Wapenda nchi, lets give him benefit of doubt. Lakini kwa kweli uvumilivu una mwisho. Iwapo hakuna jambo 'tangible' hotuba tupu ni lazima ikemewe na wote wapenda nchi hii kwa ukali wote unaostahili. Ni vema wapambe wake kama wako humu, wamfikishie ujumbe huu mapema, bado ana masaa ya kufanyia hotuba yake modification, japo sina hakika kama anao tena masaa ya kuchukua hatua. Tired of empty words! Taarifa zote tulizonazo zinatosheleza kwa hatua hivyo, hakuna sababu ya kisingizio chochote kwa sababu yeyote ile. EPA, Twin Tower, Ufisadi ndani ya Debt Conversion Scheme ( na hapa siongelei madeni), ufisadi ndani ya CIS (Commodity Import Support), maswala yote ya TANGOLD, MWananchi Gold Company, Meremeta, Deep Green Finance Company Ltd na mengine mengi. Hatuwezi kuendelea kuwa na Serikali isiyo na meno, hata kama inauma, ukweli lazima usemwe, na uchukuliwe hatua. Dhamira njema itajulikana tu kwa hatua dhabiti. Nchi Sovereign, haiwezi kuachia Investigations zake kufanywa na SFO (ambao wanafanya upelelezi kwa mujibu wa Sheria za Uingereza)! This is mockery of democracy. Kama nilivyosema, ninampa Mhe. Rais Benefit of Doubt, lakini Expectations are very high, and ought to be met! It is the minimum I and all those who wish this country well expect.