Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hahahahaaaaaaaaa watani walikufanyiaga nini mkuu? Angalia tu usinivunje mbavu zangu. Ninasubiri kwa hamu kufahamuWatani watu wabaya sana
Doooh, hatari sana baba la babaDah! Aisee mimi watani na waogopa sana, wana kuhaibisha hata mbele za watu, nimitaniaga mtani wangu watu wakacheka ilivyofiza zamu yangu mbele za watu alinitania huo utani, hadi leo siwatanii tena
Una maana gani mkuu?Kati ya watani zetu wote wanyonge kwetu, yaani hawapindui sijui tulijichagulia!!
Watani wenu ni akina naniKati ya watani zetu wote wanyonge kwetu, yaani hawapindui sijui tulijichagulia!!
Una maana gani mkuu?
Watani wenu ni akina nani
Wazaramo wanavyoongeaga mkuu nyie mtakuwa ni balaaWatani zetu ni Wagogo, Wazaramo, Wangoni.... hovyo kabisa hawa watu.
Zaramo people of the eastern coast of Tanzania are talkative like no other. I used to have a friend of mine who belonged to that kind of tribe.Wazaramo wanavyoongeaga mkuu nyie mtakuwa ni balaa
Nawajua wazaramo, wagogo, wamachinga na wengineo.Kwa mimi msukuma ni makabila yapi hapa tanzania na nje ya nchi ya tanzania ni watani zangu?
Nimeuliza tu wakuu
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.
Eti ndugu zangu wa Tanzania;
Ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti (Mfano: Msukuma Vs Mzaramo) kisha ukaumia nafsi yako kimoyomoyo?
Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, mimi Infantry Soldier kabila langu halisi ni MJALUO, mwenyeji wa mkoa wa MARA katika wilaya ya RORYA. Kuna weekenda moja siku ya jumamosi jioni nilienda Pub moja hivi ipo karibia na huku ninapokaa.
Nilienda kupata beer mbili tatu moja ya moto na nyingine ya baridi kabisa kwa ajili ya kupunguza stress kidogo za hapa na pale za kimaisha. Kwa kawaida nikiendaga kunywa beer huwa ninabebaga 20,000/= kwa maana huwa ninakunywa beer mara moja tu kwa week (Jumamosi Jioni Pekee).
Sasa week hiyo nilikuwa nimechacha vibaya sana. Nina 10,000/= tu kwenye wallet ambayo ingeniwezesha kupata beers labda nne tu zile Lite kisha narudi home. Sasa bwana wakati nimepiga beer yangu ya kwanza ninajiandaa kupiga chupa ya pili akatokea mzee mmoja wa KIHAYA.
Sisi WAJALUO watani zetu huwa ni hawa WAHAYA, WAKEREWE pamoja na WAHA. Huyu mzee wa Kihaya alikuwa amezoeana sana na mzee wangu na anapajua home kwa maana nilipopanga mimi na nyumbani kabisa ni mwendo kama wa 30 minutes tu kwa miguu.
Sasa huyu mzee aliponiona tu akaanza mambo yake kama kawaida, "aaaah mtani nakuona mwanangu. alafu wee mtani huo ukitoka katika shughuli zako huko mkoani huwa haunipigi hata offer kidogo mzee wako nipooze koo langu" mara paaap yule baba akachukua beer yangu akafungua kwa meno kisha akaanza kuinywa.
Daaaah aisee roho iliniuma ile mbaya. Nikiangalia mfukoni nina buku teni tuu la kulipia bill, alafu huyu mzee ndio kanywa beer yangu kisha akavuta kiti akakaa karibu yangu zikaanza story. Roho iliniuma sana. Kumpiga siwezi kwa maana mimi sina hulka za kupigana na huyu ni baba mtu mzima wa miaka kama 50 hivi. Nikasema sawa bwana yote kheri.
Je, wewe mwana JF ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti (mtani wako) kisha ukaumia nafsi yako kimoyomoyo?
ANGALIZO: Ukiachana na utani wa kupitiliza utani una faida kubwa. Wengi tumefanikisha mengi kupitia watani zetu. Ukienda eneo la ugenini na ikatokea ukamkuta mtani wako huko hakika hautakuwa mpweke.
Watani ufanikisha sherehe na hata misiba kwa sababu uhamasishana wenyewe kwa wenyewe na kuhamasisha wengine na kufariji wafiwa.
Yanakera matani ya kikabila ila nasisitiza yaendelezwe maana Yanaleta mshkamano na kuambizana ukweli bila kuoneana haya.
Jamii inapumua kupitia haya matani na kuishi kwa mshikamano. Waliosoma social engineering courses tunaelewa dhima ya hili suala.
OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
hahahahahaaaaaJamani utani mzuri ila uwe unauweza kuna MKURYA alikuwa anapenda kunitania sana mara wahaya hivi mara vile mara mhaya Toleo la Mwisho wahaya wenzio Maprofessa na mkalia kimya. Cku akaja ooh me mwenzio Sajent wa jeshi alafu mtu mzima kweli nikamwangalia nikatema nikamuuliza sasa na iyo kazi kazi gani hata ukimfundisha MBWA anaweza Ebu nitolee huko kazi kazi kazi ya mbwa tu hiyo unachomzidi ni mshahara 🤣🤣🤣
Nilikula mtama wa Mbasha mdgo nikazimia toka siku hiyo anitanii
[emoji23][emoji23][emoji23]Jamani utani mzuri ila uwe unauweza kuna MKURYA alikuwa anapenda kunitania sana mara wahaya hivi mara vile mara mhaya Toleo la Mwisho wahaya wenzio Maprofessa na mkalia kimya. Cku akaja ooh me mwenzio Sajent wa jeshi alafu mtu mzima kweli nikamwangalia nikatema nikamuuliza sasa na iyo kazi kazi gani hata ukimfundisha MBWA anaweza Ebu nitolee huko kazi kazi kazi ya mbwa tu hiyo unachomzidi ni mshahara [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nilikula mtama wa Mbasha mdgo nikazimia toka siku hiyo anitanii
Hakika umenena vema mkuu...Jamani utani mzuri ila uwe unauweza
🤣🤣🤣 mtani ninakuona unaanza kuliamsha dude hahahaaaaaa au sio???Sasa mtani wangu kama bia uliumia ivo angekuja kula au kumtongoza mkeo ingekuwa [emoji23][emoji23]Kwanza MJARUO gani bado huko unatanga tanga wajaruo wenzio wote wako Marekani (USA) we uchoyo tu unakuta hata kisumu upajui 🤣🤣🤣kwenda huko