Tanzania? Jiulize kwanini?
 
Mwana FA au Babu Tale wataweza kuongea nini kwenye hili? Ila yule mwendazake alituweza kwakweli
Kiukweli jiwe ndio alaumiwe Sana, wagombea ubunge wenye IQ kubwa aliwafanyia figisu, na uchaguzi kwa ujumla aliuharibu mtokeo yake kupata baadhi wabunge ambao weupe kichwani
 
Bunge la ulaya ama limejaa vilaza vyeti feki wa ulaya au limejaa njaa. Yaani kila mwenye hela anaweza kupisha lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…