Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Jamani mlio Bongo tuwekeeni pdf. document ya hii tenda kesho mkiingia kazini.

Mimi nafahamu updates za websites za Bongo ni JF pekee ambayo iko updated every second nyingine nyingi hasa za serikali inachukua one light year kuwa up-dated.
 
GT

Tangazo la Tenda hilo hapo juu. Mwisho tare20/June/2008

Thanks Pascal
 
GT
kuhusu kuomba radhi katika kujaribu kupotosha umma kwa mara nyingine(mara ya kwanza ulikuwa na kusema MEMBE anayo kampuni na RAMA MAKALIO,ambayo mwenyewe kwa ungwana wako na heshima uliojivunia mwenyewe humu ndani ukaja kuomba radhi,naukaungwa mkono na wachangiaji wanaokudhamini kama mwenzao),hila imeonekana wazi wewe tatizo lako kubwa sio vitambulisho,bali ni MEMBE,je wewe katika mtazamo wako katika huu mjadala wa vitambulisho,umewatendendea haki watu wanaodhamini mchango wako unapoutoa?
naomba upime uzito mwenyewe kilongola
 
Kwani hivi vitambulisho vinamaana sana kwani kwetu?

Toka tumeanza kuishi bila vitambulisho kuna bugdha wananchi tumepata?

Je hizo pesa zote zingegaiwa kwenye halmashauri wilaya zote si zingejengwa kwa kiwango cha lami?

Kwa maana wabongo kwa dili usikute tayari dili limesha chongwa hapo watu wakaneemeka noi bora kuvikataa kwani ss watanzania tunajijua hata aingie mtusi/mcongo/mzambia wote tunawajua vitambulisho vya nn hapo?
 

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=9262&page=23
 
Naombeni wakuu swala hili lazima tupime kwa undani tusije tukawa tunawatengene MAFISADI ulaji tena kwani mkwanja uliotangazwa ni balaa pesa nyingi sana.

Lakini mbona zile card za kupigia kura watu tunzitumia sasa hivi katika shughuli mbalimbali kwa nn zile zisiendelee kutumika kama vitambulisho?
 
GT
napenda kusifu kitu kimoja kwako kwamba umeweka wazi nia yako hapa
https://www.jamiiforums.com/member.php?u=275

hila ni vema ungeanzisha thread ya kwako kuhusu MEMBE labda jina la hiyo thread inngesema "MEMBE IM YOUR WEB STALKER" or "MEMBE IM JUST OBSESSED WITH YOU" au labda therapy inaweza kukupa mwongozo ndugu mganganyika ,wale jamaa wanao toka kinu wa 118-118 wa uingereza bado wapo? wanaweza wakakupa shavu,hila sijua Kama NHS wanaweza kukulinda.

Sijui umeingiliwa na nini mngwana ulukuwa mtu wakupost mikiki,sababu zako wewe na MEMBE mnazijua wenyewe sizani kama wewe ungependa zijulikane ,mie binafsi nisingependa kuzijua

msaada wangu kwako kwenye hili ni number ya MEMBE mpigie mmalizane chukua kalamu mngwana +255 754 815815

Maanake unayumbisha huu mjadala muhimu sana katika taifa letu kama kuna mazuri ya hivi vitambulisho tuyajue kama kuna mabaya pia ni vema kuya jua mapema,kuna watu wameleta hoja za msingi je vitabulisho wapewe kina nani husan jamii ya kiafrica na wasipewe wengine kuangalia nyakati na kadhalika,

mngwana bado unanafasi na huku chimboni kwetu heshima bado inaendelea Mtaalamu wa mikiki GT
 
Ndg zangu wa JF,

Ni vizuri tukawa na utaratibu wa kufikiria kabla ya kutenda, kuliko kutenda halafu ndio tunafikiria, kwani madhara ya kufanya hivyo ni zile gharama za kujitengenezea utetezi wa pale palipoharibika.

Nimefuatilia kwa kina sana mjadala wa mradi wa Vitambulisho, nimeshangaa kuona hata wale wengine walioko nje ya Tanzania wanaupinga. Nina mashaka nao.

Tumekuwa tukipata malalamiko makubwa sana wakati wa uchaguzi. Kila chama kilichshiriki ktk uchaguzi kimekuwa kikilalamika kuwa kimeibiwa kura. Chombo pekee cha kudhibiti wizi wa kura na kupunguza malalamiko ni Kitambulisho.

Tumeshuhudia wanafunzi Mlimani wakilalamika kuwa kuna watu wamepewa mikopo ya Elimu kwa upendeleo au pesa kuliwa kwa kudai zimetumika ktk malipo ya wanafunzi. Bila Kitambulisho hadithi hii haitaisha.

Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa mahesabu ya Serikali ipo wazi kuwa kiwango cha mishahara hewa ni kikubwa sana ktk sehemu kubwa ya Serikali. Ni kitambulisho pekee ndio kitakachopunguza ubadhilifu huo.

Hivi ni kweli Serikali inaweza kufanya mipango yake ya maendeleo vizuri bila kuwa na takwimu iliyo sahihi? Itawasaidiaje wananchi wake waliokubali kukaa na wakimbizi kama hakuna kitu cha kuwatambua?
Kitambulisho kitatolewa BURE kwa kila Raia wa Tanzania. Halazimishwi kutembea nacho, ila atakapohitaji kukionesha itabidi afanye hivyo ndani ya masaa 24.

Kwanini tunajenga hoja "potofu" kiasi hicho? Maana kuna watu wamerudia tena kusema eti Membe anahusika na mradi huu. Membe yupo Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, anahusika vipi na mradi unaotekelezwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi?

Suala la Elimu kwa wananchi juu ya vitambulisho litafanywa baada ya mzabuni kupatikana, kwani ndio atakayesema itamchukua muda gani kutekeleza mradi, baada ya hapo ni LAZIMA pilot project ifanywe as a part of proof of the system then they will rollout.

Hapa nana kuna mtu ana hasira au chuki binafsi na Membe sasa anajaribu kutafuta kijisababu tu. Kama umetumwa ni vema ukarudi kwa waliokutuma na uwaulize vizuri, Membe anahusikaje ktk mradi wa Vitambulisho?

Mtu huitwa mjinga au mpumbavu kama atafanya jambo la kijinga au la kipumbavu.... utoto ni sifa kwani hata mtu mzima akifanya jambo la kitoto huitwa mtoto.

Napenda kuwahakikishia ndugu zangu kuwa "Vitambulisho" ni MUHIMU sana kwa nchi yetu. Nawashauri tujadiliane namna ya kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kupata Vitambulisho. Tuache "UDAKU" kwenye mambo nyeti ya nchi kwani tutabakia kuwa wajinga/wapumbavu huku wenzetu wakiendelea.
 
you are getting so emotional and touchy...i must have hit the nerve
 

zaidi soma hapa:
http://www.raiamwema.co.tz/08/03/12/3.php
 
GT,

Mimi nina swali dogo sana, na ningependa ulijibu toka moyoni mwako... Je, wewe una ugomvi na Mh. Membe? Je, Mh. Membe analijua hilo..???
 
Vitambulisho vya Uraia bomu jingine Shaka hiyo inatokana na ukweli kwamba tangu mwanzo mradi huo umesimamiwa na maofisa wa Serikali kutoka Wizara za Mambo ya Nje na Ofisi ya Rais (Utumishi) kama washauri na ambao sasa inaaminika tayari wamekwisha kulipwa kwa kazi yao hiyo. Taarifa zinasema pia kwamba sasa washauri hao kutoka serikalini wamejipanga katika nafasi za asasi zitakazokuwa zikisimamia mradi huo. Raia Mwema imefanikiwa kuona orodha ya washauri mbalimbali wa mradi huo ambao baadhi yao wako karibu na vigogo serikalini. Orodha ya washauri hao ni pamoja na Profesa Damas Muna said:
mngwana unaji qoute mwenyewe tena?
emotional.......mhh
nimekusoma,pole
 

GT
mgwana unaji quote mwenyewe tena?
emotional.......mhh
nimekusoma,pole
 
GT,
Leo nisingependa kutoa mapungufu lukuki yaliyo ripotiwa ktk gazeti la Raia Mwema. Ila ukitaka kufanya hivyo nitafanya mkuu ilimradi tu nijue baada ya kufanya hivyo kutakuwa na kitu gani cha manufaa.

Naenda kuwajibika, nitakuwa tayari kuchangia hoja hii pale nitakapotakiwa kufanya hivyo. Alamsiki....
 
Vitambulisho vya uraia, ufisadi unaopikwa

ZAIDI SOMA HAPA:
http://www.raiamwema.co.tz/08/05/21/3.php
 
GT,
Mkuu unajua ningekuwa nawe kama swala hili lingemhusisha MEMBE moja kwa moja na utengenezaji wa vitambulisho hivyo ikiwa ni pamoja na kusuka deal kama alivyofanya Lowassa na Richmond lakini hadi sasa hivi yote mlozungumza ndio utaratibu wenyewe unaotakiwa kufanyika.

Hizo kampuni za nje mnazoiziwekea mashaka nitafurahi sana kama mtaweza kuonyesha kwamba hawana uzoefu wa kutengeneza Social Security hawana kwa sasbabu hapa sio utengenezaji wa vitambulisho tu kuna database la nguvu linatakiwa lenye uwezo mkubwa kitu ambacho tanzania hatujawahi kuwanacho wala hatuwezi kuwanacho kwa kutumia makampuni ya ndani.

Pili ID card hazihusiani na wapiga kura hata kidogo kwa sababu kupiga kura sio lazima kwa kila mwananchi. isipokuwa upigaji kura utaweza kufanikiwa zaidi ikiwa kila mwananchi ana kitambulisho bila kujali kabila au rangi isipokuwa vitambulisho hivi havitakuwa vyote sawa kwa raia na wale wahamiaji ambao bado hawajapata Uraia.

Hivyo kulingana na sheria zetu za kura haiwezekani mtu kujiandisha kupiga kura kama huna kitambulisho cha Uraia...Hii ni ktk kuepuka wagombea kwenda vizia Wahutu huko Ngara.

Kwa hiyo hao walioandika hapo juu wakitaka vitambulisho hivyo viambatane na records za Upigaji kura wamechemsha sana kwa sababu hakuna vitambulisho vya namna hiyo..Upigaji kura ni hiari ya mtu, record hupatikana tu pale mtu atakapo piga kura, namba yake haiwezi kurudiwa na mtu mwingine.

Amini mkuu tunahitaji sana vitambulisho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…