Tanzania na Uganda zapigwa marufuku na Ulaya kuendeleza Miradi ya Mafuta na Gesi

Tanzania na Uganda zapigwa marufuku na Ulaya kuendeleza Miradi ya Mafuta na Gesi

Afrika watakaopata maendeleo ni wachache. Wengi watabaki na umaskini.
Hakuna aliyebisha. Ila je, wakati wao wanjiletea maendeleo hawakujali kuhusu wanyama, ila imefika zamu yetu ndio wanyama wamekuwa muhimu all of a sudden, au sio
 
Salaam Wakuu,

Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia Azimio linalozitaka Tanzania na Uganda kusitisha mara moja uendelezaji wa Miradi ya mafuta na Gesi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Wanadai miradi hiyo inaharibu mazingira.

Wakati Bunge la Tanzania likiwa kimya, Bunge la Uganda limelaani azimio hilo walilodai ni kiwango cha juu cha Ukoloni Mamboleo na ubeberu dhidi ya Uhuru wa Uganda na Tanzania.

View attachment 2358292

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima Nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani Mkoani Tanga Nchini Tanzania, ni Mradi wenye urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.

Bomba linapita katika mikoa 8 ya Tanzania Bara ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, vilevile linapita katika wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.

Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Lengo la Mradi
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.

Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili lilitarajiwa kujengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).tuna subili tamko la bunge letu
 
Mzungu sio kwamba anasema ukweli kuhusu mazingira ila mbinu yake anataka iwe chini yake ili atuburuze kama ilivyo kawaida yao kueneza fitna hadi vita
Hali ilivyo duniani kote sasa hivi ni lazima hata wao wawe wameanza kutambua kwamba mbinu zao hazifanyi kazi tena.
Wameanza kuwa watu wa kupuuzwa tu kwenda mbele.

Vimisaada vyao wanavyovitumia kuburuza nchi nyingine mwishowe vitakuwa havina nguvu tena.
 
Hivi tuna timu nzuri ya kuweza kutoa hoja kama hizi mbele ya hao mabeberu?
Hapa nathani tutashindana ni kweli haya ni mawazo yetu ili tuweze kujikwamua kiuchumi sasa wao kama waona kunashida wazieleze. Na sisi tunawasomi tutaziona hizo athari. Kinyume cha hapo tukaze buti tufanyie.
 
Mradi na uendelee... mambo yetu watuachie wenyewe...
 
Waambieni hao kima weupe kwamba Mradi utajengwa Total awepo au asiwepo,Mwenye mali kasema mafuta yata flow come 2025 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220917-173957.png
    Screenshot_20220917-173957.png
    107 KB · Views: 1
Salaam Wakuu,

Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia Azimio linalozitaka Tanzania na Uganda kusitisha mara moja uendelezaji wa Miradi ya mafuta na Gesi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Wanadai miradi hiyo inaharibu mazingira.

Wakati Bunge la Tanzania likiwa kimya, Bunge la Uganda limelaani azimio hilo walilodai ni kiwango cha juu cha Ukoloni Mamboleo na ubeberu dhidi ya Uhuru wa Uganda na Tanzania.

View attachment 2358292

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima Nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani Mkoani Tanga Nchini Tanzania, ni Mradi wenye urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.

Bomba linapita katika mikoa 8 ya Tanzania Bara ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, vilevile linapita katika wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.

Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Lengo la Mradi
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.

Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili lilitarajiwa kujengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Angekuwapo Magu lingejengwa kibishi. Haya tusubiri tamko rasmi la serikali wanasemaje ingawa lazima wa lay down na kuufyata kwa kwenda na beat la beberu aka bunge la EU
 
Inabidi ifike mahali tuwe na misimamo yetu kama nchi
Sio kupelekeshwa na mataifa mengine kwenye ishu ya maendeleo,
Nishukuru wenzentu bunge lao na serikali (rais) wao wametoa msimamo wao
Huku kwetu bunge linatakiwa lionyeshe Njia kwa serikali sio tu kusubiri rais anasemaje

Naamini kila mradi unakuwa na bajeti ya kutunza mazingira,
Binadamu ndo mmiliki wa mazingira na sio mtumwa wa mazingira,anaweza kuamua uyaweke vipi kwa fAida zaidi
Unaweza utoe msitu eneo A upeleke eneo b
 
Kwa nini hawakusema hayo wakati wa JPM?
Tayari wameshaona tuliobaki ni mapoyoyo tu hata wakitutisha kidogo tu,tutasalimu amri.
RIP, JPM BABA YETU MPENDWA NA MZALENDO WA KWELI.
 
Ninakubaliana na wazo hili.

Hakuna sababu muhimu ya kuendelea kuwapapatikia hawa watu.

Dunia inavyogeuka sasa, utegemezi kwao hautakuwa wa lazima sana, kama China, India, Urusi na mataifa mengine yataamua kuachana na mifumo inayotumiwa na hawa wahuni kuendelea kutawala dunia kiuchumi. Teknologia sasa imeenea, haihodhiwi tena na haya mataifa machache.
Wamechanganyikiwa majuzi mipanho yao yote pamoja na dalali wao kwenda kuweka mambo sawa bado wakapigwa na kitu kizito...Mungu anatupenda sana, safari ndiyo hiyooo kuelekea canaan...Hureee!

Ukiona wanagugumia maumivu yamewapata sehemu nyeti...
 
"Kula uliwe" - Kikwete.

Dunia ya leo wewe kinyangarakata ukijifanya mroho na kutaka kula peke yako, shibe itakutokea puani. Tusisahau yaliowakuta GHddafi na Saddam Hussein. Kosa lao lilikwa ni kukata mirija tu.

Tanzania inatakiwa tusikurupuke, diplomasia ya hali ya juu itembee, na naamini tuna wana diplomasia waliobobea ndani ya Tanzania.
Mbona unatutia uwoga?
Wenzio hatuogopi wala hatupo tayari kuogopa tulishatoka huko zamaniiii...RIEP JPM, wazalendo bado tutaendeleza mpambano mpaka iwe njema!
 
Isifike mahali tukaona tunaweza kukabiliana na mabeberu bado tupo nyuma Sana kupata maendeleo ya nchi inategemea zaidi juhudi za mwananchi mmoja mmoja
Usitutishe...We are determined, na haturudi nyuma, mtarudi wenyewe...Sisi hao, ndiyo mtajua hamjui!
 
This is another version of international devolution in natural resources planning, management and utilization. The top-down approach is clinging into power just like Museveni does. We are waiting for the Tanzanian government to kizengalize(copy) from Uganda's statements.
M7 anajua anachokifanya japo anapunguziwa nguvu ila mungu mkubwa amepata mkono wa ziada...
 
Hakuna Vita ya Uchumi duniani.
Tatizo letu Afrika ni kukosa msimamo unaoungwa mkono na Wananchi wetu.
Ni nani huku kwetu anayejua miradi inayofanyika huko Ulaya na athari zake kimazingira?
Jibu ni kwamba, hakuna.
Kama hatujui kinachofanyika kwao, kwa nini tunawasikiliza wanapozungumzia yanayofanyika kwetu?
Jibu ni moja tu. Hatujiamini.
Ni nini chanzo cha kutojiamini kwetu?
Ukishaanza kusikia ooh diplomacy ujue ni ukosefu wa kujiamini na pia maslahi binafsi, period!

Ila safari hii jiwe lililokataliwa na waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni...Ahsante m7 Mungu akupiganie usikengeuke, angalia picha kubwa na siyo hiyo ndogo, aliyeletwa na Mungu japo hana stake atakusaidia, sisi tuliyoachia mbio kabla ya kutwaa taji bado Mungu anatukumbuka...The spirit is more powerful than the physical...Our angel in heaven please pray for us!
 
Back
Top Bottom