Timu yetu ya taifa leo imefundishwa mpira na Algeria kuwa kuipgwa 7-0! Hii ni rekodi.Sijawahi ktk akili zangu timamu kuwahi kusikia Tz ikipata kisago cha aina hii. Sote tunawajibika lakni wewe ni zaidi.
Kwa mtazamo wangu wewe mwalimu wetu, pamoja na ubora wa Algeria, umeonesha udhaifu mkubwa sana ktk michezo yote miwili. Kama ungekuwa makini zaidi tungeweza kupunguza aibu hii ya milenia kwa mchi yetu.
Udhaifu wako mkubwa unatokana na kuendana na matakwa ya mashabiki hasa wanaoendekeza unazi wa Simba na Yanga. Ukiendelea kufanya hivi utaipoteza timu haraka na utajikuta unakalia kiti cha moto.
Udhaifu wako pamoja na benchi lako la ufundi unatokana na kile ulichodai kuwa sub ulizofanya taifa ndio ziliigharimu timu kitu ambacho si kweli. Ulifanya hivi kuwarishisha watu fulani ili kuficha udhaifu wa kweli wa timu ambao ni kupoteza umakini kwa defence yetu(loss of concentration). Unajua kuwa magoli yalirudishwa sio kutokana na timu yetu kuzidiwa na mashambulizi, la hasha! Ilitokana na ukosefu wa umakini wa walinzi wetu hususani Ngwali na Cannavaro. Unajua goli la kwanza lilifungwa wakati walinzi wetu wakimiliki mpira na kupigiana pasi za hapa na pale na walipopokonywa goli likafungwa. Unajua pia kuwa morali ya timu ilishuka sana baada ya goli hilo kiasi cha kurudia makosa yale yale yaliyopelekea goli la pili. Wewe ni shahidi kuwa Algeria walikuwa wameshapoteana kabisa baada ya kufungwa magoli 2, na kwamba magoli yao ilikuwa ni sawa na kuokota embe jangwani. Narudia tena, pamoja na sub zetu Ndemla na Ngassa kushindwa kufanya jipya ktk timu, lakini Mkwasa na benchi lako mnajua magoli waliyopata Algeria hayakutokana na pressure yao kuwa kubwa kwenye lango letu, laa bali udhaifu wa ulinzi na utumiaji wao bora wa nafasi.
Hapa ulijiweka ktk mtego wa kujiaminisha kuwa timu ile ya kwanza iliyoanza Taifa ndio ilikuwa bora zaidi na kwa maana nyongine ulitaka icheze hiyohiyo tu, nadhani tena bila sub!!!!! Inaweza kuwa kweli lkn hukupaswa kukariri. Hukupaswa kuwaza kishabiki, wewe ulitakiwa kuzingatia weledi wako kuelewa tatizo ilikuwa nini kiufundi. Ulipaswa kuangalia mazingira ya mechi.
Na ni kosa hili tena ndio limepelekea timu kupigwa kipigo cha milenia leo huko mjini Blida, Algeria. Tatizo sio kuwa kikosi chetu ni wabaya, hapana, tatizo ni kukariri na mazoea bila kujali mazingira ya mechi.Ulishindwaje kujua kuwa ni makosa kuanza na fowadi watatu hadi wanne ugenini kupishana na timu kama Algeria? Hebu fikiria wao walipokuja taifa pamoja na ubora wao lkn waliweka washambuliaji wawili tu na wakati mwingine akawa anabaki 1. Lkn wewe kwa sifa za Dar ukaona uweke 3!!!
Kutokana na ubora wa Algeria lkn ulipaswa kubadilisha mbinu kidogo tu ili kuwachanganya ambapo ktk nafasi ya Maguli, ungemwanzisha Malimi Busungu, kucheza kama winga mwongo wa kulia lkn mwenye majukumu makubwa ya ukabaji na kumsaidia Kapombe na hapo hapo kutengeneza nafasi kutokea winga ya kulia.
Samatta alipaswa kuanzia kushoto kwenye nafasi ya kijana Farid Mussa na mshambuliaji wa kati angekuwa Thomas Ulimwengu wakati kiungo cha ukabaji wangecheza Mkude na Himid Mao huku ukimpunguzia kazi ya ukabaji kijana mdogo Mudathir Yahya ambaye angeweza kusaidia kulainisha mipira na kuipandisha timu.
Kutokana na tamaa ya kushambulia, umewapa kazi sana Himid Mao na Mudathiri kuwakaba Algeria kiasi cha kusababisha timu kufa katikati, huku muda wote mipira ikiwa miguuni mwa Algeria na kuwapa wakati mgumu sana walinzi wetu. Narudia tena pamoja na ubora Algeria lkn Mkwasa nabenchi lako umewarahishia sana kazi.