Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

mnafuatilia nini huo utumbo wa jana unaoitwa hotuba? huenda hawataitoa kwa sababu tatu

1.0, katika hotuba kikwete aliweka precedence mbaya sana, kuwa wezi wanaiba na wanaweza kusamehewa kama wakipewa muda wakarudisha walichoiba, tena bila woga anatoa precedxcence hii ndani ya bunge, sasa wale wezi waliovunja benki ya nbc, kwa mtindo huu warudishe yale mamilioni na kesi dismiss

2.0 amerudisha tena serikali ya tanganyika kwa kutamka wazi kuwa ndani kuna serilkali ya zanzibar na tanganyika na nje kuna serikali ya muungano.

sasa kweli kama huyo salva an kichwa juu ya mabega atathubutu kuanika pumba zote hizi, zije kumhukumu yeye na kikwete wake?

huenda anajaribu kuikarabati !
 
Mi nafikiri hotuba ya rais ni yale aliyoyasema jana bungeni. maandishi hayana maana, Kwa nini waandishi wasisikilize hotuba waliyoirekodi na kuiweka katika maandishi?

Hawa jamaa wa ikulu wanasita huenda kuna vitu muungwana kavi skip wakati wa kutoa hotuba. Maana hotuba ndefu kama ile lazima jamaa kuna yake aliyaweka ambayo Ikulu wanaona kwenye original hayapo.
 
Yaani tangu jana nimefuatilia na leo masaa zaidi ya 24 baadaye hawataki kutoa; hata Bunge hawakupewa nakala ya soft copy kwa hiyo inabidi watranscribe kutoka kwenye rekodi zao za Bunge ili kutengeneza hansard.

MMK, Mbona leo asubuhi spika wa bunge amesema kuwa kutokana na maombi ya wabunge wengi kutaka kuijadili hotuba ya raisi ameamua kuchapicha nakala ya hotuba hiyo iliyoachwa na raisi ili kila mbunge aweze kuipata na kuisoma then waijadili.

My question is, Inamaana Spika ameongopa kuwa wana nakala (soft copy) ya hotuba iliyosomwa na raisi jana?
 
MMK, Mbona leo asubuhi spika wa bunge amesema kuwa kutokana na maombi ya wabunge wengi kutaka kuijadili hotuba ya raisi ameamua kuchapicha nakala ya hotuba hiyo iliyoachwa na raisi ili kila mbunge aweze kuipata na kuisoma then waijadili. My question is..... Inamaana Spika ameongopa kuwa wana nakala (soft copy) ya hotuba iliyosomwa na raisi jana?

Please Give Me A Break!Nadhani akina Slaa na CUF baada ya kutoa msimamo wao its high time Wabunge badala ya kujadili hii hotuba wajadili ni jinsi gani anweza kuwa impeached ama forced to resign!

CCM for once hamna feeelings with the masses in these Country?Could you be so heartless kiasi hicho kwa watu waliowaweka in those positions?
Get him out of that seat!We are fed up!
 
MMK, Mbona leo asubuhi spika wa bunge amesema kuwa kutokana na maombi ya wabunge wengi kutaka kuijadili hotuba ya raisi ameamua kuchapicha nakala ya hotuba hiyo iliyoachwa na raisi ili kila mbunge aweze kuipata na kuisoma then waijadili. My question is..... Inamaana Spika ameongopa kuwa wana nakala (soft copy) ya hotuba iliyosomwa na raisi jana?

Wana nakala ya hard copy, wanakwenda kuipiga photo copy tu
 
Nadhani kweli hotuba ilikuwa na nyongeza ambazo Mh. Rais aliongezea kubadili hali ya hewa pale Bungeni mfano:
".........Mimi kama Rais nina mamlaka makubwa ninao uwezo wa kusema kamata Slaa........ Mwema atakwenda kumkamata bila kuniuliza kwanini nimetoa amri ya kumkamata. Baadaye ndipo atakuja ...Sasa Mzee yule mtu yuko ndani tumfungulie mashitaka gani. Nami nikasema mwache akae kwanza..."

Kaeneo haka ni porojo ili kubadili hali ya hewa ndani ya bunge nadhani wabunge walishaonekana ku-boreka na hotuba yenyewe akaona atoe kichekesho fulani ili waamuke waendelee kumsikiliza.
 
Leo tumepata nafasi ya kusikia mawazo ya kiongozi mkubwa wa upinzani Dr. Wilbroad Slaa akitoa mwitikio wake wa hotuba ya Rais. Katika kuendelea falsafa ya equal access ya KLHN siku ya Jumapili kuanzia kwenye saa nane za mchana EST (9:00PM EAT, -5GMT) tutakuwa na mmoja wa viongozi wakubwa kabisa wa Chama cha Mapinduzii ambaye naye atatupa mtazamo wake kuhusu hotuba hiyo.

Tutawatajia jina na cheo cha kiongozi huyo masaa machacha kabla ya onesho letu hilo.

Kama mipango itakuwa mizuri matangazo hayo pia yatarushwa na Bongo Radio. Stay tuned.
Wote mnakaribishwa.
 
Last edited by a moderator:
Tabu watu wanaosema hotuba mbaya wanataka kuchafua nchi tu sasa mnataka angeenda anza kutoa namba za gerezani wapewe wezi wa EPA. Hizo hela mmeshaambiwa sio za serikali, Serikali zimeziweka chini yake sasa hivi. Hizo hela hata watu wa JF mngeweza kuzipata mkengiztaka

Kikwete kawanyamazisha sana kwani Ushindi 2010 pale pale. Na kina slaa wakiongea zaidi kashawapa warning in a joking way so pole wana JF tafuteni lingine.
 
Sizzla
Its whether umetumwa,or ni madhara ya kuugua malaria kwa muda mrefu.Nway,may be ndo uhuru wa kutoa maoni!
 
Hotuba ya masaa 3+? Halafu pumba kwa wingi! Wataalamu fulani wanasema kwa dakika 10 za mwanzo unaihutubia hadhira yako. Dakika 10 zinazofuata unajihutubia mwenyewe. Baada ya hapo unamhutubia shetani.

Akina Salva na Januari hawamshauri au kumwelimisha JK juu ya art of speech?
 
WAKATI Rais Jakaya Kikwete, akionyesha huruma kwa watuhumiwa ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), Spika wa Bunge Samuel Sitta, amemkumbusha kuwa ni makosa kusimamia haki za binadamu kwa wahujumu uchumi.

Spika alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya hotuba ya Rais Kikwete bungeni, ambayo pamoja na mambo mengine iliwapa ahueni mafisadi wa EPA kwa kuwaongezea muda wa kuzilipa hadi Oktoba 31, mwaka huu.

Baada ya hotuba ya rais, Spika alimtaka kuongeza ukali kidogo katika masuala ya rushwa na ufisadi na kwamba Bunge litasaidia kuiweka nchi sawa.

"Hongera sana mheshimiwa Rais, umetoa hotuba nzuri, tumesikia, kuna mambo ya msingi, kuna hili la utawala bora, ukiongeza ukali kidogo basi sisi wabunge tutakusaidia. Lakini, wakati mwingine haya mambo ya kuweka visingizio vya haki za binadamu kwa wahujumu uchumi, yanakwamisha maendeleo ya nchi," alisema Sitta huku Rais akitabasamu.

Spika Sitta alifafanua kwamba, wakati mwingine kushindwa kushughulikia wahujumu uchumi kwa kisingizio cha haki za binadamu hurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Alisema nchi za Asia Mashariki zimeweza kupiga hatua kutokana na kuwa makini katika masuala ya rushwa na kwamba kama zingeendekeza visingizio hivyo zisingefanikiwa.

Spika Sitta ambaye chini ya uongozi wake, Bunge limetoa maamuzi mazito dhidi ya uhujumu uchumi, ikiwemo mkataba wa umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond, alisema kuwapo kwa ufisadi katika Mfuko wa Uagizaji Bidhaa nchini (ICF) ni ishara kwamba zinahitajika juhudi za kusafisha nchi.

Alisema hivi sasa mwananchi wa kawaida hawezi kuelewa akisikia eti wahujumu uchumi mabilionea hawakamatwi kwani kuwakamata ni vigumu.
 
pia katika hotuba ile Jk alikuwa anawatisha wabnge wakereketwa unakumbuka aliposema mara nyingine nikiangalia naona mnazidisha kunyanyasa mawaziri(Ana Kilango!!), pia alikua kama anwaahidi ulaji hivi.. ofisi za milioni 40 na akwaambia mambo yao sio mabaya sana.

Pia aliikana rasmi ilani ya chama kwa kusema si yake ni ya chama unakumbuka aliposema aliwaambia kwenye neck kuwa wasiweke idadi ya ajira milioni moja!!It is another way of saying it wasnt me, it is the party.

Mwisho akawadharau wananchi kuwa wanataka kunywa chai kwa mbunge na kwamba haiwezekani wabunge wawasomeshee watoto wao, sidhani kama kuna mwananchi anayataka hayo yote..nikakukumbuka aliyosema njombe kwamba hajaja kugawa pesa za bure kanan kwamba wamemwomba toka mfukoni mwake.

Kwa ujumla JK ana lugha ya kiburi sana zidi ya wananchi kwa sasa ya EPA siku nyingine.Nilitamani kumwuliza vipi foreign exchange losses ya hayo madeni je huo sio wizi, manake hizo dollar waliziconvert kwa rate za sasa wakati hiyo miaka 23 rate ilikuwa chini

vipi hapo serikali haijaibiwa.. auau na hizo si za serikali... jamani jamaa akiendelea hadi 2010 basi nchi imekwisha something must be done .. very fast
 
Binafsi nimesikiliza ile clip aliyokuwa akizungumzia mamlaka ya Rais aliyopewa na katiba na nimeshtushwa na kitendo cha wabunge kufurahia . Rais ana madaraka makubwa sana na nimefurahi ya kuwa yeye mwenyewe ameliona hilo.

Kitendo cha kusema anaweza kuamuru mtu kutiwa ndani bila ya kufunguliwa mashtaka ni kitendo cha hatari sana!

Kikwete inabidi awe wa kwanza kushawishi mabadiliko ya katiba kwani kipengele hiki hiki kinaweza kutumika kumuweka yeye mwenyewe ndani once he stepped aside.
 
Lakini kusema za ukweli mimi nawajua watu zaidi ya 2 ambao wameshachukuliwa hatua kutokana na huo mzozo wa epa ulizeni muambiwe , mfano yule kijana wa airport amenyanyanywa tenda ya parking , sikuhizi anatembelea na daladala

Shy acha longolongo, hakuna mtu aliyenyang'anywa tenda airport, actually ameingia mitini bila ya kukabidhi mapato yoyote aliyokuwa akikusanya kwa zaidi ya miaka miwili. Mapato sasa kwa kutumia vikaratasi tu ni zaidi ya ilioni mbili kwa siku. sasa piga mahesabu ya miaka miwili. Ameacha mitambo yote mibovu bila ya kuitengeneza kama mkataba unavyomtaka.

Na sasa anaingia kwa njia nyingine kupata tender ya kutengeza upya mitambo hiyo kwa malipo mapya na kampuni mpya. Labda unayemsema alikuwa front man tu wa huo ufisadi.........lakini sio yule mtoto wa nanihiiii........

Tanzanianjema
 
Hotuba ya masaa 3+? Halafu pumba kwa wingi! Wataalamu fulani wanasema kwa dakika 10 za mwanzo unaihutubia hadhira yako. Dakika 10 zinazofuata unajihutubia mwenyewe. Baada ya hapo unamhutubia shetani.

Akina Salva na Januari hawamshauri au kumwelimisha JK juu ya art of speech.

Mna uhakika kuwa ndio waliotayarisha hotuba hiyo? Hivi mnajua hata hotuba zinavyotayarishwa? Acheni kuhukumu watu bila ya chembe ya ukweli........

Tanzanianjema
 
Najaribu kupata nakala niisome vizuri, kwani kuna mambo yanahitaji kutafakari kidogo.

Hotuba hii imejaa data nyingi za kiuchumi ambazo ni economic indicaters muhimu, naimani approach hii ni nzuri na viongozi wengine wataiga, mfano aliposema dept/gdp ratio yetu sasa ni 25% ukilinganisha na 90% mwaka 2005 hii nidata muhimu kwa mwanauchumi makini.

Nimefurahishwa na approach ya kuanza kuukataa umaskini kwa kukataa kurudi HIPC, jambo hili jamani hebu tulipongeze.

Kuna hili la Imported inflation nadhani hapa anahitaki kwenda deep kidogo, mfano kitasa cha yale/union kimeuzwa shs 17,000/= tangu 2005 hadi leo bei ni hiyo hiyo. kigae cha spain 1' x 1' kimeuzwa shs 1200/= hadi leo. sealing board ya SA imepanda kutoka 9500/= hadi 12000/= ongezeko hili inawezekana nikutokana na kupanda kwa gharama za usafirishaji.

Hebu tuangalie locally produced goods katika soko la kamachumu, mchele umepanda kutoka shs 180/= mwaka 2005 hadi 1400/= todate, saruji imepanda kutoka 9800/= hadi 25,000/=, sukari kutoka 380/= hadi 1800/= vyote hivi has nothing to do with imported inflation.

Suala la diesel; iweje diesel kigali iuzwe franc 770 (= tshs 1400) na dar diesel iuzwe tshs2000! wakati rwanda wanapitishia diesel bandari ya dar!

Amesema alipofika Dodoma university alishangaa kweli, naimani alishangazwa na ujenzi uliomahili na sio uzuri wa students wanaosoma pale.
 
Hotuba ya masaa 3+? Halafu pumba kwa wingi! Wataalamu fulani wanasema kwa dakika 10 za mwanzo unaihutubia hadhira yako. Dakika 10 zinazofuata unajihutubia mwenyewe. Baada ya hapo unamhutubia shetani.

Akina Salva na Januari hawamshauri au kumwelimisha JK juu ya art of speech.

Kama nao wanajua nini maana ya ART of Speech.

Nasema hivyo kwasababu kuwa mwandishi wa habari hata kwa karne moja hakukufanyi uwe speaker mzuri.
 
unajua, nilisinzia mara tatu, wakati hotuba bado inaendelea. ilikuwa porojo tu, na haifai kuigwa na kiongozi yeyote.

pia naona Hosea aliamua kutoka nje baada ya kutokuwa acknowledged na Swahiba wake J.K
 
Back
Top Bottom