Kabudi Yu wap kwanHivi ndani ya bunge letu la michongo ni mbunge gani anaweza kujenga hoja juu ya hilo? Pengine kukaa kwao kimya kumeepusha aibu kubwa zaidi maana kama wangeongea hatuna hakika wangeropoka nini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabudi Yu wap kwanHivi ndani ya bunge letu la michongo ni mbunge gani anaweza kujenga hoja juu ya hilo? Pengine kukaa kwao kimya kumeepusha aibu kubwa zaidi maana kama wangeongea hatuna hakika wangeropoka nini
MmhKabudi Yu wap kwan
Yameona wivu, hayataki tuendelee, yanatake menyewe tu ndo yawe na maendeleo. Sis tubaki kujikomba kwa menyewe. Washindwe na walegee.
MmhKabudi Yu wap kwan
Kama unamaanisha ulicho andika(japo sijawahi kuwa sapota wa magufuli kwa mengi isipokuwa kwa mradi wa umeme) basi tanzania tunayo safari ndefu sana
Awamu ya 6 ya serikali ya CCM, mmesaini mikataba mingi ya kukubali kufungua milango ya demokrasia, uhuru, haki ya kukusanyika n.k bila kusahau katiba yetu inaruhusu shughulu za kisiasa. Sasa huku kubabaika kunatoka wapi
Mohamed mbona ana count? Au hajafa?Tuondokee hapa, dead men don't count.
Marahaba za porini au Kibaha? Mwenzio najiandaa kwenda msibani kwa mama hayo ya mafuta yatapita mradi kazi iendelee lakini siyo maneno na mipango isiyoisha.Shikamoo dada
Hivi si Makamba alikwenda kwenye mkutano wa mazingira hivi majuzi tu??Asilimia kubwa ya mradi umebebwa na Uganda kwa hiyo muamzi mkuu ni Uganda but sioni dalili ya chochote kusimama,hizo kampuni za mzungu zinaweza wekewa vikwazo ila tutaendelea na Wachina na pesa za Nchi za Tanzania,Uganda na Sasa DRC 👇
Very goodHio diplomasia ilisaidia nini toka kuanza kwa taifa hili. Watu mnahubiri diplomasia ili muendelee kuliibia taifa na kuhujumu watanzania wenzenu kwa amani. Mi naona kuheshimiana ni muhimu kuliko amani ya kijinga
KIMEUMANASalaam Wakuu,
Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia Azimio linalozitaka Tanzania na Uganda kusitisha mara moja uendelezaji wa Miradi ya mafuta na Gesi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Wanadai miradi hiyo inaharibu mazingira.
Wakati Bunge la Tanzania likiwa kimya, Bunge la Uganda limelaani azimio hilo walilodai ni kiwango cha juu cha Ukoloni Mamboleo na ubeberu dhidi ya Uhuru wa Uganda na Tanzania
View attachment 2358292
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima Nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani Mkoani Tanga Nchini Tanzania, ni Mradi wenye urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.
Bomba linapita katika mikoa 8 ya Tanzania Bara ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, vilevile linapita katika wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.
Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Lengo la Mradi
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.
Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili lilitarajiwa kujengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Japan na Korea Kusini waondoe hao ni vibaraka na washirika. Japan ni mshirika wa hayo mataifa na Korea Kusini ni kibaraka.Watakachofanya ni kuwapiga mkwara makampuni na mabenki yao na hivyo watajitoa kufadhili na kuendeleza huu mradi. Huu ndiyo wakati sasa Afrika inatakiwa kushirikiana na mataifa mengine yanayoibuka kuwa na nguvu kiuchumi na kiteknolojia kama China, Urusi, Japan, India, Korea kusini na kuachana na utegemezi kwa mabeberu wa magharibi.
Inawezekana eti. Si kuna wakati Bunge lilimpongeza Magufuli kwa habari fake hadi idara ya maelezo wakaitolea press release!kwa hiyo hata hao uganda wamekaa hapo kujadili porojo?