Tanzania namba 3 kuingiza nguo za mitumba Afrika, yatumia Sh379.9 bilioni

Tanzania namba 3 kuingiza nguo za mitumba Afrika, yatumia Sh379.9 bilioni

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Tanzania imetajwa kushika nafasi ya tatu ndani ya Bara la Afrika kwa kuingiza nguo za mitumba katika mwaka 2022, ripoti ya tovuti inayojihusisha na masuala ya biashara Observatory of Economic Complexity (OEC) inaeleza.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Tanzania ilitumia Sh379.921 bilioni kuingiza nguo hizo nchini huku ikitanguliwa na Ghana iliyotumia Sh418.92 bilioni na kushika nafasi ya pili, huku Kenya ikiwa kinara kwa kukamata namba moja na kutumia Sh514.6 bilioni kwenye kuagiza mitumba.

Tanzania inashika namba tatu katika orodha hii wakati ambao imeendelea kushuhudia ongezeko la mauzo ya pamba inayozalishwa katika masoko ya nje kwa miaka minne mfululizo kati ya 2020/2021.

Katika uchambuzi zaidi kupitia ripoti ya OEC nchi nyingine ili kukamilisha orodha ya nchi 10 vinara katika uingizaji wa nguo za mitumba ni Angola ambayo ilishikilia nafasi ya nne na kutumia Sh303.93 bilioni kuagiza bidhaa hizo.

Wengine ni Nigeria iliyotumia Sh240.61 bilioni, Cameroon (Sh238.08 bilioni), Msumbiji (Sh212.75 bilioni), Benin (Sh205.15 bilioni), Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ilitumia Sh164.63 bilioni na Tunisia ambayo ikikamilisha orodha ya nchi 10 ilitumia Sh154.5 bilioni.

Mauzo ya pamba yapaa

Wakati ambao fedha nyingi zikitumika kuingiza nguo zilizotumika katika nchi mbalimbali, mauzo ya pamba katika masoko ya nje yameendelea kuongezeka.

Ripoti ya mwaka ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaonyesha kuwa mauzo ya pamba yaliongezeka kwa asilimia 52.3 kati ya mwaka 2020/2021 hadi mwaka 2023/2024.

Katika mwaka 2020/2021 mauzo ya pamba yalikuwa Sh349.5 bilioni, mwaka 2021/2022 yalikuwa Sh416.14 bilioni, mwaka 2022/2023 mauzo ya pamba yakifikia Sh510.86 bilioni na kufikisha Sh532.6 bilioni mwaka 2023/2024.

Hii ina maana gani

Akizungumzia suala hili, mchambuzi wa uchumi na biashara, Dk Balozi Morwa amesema kuzalisha pamba na kuuza nje ya nchi huku wewe ukiingiza mitumba si jambo linalopaswa kushangiliwa.

Badala yake anashauri, nguvu iongezwe zaidi katika kuvutia wawekezaji wanaotumia pamba kuzalisha nguo zinazoweza kuvaliwa na watu wa vipato tofauti, ili kuongeza wigo wa ukuaji wa uchumi na kuimarisha sarafu ya ndani.

“Kuzalisha nguo nchini na kuuza nje kutatufanya sisi kupata hela zaidi kuliko ambavyo tunauza pamba ambayo haijaongezewa thamani, tuvute wageni tuwape nafuu za kodi kwa masharti ya kutumia malighafi zinazozalishwa nchini,” amesema Dk Morwa.

Amesema hili linaweza kufanyika kwa kupitia upya misamaha ya kodi inayotolewa kwa wawekezaji kwa kuweka makundi, na si kila anayekuja wakati mwingine nchi inanufaika kidogo.

Msamaha wa kodi utolewe kwa masharti kwamba mwekezaji atumie malighafi za ndani kuzalisha bidhaa ambayo inafaa kwa soko lililopo na lile la nje. Mwekezaji wa kuzalisha pamba tu na kuuza nje huyo asiruhusiwe,” amesema Dk Morwa.

Amesema kufanya hivi, ukuaji wa uchumi utashuhudiwa kwa mtu mmojammoja akimaanisha wakulima na wale watakaoajiriwa katika viwanda vya uzalishaji wa bidhaa, huku nchi ikinufaika kwa kupata kodi kwenye mnyororo wa bidhaa.

Source: Mwananchi News

1738542406480.png

My Take

Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa nchi yetu kuwa ya tatu barani kwa kuingiza mitumba.

Hii inatoa fursa kwa vijana wetu machinga kupinga pesa ndefu mbali na wadanganyika kujikwatua na kujipamba hata kama wanalima pamba.

Hili ni jambo la kumshukuru Mungu na mheshimiwa rais kwa kuliwezesha na kuleta mapinduzi kama haya ambapo watu wetu watavaa nguo za bei nafuu huku wakiuza pamba kwa bei mbaya ughaibuni.
 
Attachments

  • 1738542540102.png
    1738542540102.png
    376.5 KB · Views: 4
View attachment 3223040

Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa nchi yetu kuwa ya tatu barani kwa kuingiza mitumba.

Hii inatoa fursa kwa vijana wetu machinga kupinga pesa ndefu mbali na wadanganyika kujikwatua na kujipamba hata kama wanalima pamba.

Hili ni jambo la kumshukuru Mungu na mheshimiwa rais kwa kuliwezesha na kuleta mapinduzi kama haya ambapo watu wetu watavaa nguo za bei nafuu huku wakiuza pamba kwa bei mbaya ughaibuni.. KWA HABARI ZAIDI BONYEZA HAPA TAFADHALI.
View attachment 3223041
Sio Jambo la kujivunia hata kidogo. Kuvaa mitumba wakati nyie ndio wakulima wa pamba, ni kielelezo halisi kinachoonyesha Viongozi wa nchi yenu Hawana akili, wameshindwa kuendeleza viwanda.

Nyerere ALITUACHIA viwanda kedekede vya kutengeneza nguo, viwanda vilikuwa ni Chanzo cha ajira na kukuza uchumi wa Mtanzania.

Unapouza malighafi nje, unauza kwa bei ndogo kuliko unavyonunua kutoka nje. Pia kununua nje sana kunapelekea unfavorable balance of trade.

NI UPUMBAVU wa hali ya juu kushabikia mitumba.

CCM omelamaza sana akili zetu. Imetuondolea kabisa ubunifu, hatuwazi lolote zaidi ya kufikiria mitumba tu. Nguo za mitumba, simu mtumba, computer mitumba, magari hata akili tunategemea wenzetu wawaze na kufikiria ndipo sisi tuje tu adopt maarifa yao.
 
Kuvaa mitumba au kutumia mali zilizokwisha kutumiwa na wazungu huko ni kukubali ya kuwa a second class person
 
Machalii wa kaskazini hawavai nguo mpya ni mwendo wa mitumba tu .Mingine wanachukuliw Kenya .
 
Hapa ndipo CCM ilipotufikisha!! Kuna siku tutatangazwa kama nchi mshindi namba moja kujengewa vyoo Duniani.

Yaanzishwe mashindano ya ujinga, uone kama kuna atakayeikaribia CCM.
 
Mitumba tunavaa na inatupendeza kweli! Ila siyo jambo la kufurahia hata kidogo. Maana tunavaa nguo ambazo wengine wamezichoka! Ukija kwenye magari, hali ni hiyo hiyo! Yaani miaka nenda sisi ni watu wa kutumia vitu used tu!!

Inasikitisha sana. Viongozi wetu hawana maono! Wengi wao wamewekeza zaidi kwenye siasa ili wao na vyama vyao, na familia zao, na marafiki zao; watawale milele! Na siyo kuzijenga nchi zao kiuchumi, kiteknolojia, nk.
 
Sio Jambo la kujivunia hata kidogo. Kuvaa mitumba wakati nyie ndio wakulima wa pamba, ni kielelezo halisi kinachoonyesha Viongozi wa nchi yenu Hawana akili, wameshindwa kuendeleza viwanda.

Nyerere ALITUACHIA viwanda kedekede vya kutengeneza nguo, viwanda vilikuwa ni Chanzo cha ajira na kukuza uchumi wa Mtanzania.

Unapouza malighafi nje, unauza kwa bei ndogo kuliko unavyonunua kutoka nje. Pia kununua nje sana kunapelekea unfavorable balance of trade.

NI UPUMBAVU wa hali ya juu kushabikia mitumba.

CCM omelamaza sana akili zetu. Imetuondolea kabisa ubunifu, hatuwazi lolote zaidi ya kufikiria mitumba tu. Nguo za mitumba, simu mtumba, computer mitumba, magari hata akili tunategemea wenzetu wawaze na kufikiria ndipo sisi tuje tu adopt maarifa yao.
Nyerere alitaifisha viwanda vya watu kibabe na kuwapa watu wasio na weledi kuvisimamia vikafa. Angeacha kina Chande waendeshe viwanda vyao huenda sasa hivi tungekuwa na viwanda vingi huku serikali ikichukua kodi ya kutosha.
 
The Observary of economic complexity

Top 10 Biggest Importers Of The Second-Hand Clothes In Africca
1)- Kenya🇰🇪 $202 million
2)- Ghana🇬🇭 $164 million
3)- Tanzania🇹🇿 $148 million
4)- Angola🇦🇴 $127 million
5)- Nigeria🇳🇬 $94.7 million
6)- Cameroon🇨🇲 $94 million
7)- Mozambique🇲🇿 $84.3 million
8)- Benin🇧🇯 $80.5 million
9)- Madagascar🇲🇬 $56.8 million
10)- Togo🇹 ...
 
Nyerere alitaifisha viwanda vya watu kibabe na kuwapa watu wasio na weledi kuvisimamia vikafa. Angeacha kina Chande waendeshe viwanda vyao huenda sasa hivi tungekuwa na viwanda vingi huku serikali ikichukua kodi ya kutosha.
Sera mbovu za uchumi za utawala dhalimu unaojua kudhulumu tu wa TANU/CCM
 
Back
Top Bottom