Kituko kumbuka Afcon iliyochezwa Gabon hawa wabotswana walifuzu kucheza fainali hizo,na Afcon prequalifiers hizi majuzi wamemwondoa Burundi,si timu ya kubeza.
Kaka
Jamal Malinzi, ni kweli tumefungwa na Zebras
(Kitswana: Dipitse) timu ya taifa ya Botswana, lakini nikizani kabla ya kukubali ubora wa Botswana ungejaribu angalau kuangalia wametoka wapi na wewe kama kiongozi wa soka na wenzio mjipime, na ndio kisa cha mimi kushangaa na kuibeza Tanzania.
Ni kitu cha ajabu sana hapa, Botswana ina watu 2.5Million na ukitoa watoto, Wazee na akina mama ambao ndio majority utapata vijana chini ya laki tano (<500000) wenye uwezo wa kucheza soka , na katika hiyo namba yao ndogo wameweza kupata watu 11 wakucheza soka na kwenda Afcon
kwa upande wako una watu 45million na wenye uwezo wa kucheza soka si chini ya 5million, Hivi kweli katika hiyo 5mil mumeshindwa kupata vijana 11 tu wa kutuwakilisha kwa ufanisi?
nimeweka hizo rough statistic kukuonyesha mapungufu makubwa mliyonayo viongozi wetu wa soka, naizungumzia kiundani Botswana kwa sababu naifahamu vizuri na najua wametoka wapi kisoka, Tulikuwa kule na kina Oscer Dan Korosso, Said Mshamu, Maalimu Salehe, Peter Manyika, Bakari Iddi na wengine wengi tu
Kihistoria Botswana kulikuwa hakuna soka ya kiushindani kwa miaka mingi tu, Miaka 10-15 iliyopita Botswana walikuwa poor sana, kwenye miaka ya 2000 Bakari Iddi alikuwa ameshachoka kisoka hapa Tanzania, lakini Botswana alikuwa ni Mfalme wa soka, aliikuta timu ya Mochudi Chiefs iko kwenye kushuka Daraja na ndani ya mechi tano alizocheza Bakari Iddi aliinyanyua timu, alikuwa anafunga goli zaidi ya tano kila mechi na zingine alikuwa anachukua mpira kwa kipa mpaka anafunga mwenyewe, alikuwa anafanya vitu ambavyo hata kwenye mechi za mchangani hapa Tanzania huwezi fanya, nimeiweka hiyo ili nikuonyeshe soka yao ilikuwa ya aina gani
Naongea hayo yote ili nikufahamishe hao jamaa chini ya kina Ashford Mamelodi (Fifa/Cosafa) wako serious na wanachokifanya, ndani ya uchache wao wameweza kupick cream lakini sisi pamoja na wingi ni ziro kabisa,
Kaka
Jamal Malinzi, tuna mfumo mbaya kabisa wa Soka, utafutaji wa wachezaji wa Taifa ni wa hovyo sana, jaribu kukusanya ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali hata ambao hawana majina ya soka hapo Tanzania, ukikaa ofisini na kusubiri report ya kina Kayuni(sijuhi kama bado yupo) hatutafika kokote,