Ok.. basi inawezekana bunge halitavunjwa kama wana mpango wa Ijumaa lakini duniani vyote vinawezekana. Kwa sababu itakuwa muhiimu kwake kuunda timu mpya kabisa kuanzia Bungeni na hivyo kuhakikisha anajipatia kundi jipya la kumsaidia ushindi 2010.
Kikwete akivunja Bunge sasa na baada yake mchakato mpya kuanza kutafuta wagombea ukaanza na yeye akagoma kuwaunga mkono wagombea kama kina Lowassa, Rostam n.k au kinyume chake kina Selelii, Mwakyembe na Kilango etc basi anaweza kujijengea heshima kubwa.
Catch 22 ya hapa ni kuwa akivunja Bunge na yeye anapoteza Urais!!
....Kwa taarifa ni kwamba KESHO KUNA KISHINDO
Hotuba itakuwa JF live. I will take that serious mkuu Yebo Yebo!
Nina mpango wa kuirusha live...
Hotuba ya Rais kwa mujibu wa Ratiba ita kuwa saa 4.45 Asubuhi saa za Afrika Mashariki,baada ya Gwaride Rasmi. Tuwe pamoja katika safari hii muhimu.Itaanza muda mnfupi baada ya saa 4 kamili kwa saa za afrika mashariki
Wapenda nchi, lets give him benefit of doubt. Lakini kwa kweli uvumilivu una mwisho. Iwapo hakuna jambo 'tangible' hotuba tupu ni lazima ikemewe na wote wapenda nchi hii kwa ukali wote unaostahili.Hakutakuwa na jipya katika hotuba hiyo. JK ni fisadi maana ameingia madrakani kwa kufanya ufisadi kupitia kwa akina fisadi Rostam Aziz, Fisadi Manji, Fisadi Subash na mafisadi wengine kibao chini ya uongozi wa mtandao wao ukiongozwa na Membe na wengineo. Anajua fika akipambana na mafisadi basi na wao watamtosa kwa kuanika uozo uliofanyika ili kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha mgombea wa chama cha mafisadi. Anajua fika kama bila kufanya ufisadi leo hii asingekuwepo Ikulu. Kwa hiyo waungwana kwa mara nyingine tena msishangae kama fisadi JK atashindwa kukonga kiu yenu ya kupambana na ufisadi, miradi bomu ya madini na uozo mwingine chungu nzima.
Wapenda nchi, lets give him benefit of doubt. Lakini kwa kweli uvumilivu una mwisho. Iwapo hakuna jambo 'tangible' hotuba tupu ni lazima ikemewe na wote wapenda nchi hii kwa ukali wote unaostahili. Ni vema wapambe wake kama wako humu, wamfikishie ujumbe huu mapema, bado ana masaa ya kufanyia hotuba yake modification, japo sina hakika kama anao tena masaa ya kuchukua hatua. Tired of empty words! Taarifa zote tulizonazo zinatosheleza kwa hatua hivyo, hakuna sababu ya kisingizio chochote kwa sababu yeyote ile. EPA, Twin Tower, Ufisadi ndani ya Debt Conversion Scheme ( na hapa siongelei madeni), ufisadi ndani ya CIS (Commodity Import Support), maswala yote ya TANGOLD, MWananchi Gold Company, Meremeta, Deep Green Finance Company Ltd na mengine mengi. Hatuwezi kuendelea kuwa na Serikali isiyo na meno, hata kama inauma, ukweli lazima usemwe, na uchukuliwe hatua. Dhamira njema itajulikana tu kwa hatua dhabiti. Nchi Sovereign, haiwezi kuachia Investigations zake kufanywa na SFO (ambao wanafanya upelelezi kwa mujibu wa Sheria za Uingereza)! This is mockery of democracy. Kama nilivyosema, ninampa Mhe. Rais Benefit of Doubt, lakini Expectations are very high, and ought to be met! It is the minimum I and all those who wish this country well expect.
MKJJDr. Slaa mood ikoje hapo?
kesho kisura,hatajaribu kujibu mashambulizi dhidi ya serikali yake kwa wale wote wanaoipaka matope juu ya ufisadi,na hivyo kuhitimisha mjadala yote ambayo iliundiwa tume.Hapo ndipo utakuwa mwisho wa mjadala ndani ya bunge na nje ya bunge.
Mwisho atawaomba watanzania wajishughulishe na mambo yanayo waletea maendeleo na kuachana na malumbano ambayo yanawapotezea muda.pia atalishukuru bunge kwa kuwa msitari wa mbele ktk kuikosoa serikali.
Wabunge watashangilia sana kisha baada ya hotuba kwisha watatoka wakisemezana pembeni.
Kisha CCM wataanda maandamano nchi nzima kuhunga mkono hotuba ya raisi.2008 ndio itakuwa imekwisha na watu wataanza kujiandaa na uchaguzi.
Mambo Jambo huyu jamaa amejivua nguo kuwa ni mtu wa ndani ya TAKUKURU tena ngazi ya Ukurugenzi, kwa kuwa amehusika katika kupitisha takwimu zilizotakiwa na IKULU katika draft speech yao, ambayo si lazima wazitumie katika kuandika speech. Angekuwa makini kidogo angefanya uchambuzi hata wa EPA ili angalao kuonyesha kwamba hatoko TAKUKURU.
Mhusika huyu mwenzetu hapa JF, amekuwa na mchango mzuri sana katika kutoa taarifa za kusaidia mapambano dhidi ya ufisadi ikiwa ni pamoja na ile taarifa ya ununuzi wa nyumba ya Mkurugenzi Mkuu wake, Edward Hosea, lakini pia alichemsha kwa kushindwa kuficha nyayo zake hadi akajulikana.
Awe anawasiliana na watu kama kina invisible ama mwanakijiji kabla ya kupost ili wamsaidie kuweka bila kuacha nyayo.
Kwa taarifa ni kwamba KESHO KUNA KISHINDO
Dr. Slaa vyovyote vitakavyokuwa kesho ni muhimu wabunge mdai hiyo ripoti ambayo yeye hakuiagiza iwekwe hadharani ili hatua zitakazochukuliwa zionekane kuwa zimeendana na ripoti hiyo. Hilo moja, la pili naamini wabunge mna haki ya kuwaita kina Mwanyika, IGP na Hosea (wawe na nyadhifa zao au la) kuwahoji kuhusu ripoti hiyo na kwanini hawakuchukua hatua. Naamini hii inaangukia katika nyinyi kuisimamia serikali.