Issues sio katiba issues kiongozi kuwa na ujasiri kuanziasha harakati na kuwaface wazungu. Hii issues haitaji sana katiba bali nguvu kutoka kwa Rais na jopo la wasomi,sio wanasiasa wasiokuwa na misimamo.Mh Lissu ameeleza katiba inasema nini ili Raia awe mbunge. Kigezo ninlujua kutambua a e i o u. Hao ndo tunaowatarajia wachallenge wenzao wa E U na kututungia mikataba
Itakuwaje ni porojo wakati umeona clip inayoonyesha bunge la Uganda limejibu hoja hiyo?Tuwekee source ya habari hii, la sivyo ni porojo tu
Hakuna Vita ya Uchumi duniani.Sikieni enyi nchi na wakaao ndani yake. Vita ya uchumi ni ngumu na kuishinda kwake ni kushupaza shingo bila kubwabwaja. Yaani wanaona tu mnalaza pipes bila kuwatajataja wala kuwabeza na kuwaita majina yasiyo faa n.k.
India china ethiopia n.k miradi yao mikubwa waliziba masikio na wakafanya.
Kwenye swala la nishati sijawahi kuwa rafiki na yeyote anaye kwamisha huo ndio mskmamo wangu
Binge la Tanzania wao wako busy kujadili nguvu za kiumeSalaam Wakuu,
Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia Azimio linalozitaka Tanzania na Uganda kusitisha mara moja uendelezaji wa Miradi ya mafuta na Gesi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Wanadai miradi hiyo inaharibu mazingira.
Wakati Bunge la Tanzania likiwa kimya, Bunge la Uganda limelaani azimio hilo walilodai ni kiwango cha juu cha Ukoloni Mamboleo na ubeberu dhidi ya Uhuru wa Uganda na Tanzania.
View attachment 2358292
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima Nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani Mkoani Tanga Nchini Tanzania, ni Mradi wenye urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.
Bomba linapita katika mikoa 8 ya Tanzania Bara ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, vilevile linapita katika wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.
Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Lengo la Mradi
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.
Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili lilitarajiwa kujengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Watakachofanya ni kuwapiga mkwara makampuni na mabenki yao na hivyo watajitoa kufadhili na kuendeleza huu mradi. Huu ndiyo wakati sasa Afrika inatakiwa kushirikiana na mataifa mengine yanayoibuka kuwa na nguvu kiuchumi na kiteknolojia kama China, Urusi, Japan, India, Korea kusini na kuachana na utegemezi kwa mabeberu wa magharibi.
Lakini wanaopinga ni asasi za kijamii ambazo idadi yao 263, zikiwemo baadhi za Uganda, Tanzania na Kenya japo nyingi za Uzunguni, haitakua haki kulaumu hayo mabenki, wao walikua wameridhia kutoa mikopo. Kimsingi ni kushughulkia na kujibu madai yao kitaalam.
JidanganyeeeNinakubaliana na wazo hili.
Hakuna sababu muhimu ya kuendelea kuwapapatikia hawa watu.
Dunia inavyogeuka sasa, utegemezi kwao hautakuwa wa lazima sana, kama China, India, Urusi na mataifa mengine yataamua kuachana na mifumo inayotumiwa na hawa wahuni kuendelea kutawala dunia kiuchumi. Teknologia sasa imeenea, haihodhiwi tena na haya mataifa machache.
kwa utawala wa huyu bibi sijuiSikieni enyi nchi na wakaao ndani yake. Vita ya uchumi ni ngumu na kuishinda kwake ni kushupaza shingo bila kubwabwaja. Yaani wanaona tu mnalaza pipes bila kuwatajataja wala kuwabeza na kuwaita majina yasiyo faa n.k.
India china ethiopia n.k miradi yao mikubwa waliziba masikio na wakafanya.
Kwenye swala la nishati sijawahi kuwa rafiki na yeyote anaye kwamisha huo ndio mskmamo wangu
Mavi yake!! Angewajibu kwani yeye ndiye mwenye mafuta? Huyu Magufuli mnamu over estimate sana. Alikuwa pimbi tu na asingefanya lolote.Mabeberu bana daah hapa Chuma mwamba JPm angewajibu vizuri tu
Mavi yake!! Angewajibu kwani yeye ndiye mwenye mafuta? Huyu Magufuli mnamu over estimate sana. Alikuwa pimbi tu na asingefanya lolote.
Alishindwa kuuza korosho kupitia TPDF mpaka sasa kuna baadhi hawajalipwa ndiyo mnafananisha na mafuta??
Alishindwa kuuza korosho kupitia TPDF mpaka sasa kuna baadhi hawajalipwa ndiyo mnafananisha na mafuta??
"Kula uliwe" - Kikwete.
Dunia ya leo wewe kinyangarakata ukijifanya mroho na kutaka kula peke yako, shibe itakutokea puani. Tusisahau yaliowakuta GHddafi na Saddam Hussein. Kosa lao lilikwa ni kukata mirija tu.
Tanzania inatakiwa tusikurupuke, diplomasia ya hali ya juu itembee, na naamini tuna wana diplomasia waliobobea ndani ya Tanzania
Sikuwaza hili,ila nimekuelewa haraka sana kwa kasi ya ajabu.Hivi ndani ya bunge letu la michongo ni mbunge gani anaweza kujenga hoja juu ya hilo? Pengine kukaa kwao kimya kumeepusha aibu kubwa zaidi maana kama wangeongea hatuna hakika wangeropoka nini.