Tanzania na Utani wa Makabila: Ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti ukaumia nafsi yako?

Tanzania na Utani wa Makabila: Ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti ukaumia nafsi yako?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Eti ndugu zangu wa Tanzania;

Ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti (Mfano: Msukuma Vs Mzaramo) kisha ukaumia nafsi yako kimoyomoyo?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, mimi Infantry Soldier kabila langu halisi ni MJALUO, mwenyeji wa mkoa wa MARA katika wilaya ya RORYA. Kuna weekenda moja siku ya jumamosi jioni nilienda Pub moja hivi ipo karibia na huku ninapokaa.

Nilienda kupata beer mbili tatu moja ya moto na nyingine ya baridi kabisa kwa ajili ya kupunguza stress kidogo za hapa na pale za kimaisha. Kwa kawaida nikiendaga kunywa beer huwa ninabebaga 20,000/= kwa maana huwa ninakunywa beer mara moja tu kwa week (Jumamosi Jioni Pekee).

Sasa week hiyo nilikuwa nimechacha vibaya sana. Nina 10,000/= tu kwenye wallet ambayo ingeniwezesha kupata beers labda nne tu zile Lite kisha narudi home. Sasa bwana wakati nimepiga beer yangu ya kwanza ninajiandaa kupiga chupa ya pili akatokea mzee mmoja wa KIHAYA.

Sisi WAJALUO watani zetu huwa ni hawa WAHAYA, WAKEREWE pamoja na WAHA. Huyu mzee wa Kihaya alikuwa amezoeana sana na mzee wangu na anapajua home kwa maana nilipopanga mimi na nyumbani kabisa ni mwendo kama wa 30 minutes tu kwa miguu.

Sasa huyu mzee aliponiona tu akaanza mambo yake kama kawaida, "aaaah mtani nakuona mwanangu. alafu wee mtani huo ukitoka katika shughuli zako huko mkoani huwa haunipigi hata offer kidogo mzee wako nipooze koo langu" mara paaap yule baba akachukua beer yangu akafungua kwa meno kisha akaanza kuinywa.

Daaaah aisee roho iliniuma ile mbaya. Nikiangalia mfukoni nina buku teni tuu la kulipia bill, alafu huyu mzee ndio kanywa beer yangu kisha akavuta kiti akakaa karibu yangu zikaanza story. Roho iliniuma sana. Kumpiga siwezi kwa maana mimi sina hulka za kupigana na huyu ni baba mtu mzima wa miaka kama 50 hivi. Nikasema sawa bwana yote kheri.

Je, wewe mwana JF ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti (mtani wako) kisha ukaumia nafsi yako kimoyomoyo?

ANGALIZO: Ukiachana na utani wa kupitiliza utani una faida kubwa. Wengi tumefanikisha mengi kupitia watani zetu. Ukienda eneo la ugenini na ikatokea ukamkuta mtani wako huko hakika hautakuwa mpweke.

Watani ufanikisha sherehe na hata misiba kwa sababu uhamasishana wenyewe kwa wenyewe na kuhamasisha wengine na kufariji wafiwa.

Yanakera matani ya kikabila ila nasisitiza yaendelezwe maana Yanaleta mshkamano na kuambizana ukweli bila kuoneana haya.

Jamii inapumua kupitia haya matani na kuishi kwa mshikamano. Waliosoma social engineering courses tunaelewa dhima ya hili suala.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Napenda sana utani wa kikabila....kama ulivyomalizia kuwa ukiwa ugenini ukapata mtani wako haswaa anayejua kutania,hautakuwa mpweke.

Kuna utani wa kabila na kabila,kuna utani wa babu na wajukuu,mjomba na wapwa, na utani wa koo na koo....na kwa kabila letu msiba au harusi hainogi bila kuwepo watani,ndio wachimba kaburi, wapika chakula na kupokea wageni na ndio wasema ukweli..japo katika hali ya utani
 
Ukiachana na utani wa kupitiliza utani una faida kubwa. Wengi tumefanikisha mengi kupitia watani zetu. Ukienda eneo la ugenini na ikatokea ukamkuta mtani wako huko hakika hautakuwa mpweke. Watani ufanikisha sherehe na hata misiba kwa sababu uhamasishana wenyewe kwa wenyewe na kuhamasisha wengine na kufariji wafiwa. Sitasahau jioni ya siku moja niliyoshuhudia baba yangu mzazi akipigana mieleka na mtani wake barabarani hadi wakaangushana chini mavumbini huku wote wakicheka kwa furaha. Kilichopelekea kupigana mieleka ile ni kule baba na mtani wake kutambiana kila mmoja kwamba ni mbabe na hawezi kuangushwa na mwenzie. Siku mzazi wangu alipofariki yule mtani alilia kama mtoto. Anaebeza utani yawezekana bado hajakua na kama kakua hajakulia katika haya mazingira yetu ya kiafrika. Na kama kakulia katika mazingira yetu ya kiafrika basi kakua mwili tu lakini si kiakili.
Imenigusa sana
 
Siku ya msiba wa mjomba wangu, wakaja watani yaani ndo tumetoka kuzika mtu ananivuta mtandio huku anacheka

Nilijikita nimemng'ata ule mkono hadi akatoka ngozi.

Utani wa msiba watu waache kwa kweli.
 
Mimi mndali was songwe Sasa wanyia wa huku wanasemaga wewe changamka unafanya Kama mndali au wacha ushamba Kama mndali bwana na chukiaga sana

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom