Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Fundi mchundo,
Vitambulisho vya uraia huwa ni daima tofauti na Passport, kitambulisho chga kazi ama driver's licence ambavyo unahitaji ku renew baada ya muda fulani.

Kutokana na maelezo yako yaliyotangulia inaonyesha wazi hufahamu kabisa matumizi ya vitambulisho hivi tunavyoongelea hapa.

Namba unayoipata ni namba yako wewe hadi kufa haiwezi kupewa mtu mwingine yeyote!
[/QUOTE]

Ndiyo maana napapenda hapa mahali. Watu hawachelewi kukuweka sawa. Haya basi!

Namba unayozungumzia ni tofauti na kitambulisho. Social security number ninavyoelewa mimi haina uhusiano na uraia bali ukazi (residency). Pamoja na kuwa namba hii ni ya kudumu lakini kitambulisho (lile gamba unalopewa) linabidi liwe renewed, hii ni kwa sababu wanahitaji kuupdate record zao (sura zinabadilika n.k.), uchakavu n.k. Sijui Marekani wanafanyaje lakini najua nchi nyingi za ulaya identity card inakuwa renewed baada ya kipindi fulani.

Au, Mkuu, unataka kuniambia kuwa ukizaliwa na kupewa kitambulisho, utadunda nacho hadi utakapoingia kaburini? Au hicho kitambulisho si kwa watoto?

Sasa kwa wewe unayeelewa vizuri, basi naomba unifahamishe, hiki kitambulisho ni cha aina gani?
 
Ndiyo maana napapenda hapa mahali. Watu hawachelewi kukuweka sawa. Haya basi!

Namba unayozungumzia ni tofauti na kitambulisho. Social security number ninavyoelewa mimi haina uhusiano na uraia bali ukazi (residency). Pamoja na kuwa namba hii ni ya kudumu lakini kitambulisho (lile gamba unalopewa) linabidi liwe renewed, hii ni kwa sababu wanahitaji kuupdate record zao (sura zinabadilika n.k.), uchakavu n.k. Sijui Marekani wanafanyaje lakini najua nchi nyingi za ulaya identity card inakuwa renewed baada ya kipindi fulani. Au, Mkuu, unataka kuniambia kuwa ukizaliwa na kupewa kitambulisho, utadunda nacho hadi utakapoingia kaburini? Au hicho kitambulisho si kwa watoto?

Sasa kwa wewe unayeelewa vizuri, basi naomba unifahamishe, hiki kitambulisho ni cha aina gani?[/size]


Angalia facts zako kuhusu hilo la social security number. Vile vile angalia nchi ambazo wanavitambulisho mfano Afrika ni Kenya, Zimbabwe, South Afrika. Europe nchi nyingi isipokuwa UK.
 
Angalia facts zako kuhusu hilo la social security number. Vile vile angalia nchi ambazo wanavitambulisho mfano Afrika ni Kenya, Zimbabwe, South Afrika. Europe nchi nyingi isipokuwa UK.

Mbona tunaandikia mate? Social security number ni namba anayopewa mkaaji wa nchi ili kuthibitisha residency yake. hii number ni tofauti na kadi, ambayo mara nyingi kwa wenzetu, inakuwa na chip, picha, namba na tarehe ya matumizi. marekani wanazo kadi za aina tatu. Ingawa hapo mwanzoni mtoto aliyechini ya miaka mitano alikuwa hahitaji social security number, sasa hivi imeshushwa mpaka mwaka mmoja na wazazi wengine wanawaombea watoto wao wanapozaliwa tu.

Unaruhusiwa kuomba mpya mara tatu kwa mwaka ikiwa imepotea na utapewa mpya maximum mara 10 maishani mwako. http://www.ssa.gov/pubs/10002.html#types

Afrika Kusini wana Natinal Identity document ambayo unapewa ukiwa na miaka 16 na hapo awali ilikuwa na nafasi za uandikishaji wa kupiga kura, leseni ya kuendesha gari na leseni ya kuwa na silaha. Hivyo viwili vya mwisho sasa haviingizwa kwenye hii document. Kwa mifano mingine angalia hapa: National identification number - Wikipedia

Kilicho wazi ni kuwa hakuna standard ya hizi national identity numbers na card au documents unazotakiwa kuwa nazo ili kuthibitisha kuwa kweli una namba. Kilicho common ni kuwa namba hizi zinatumika kuthibitisha uraia na residence status yako. Na kingine ni kuwa namba siyo kadi au document, ni vitu viwili tofauti.

Namba ni ya kudumu lakini document au kadi siyo ( inaweza kupotea, kuibiwa, kubadilishwa kutokana na mtu kubadilisha jina, uraia n.k.) nchi nyingine hizo document zinatakiwa kuwa renewed na nchi nyingine sivyo. Sasa nyinyi mlio jikoni mtueleze hizi za kwetu zinaangukia wapi?
 
Social Security Number anapewa mtu yoyote hata kama sio resident, the matter of fact kuna wakati ilikuwa ikitolewa hata kwa wapita njia ili wafungue Bank Account tu, pamoja na kwamba ilikuwa inafahamika wazi kwa serikali ya US kuwa waombaji hao ni wapita njia tu, na hawakai pale moja kwa moja, unless kama hizo sheria zilibadilika,

Mimi nilipoenda huko na meli in the 80s, nakumbuka tulikuwa mabaharia kama wawili wabongo, tulikutana na mbongo mmoja pale Virginia, akatupa mikasi ya kuipata, tulijiandikia barua tu kwenye address yake, kesho yake tulipozipata tukaenda ofisi ya Social Security, wakatuuliza address yetu US, na Passport, basi within two weeks tukatumiwa Social, na ninayo mpaka leo na kila kipindi fulani wananitumia maelezo kuwa nikifikia umri wa miaka 65, nitakuwa eligible kukusanya malipo flani hivi, au kwamba nikifa leo, mke wangu atakusanya malipo flani hivi,

Sasa kama ingekuwa ni mambo ya Resident tu mabaharia wapita njia tungepewaje? Tupeni darasa manojua zaidi!
 
Are there different types of cards?

We issue three types of Social Security cards. All cards show your name and Social Security number.

* The first type of card shows your name and Social Security number and lets you work without restriction. We issue it to:
o U.S. citizens; and
o People lawfully admitted to the United States on a permanent basis.
* The second type of card shows your name and number and notes, "VALID FOR WORK ONLY WITH DHS AUTHORIZATION." We issue this type of card to people lawfully admitted to the United States on a temporary basis who have DHS authorization to work.
* The third type of card shows your name and number and notes, "NOT VALID FOR EMPLOYMENT." We issue it to people from other countries:
o Who are lawfully admitted to the United States without work authorization from DHS, but with a valid nonwork reason for needing a Social Security number; or
o Who need a number because of a federal law requiring a Social Security number to get a benefit or service.

Kutoka:http://www.ssa.gov/pubs/10002.html#types

Hii nimeitoa kwenye website niliyoiweka hapo juu. Ili uweze kufanya kazi marekani ni lazima uwe raia au resident (permanent au temporary). Wengine ni resident lakini hawastahili kufanya kazi (pengine wanafunzi, diplomats?, wakimbizi n.k) Zamani pengine ilikuwa rahisi kupata lakini si hu wakati wa post 9/11 ingawa bado illegals wanazipata.

Huu mfano ni wa marekani ambako nakiri sijawahi kugusa lakini najua ulaya kuna taratibu tofauti.
 
Darisalama, ambapo pengine ndipo pana neema nchini mwetu, watu wanatembea kutoka Kimara hadi mjini kwa kukosa nauli ya daladala.

Leo unataka kumlazimisha huyu bwana au bibi ajinunulie yeye, mke wake, watoto wake na wale anaowalea walioachwa yatima na dugu zake! Huyu yuko mjini. Je yule wa kijijini ambako hakufikiki isipokuwa kwa helikopta au boti?Au hivi vitambulisho ni kama pasi, kwa wale wenye uwezo tuu?

Leo wanatugelesha na database wakati wenzetu wa Brela wenye uwezo mkubwa bado wanatuza kumbukumbu kwenye mafaili! Nchi ambayo ni asilimia 10 ya watu wake ndiyo wenye access na umeme inataka kuleta mambo ya smart card? Ni vijiji vingapi vina studio za kupiga picha? Au mambo yenyewe yote ni digital nchini mwetu! Leo asilimia 31 ya wananchi wetu hawajui kusoma wala kuandika, hivyo vitambulisho vitawasaidia vipi? Hapana, nchi yetu ni masikini na hata tukijibhalaghua vipi ukweli unabaki hivyo hivyo. tunachangiwa vyandarua na wacheza sinema lakini hatuoni tatizo kutapanya mabilioni kwa miradi ya kipuuzi kama hii!

Amandla!

Fundi Mchundo umesahau kuwa kadi za wapiga kura zote zina picha ya mwenye kadi japo vijiji hivyo havina studio za kupigia picha. Vitambulisho ni muhimu na tena vinapaswa kuwa salama visighushiwe kirahisi, maana hilo litakuwa tatizo lingine.

Labda tulilie kuhusu gharama ya kitambulisho hicho, pengine serikali igharamie kama ilivyofanya kwenye vile vya kura. Suala la mtu kutokujua kusoma wala kuandika si kigezo cha kumnyima kitambulisho. Kule kutokujua kusoma na kuandika tayari ni kiashirio cha uduni wa hali yake, sasa unapotaka huyu asiwe na karatasi yoyote ya kumtambulisha kwa maelezo ati "kwanza hajui kusoma", ni kuzidi kumdhalilisha na kumdunisha, unamfanya awe duni kuliko hata wale sokwe wa Gombe ambao wanajulikana kila mmoja kwa jina na mahali alipo!

Vitambulisho vya uraia ni haki ya kila raia, tuache ubaguzi wa kipuuzi wa kudai kuwa kama hajui kusoma wala kuandika basi hastahili kitambulisho, hii ni arrogance ya ajabu!
 
Suala la mtu kutokujua kusoma wala kuandika si kigezo cha kumnyima kitambulisho. Kule kutokujua kusoma na kuandika tayari ni kiashirio cha uduni wa hali yake, sasa unapotaka huyu asiwe na karatasi yoyote ya kumtambulisha kwa maelezo ati "kwanza hajui kusoma", ni kuzidi kumdhalilisha na kumdunisha, unamfanya awe duni kuliko hata wale sokwe wa Gombe ambao wanajulikana kila mmoja kwa jina na mahali alipo! Vitambulisho vya uraia ni haki ya kila raia, tuache ubaguzi wa kipuuzi wa kudai kuwa kama hajui kusoma wala kuandika basi hastahili kitambulisho, hii ni arrogance ya ajabu!

Kithuku! Bado haujanieleza faida ya hiyo kadi kwa mwananchi wa kawaida! Mimi nimevuka nusu karne na sijawahi kuwa na kadi ya uraia, kadi ya chama n.k . na sijapata tatizo lolote hapo nchini. Kwa wale wanaokaa mijini kuna vitambulisho vya kila aina (leseni ya uendeshaji, kadi ya chama, kitambulisho cha kuajiriwa n.k.) ambavyo vinatumika.

Na kama sababu ni kushindana na wahamiaji haramu, hawa wanakuwa ni rahisi kujificha mjini na si vijijini. Kijijini, mgeni anatambulika bila hata kuuliza kitambulisho. Wakiamua kumficha ni kuwa anafaida kwao na sioni sababu gani serikali iwaingilie kama hajavuja sheria nyingine zaidi ya hiyo ya uhamiaji!

Ninapozungumzia kutokujua kusoma ni kuainisha jinsi tunavyojichanga kwenye priorities. Nchi yetu ilikuwa inasifika kwa kuwa na watu wanaojua kusoma na kuandika lakini si hivyo tena! Kwa msingi huo huo nikaunganisha hiyo ya chandarua. Sasa hawa jamaa tumeshindwa kuwapatia nafasi za kusoma, kuwapa huduma bora za afya tunawapelekea vitambulisho ati ndiyo watakamilika kama raia na kuweza kutembea kifua mbele kuliko wale sokwe wa Gombe ambao angalau Mama Goodall anawapigia kifua! Huu mimi naona ni upuuzi.

Ni kama yule mama aliyechinjwa ufaransa alipouliza kwa nini wananchi hawali keki kama hawana mikate! Itafika wakati pengine mradi huu uta'make' sense lakini si sasa. Hivyo vijisenti tuvielekeze mahali ambapo vitamtoa mwananchi wetu kutoka katika hali duni aliyokuwa nayo.

Sidhani kama unaweza kulinganisha mfano wa kadi hizi na hivyo vitambulisho vya kupigia kura. Vitambulisho hivyo vya kupigia kura ni kwa wale wenye umri wa zaidi ya miaka 18 na si compulsory. Ushahidi ni idadi ya wapiga kura ukilinganisha na wanaostahili kupiga kura. Hizi kadi za uraia zitakuwa compulsory na ni kwa kila mtu (ama sivyo hazitakuwa na maana).

Amandla!
 
Will Tanzanians get those ID cards?
Adam Lusekeso
Daily News; Wednesday,May 28, 2008 @08:10

I GATHER that national identity cards will be ready by the end of December 2009. Plaudits will applaud. I don't. For once, the whole thing will cost 182 billion/-. Now such huge figures of money is a magnet for unsavoury characters like the ones who stole 133 billions of EPA monies.

Coordinator for the project, Dickson Maimu, has said that the tender is open to any company qualified to do the job adding: "I urge companies to compete for the tender, and I assure everybody that the tender process will be free, fair and transparent to all, provided the identity are ready in time."

Knowing Bongo, the tender might have already been awarded to one of the top officials in some party or government.

Just like in the EPA scandal. This time the top government officials might go and register a company either in South Africa or Mauritius. The name of the company has to be fancy, for most of Bongo officials are suckers for foreign names.

I just wonder if Richmond ID Card Manufacturing Company Ltd has applied in the tender. Or another company, the Kagoda ID Card Company Ltd, might also have competed for the tender. But I think, Tangold ID Company Ltd will apply to bag the tender. As you know Tangold, is wholly owned by the government.

But the wives and children of those signing for it can inherit the company! Just mark my words, dear readers, this 182 billion/- will not go without trouble. There is a national feeling that as a people we are being diddled senseless by ruthless conmen wearing natty suits.

Those who badly want the tender might be given suggestion on how to land the deal squarely on their laps. If they want it badly, then they will have to,er, 'contribute' to the party coffers while the party is readying for general elections for the year 2010. Now, as you know, the party plans to win by a landslide (kwa kishindo!).

They have to buy all those khangas for mamas who thankfully get a pair every five years. The caps, t-shirts and scarves will go to all those guys walking semi naked for four years. They are rewarded a t-shirt after every five years. There will be a lot of dosh floating around in the next five years. There will be some money to raise 'awareness'. There will be some dosh in the acquiring of offices, needless to say at highly inflated rent. In Kiswahili, the whole thing smacks of 'Ulaji'! I am definitely not doubting Mr Maimu's integrity.

But he had better keep his troops in line. Otherwise, we will not be having ID cards in the next five years. There will only be accusations and counter-accusations and a lot more 'shangingis' on our roads!

Mbwene2@yahoo.com
 
BuBu ataka kusema,
"I urge companies to compete for the tender, and I assure everybody that the tender process will be free, fair and transparent to all, provided the identity are ready in time."
Wait a minute, Tender has just been open, where does that bill of 182/b come from!..
 
25177793.jpg
 
Lakini kweli Fundi Mchundo amekaribia kufanikiwa kunishawishi kuhusu priorities. Nasema amekaribia, kwa maana bado naamini kuwa vitambulisho ni muhimu, lakini kwa kweli tutazame priorities. Wahenga walisema "kata pua uunge wajihi", na wazungu "Cut your coat according to your money". Huwezi kutaka kushonewa "tuxedo" wakati hela yako haitoshi hata mita moja ya kitambaa, na pia ni kichekesho kununua tai ya "silk" ya bei mbaya, wakati hata shati au japo fulana tu ya kujisitiri huna.

Jana nimesoma kwenye vyombo vya habari kuwa mabingwa wa fani ya tiba na upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili wameanza kutoa huduma ya upasuaji kwa kwa wagonjwa wenye maradhi ya moyo, ambayo awali ilikuwa inapatikana tu nje ya nchi. Nikasoma kuwa gharama zilizotumika (vifaa vinavyohitajika) kuiwezesha Muhimbili kutoa huduma hiyo ni shilingi bilioni moja. Basi nimefanya hesabu nyingi sana kuhusu hiyo tarakimu. Kumbe ile hela iliyokwibwa kule BoT katika EPA ingetosha kututengenezea vitengo 133 vya namna hiyo, yaani kila hospitali ya wilaya ingekuwa nacho. Na leo tunaambiwa gharama ya vitambulisho vya taifa ni sh bilioni 180, yaani hiyo inatosha kueneza huduma hiyo ya matibabu ya moyo bila shaka na maradhi mengine nchi nzima (wilaya 121), na bado zingebaki nyingi tu za miradi mingine.
 
Nimesoma kwa makini yale maoni ya wachangiaji wenzangu na mimi nikaona nimwage kidogo kuhusu faida na hasara za hizi kadi za utambulisho.

Lakini kwanza ningependa kuelezea kuhusu umuhimu wa kuwa na watu (wataalam wa kuchapisha hizo kadi) na system nzima (National Identity Register).

Ni lazima tukubali kwamba Tanzania haina kampuni inayoweza kuchapisha kadi hizo kwa uimara na ubora unaotakiwa, na kwa kuzingatia hilo wizara husika ikaweka sifa za mgombea tender na kikubwa zaidi imetiliwa mkazo suala la uzoefu.

Kwa hio bila ubishi hapa kampuni za South Africa, UK au USA ndizo zitakazoweza kufanya kazi hio kwa standards zake. Na kwa ufahamu wangu ni kwamba wamarekani ndio wanaoongoza kwa sasa katika technology hio kwa kuzingatia kwamba wao ndio wanafanya kazi nyingi za aina hio hata nchini UK.

Na ikiwa kutahitajika unafuu zaidi basi kampuni yoyote ya South Africa itaweza kupewa kazi hio.

Sasa nikirudi katika hizo kadi, mimi nikiwa naishi ughaibuni kwa muda mrefu, nimekuwa na kadi za aina nyingi tu, National Insurance card, Driving Licence, kadi ya afya ya Ulaya (European Health Insurance card),kadi zote za benki yaani debit na credit cards, na passport yangu ya Tanzania.

Katika zote hizo ni passport yangu ambayo ina sticker inayoonesha aina ya ukaazi wangu na driving Licence ndizo naweza kutumia kama aina ya utambulisho wangu ingawa zinaweza kuwa zimerudufiwa na matapeli ambao wanakuwa wabekwiba details zangu.

Lakini National Insurance Cards na kadi zingine zoote, hazimpi mtumiaji haki ya kudai kwamba yeye ndie katika hali yoyote ile ya kutakiwa kuthibitisha uraia au hadhi yake kama mkaazi halali au mhamiaji awe halai au haramu.

Kwanini serikali inaleta kadi za utambulisho za kisasa?

Hili ni swali ambalo hata katika nchi zingine ni lazima raia wake wamekuwa wakijiuliza. Kadi hii ya utambulisho ni hatua ya serikali kutaka kudhibiti na kufuatilia (kwa ukaribu na umakini) taarifa za raia wake.

Hii haiusiani na kwamba raia huyo anajua kusoma au la bali ni kuhakikisha kila raia aliezaliwa Tanzania na anaezaliwa leo anakuwa na kadi hio.

Kwa hio hapo serikali ina wajibu wa kusema ni taarifa gani zitawekwa katika kadi hio ukiondoa tarehe ya kuzaliwa na mambo mengine, kwa sababu ni kadi ambayo itatengenezwa kitaalam kulingana na maelezo ya tangazo la tender.

Mimi ninaona faida zifuatazo endapo kadi hizi zitabuniwa kwa ajili ya raia wa Tanzania.

1.Udhibiti wa idadi ya watu na mipango yoyote ya maendeleo.

Hili limekuwa ni tatizo tokea tupate uhuru na linabidi litatuliwe kwa mapana yake.

2. Udhibiti wa uhamiaji, nafasi za ajira na huduma zingine muhimu za jamii.

Wahamiaji ndio wanaofaidi Tanzania kwa miaka mingi na hilo linajulikana, ajira pia inadhibitiwa kwa kubana vibali vya kazi kwa raia wa kigeni na huduma za jamii kama afya, elimu na makazi zinakuwa zinatolewa kwa kujua ni nani anastahili kupewa huduma hizo kwanza kabla ya raia.

3.Udhibiti wa UFISADI na mambo mengine kama utoaji wa mikopo katika mabenki iwe ya elimu, biashara na makusudio mengine ambapo kwa sasa ni kila mtu anaweza kuingia benki na kufanya hivo.

Je Serikali ipo tayari.

Nafikiri kuna pesa ya msaada imetolewa kwa jaili hio na kwamba waliobuni wazo hilo ndio wanapewa dhamana ya kuhakikisha UFISADI haupewi nafasi hapo.

Lakini pia serikali ingeanzia na kuhakikisha kwamba kila mjumbe wa nyumba kumi ana orodha ya raia wake wote.

Madhara ya kadi hizi.

1. UFISADI- watu wataweza kushirikiana kukwiba taarifa kuhusu kadi hizo na kuziuza kwa f"raudsters" kwa minajili ya kutimiza shughuli zao za kihalifu kama ughaidi, wizi wa kughushi katika benki, uhamiaji haramu au uuzaji wa nafasi za elimu katika shule, vyuo na katika bodi za mikopo

2. Ufujaji wa siri za watu (privacy) ambapo watumishi katika National Identity Register wanaweza kupatwa na majaribu na kuvujisha taarifa hizo kwa makusudio mabaya. Pia vyombo vya serikali kuwa na haki ya kupekuapekua humo ndani ya hio register bila idhini ya raia mhusika.

3.HALI YA MACHAFUKO- Nchi yetu imejaa raia wengi wa kigeni ambao ni haramu na wanajulikana. Mimi nendelea kuwakaribisha raia wa nchi zingine wenye matatizo kama vita na magharika lakini wale ambao wapo tu wanabangaiza sijui itakuwaje endapo hawataweza kupata nafasi ya kutambulika kama raia wa Tanzania na kukosa mambo yote mazuri ambayo raia wa Tanzania anastahiki.

Pia itabidi raia wale ambao wapo maeneo ambayo kwa sababu za kutafuta maisha, wamejikuta wapo maeneo ambayo sio waliyozaliwa.

Kwa mfano mtazamo wangu ni kwamba mjumbe wa nyumba kumi ndie awe mtu wa kwanza kuwa na taarifa za raia katika nyumba hizo kumi na wapi wanaishi na wanafanya nini.

Kwa ujumla nikiangalia kwa undani, naona serikali inaiga mambo ambayo kwa sasa bado hatujayafikia ya kutengeneza Register ya raia wa Tanzania. Ni muhimu kwa sasa serikali ikazingatia mipango mingine ya maendeleo ambayo mpaka sasa bado imekwama na sio kutafuta umaarufu wa kwamba eti na sisi moja ya nchi maskini sana duniani yenye raia milioni 37 tunabeba ID cards.
 
Serikali ina mpango wa kutengenaza vitambulisho vipya vya kiraia na zaidi ya billioni 100 zitatumika.zabuni imeshatangazwa mafisadi midomo wazi.
mtavimbiwa mafisadi
 
i hear there are 100 companies ready to bid ... dont know what criteria going to be used here ... nchi ya kitu kidogo????
 
i hear there are 100 companies ready to bid ... dont know what criteria going to be used here ... nchi ya kitu kidogo????

Kampuni 100 halafu vigogo wengi kutoka wizara ya mabo ya ndani.bonge la ufisadi.
 
mojawapo ni ya waziri wa mambo ya ndani?
kwa kukisia nani atashinda tenda?
 
mojawapo ni ya waziri wa mambo ya ndani?
kwa kukisia nani atashinda tenda?

Hii kali sasa.I used to idolise huyu jamaa lakini naona I was mistaken anachipukia kwenye ufisadi kwa kasi ya ajabu.
 
mojawapo ni ya waziri wa mambo ya ndani?
kwa kukisia nani atashinda tenda?

Hawa wanasiasa si waliambiwa na JK kwamba wachague siasa au ufanyabiashara hawawezi wakashika mawili yote kwa wakati mmoja, au ilikuwa ni danganya toto?
 
Hawa wanasiasa si waliambiwa na JK kwamba wachague siasa au ufanyabiashara hawawezi wakashika mawili yote kwa wakati mmoja, au ilikuwa ni danganya toto?

Kwani yeye mwenyewe JK ni mwana siasa ama mfanya biashara?, maana mkuu wa kaya nae haeleweki.
 
Back
Top Bottom