Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Jamani,

Wana CCM Dar wameandamana kwa wingi kumuunga mkono JK kuhusu hotuba yake aliyotoa Dodoma bungeni.

Wananchi wa Tanzania wanaelewa kweli hali ya kisiasa nchini?

Naomba maoni yenu

FP
 
popup zote tumeshashughulikia jana.. so sasa hivi kila kitu kiko sawa. Kulikuwa na tatizo moja la kiufundi. Mnakaribishwa.
 
I have tried and tried to do so but I have failed. It is such a subjective speech. It elicit subjective, if not biased, analysis. One thing is clear though. The President is far ahead. His strategies are too elusive for critical analysts. JK knows his constituent so very well!

Women constitutes more than 50% of the population. Peasants constitutes more than 75% of the population. In sum they both constitutes more than 80% of the voting population. So the guy was so far sighted when he hijacked the 50-50 gender parity agenda. He was more than cunning when he promised that EPA money will subsidize farming equipment. Surely he was acting so cleverly when he alluded to the billions of 'Bwana Fulani'!

Lets accept the fact that the Presider is not as short sighted as some think. In fact he has caught a glimpse of 2010 and beyond. He is such an astute political strategist. As such it easy to miss the mark by trying to analyze his speech objectively. From now onwards I will analyse what Muungwana says subjectively, albeit, critically.
 
Kuna watu wanadhani President aki-address nation, anatakiwa aongee lugha ya kuongea na Havard University!!!

In short wengi wako very wrong sana na analysis zao... anyway by the way they have never done analysis anyway.
 
Watanzania wengi wa leo siyo kama wale wa mwaka 47!! Wengi wana uwezo wa kuchanganua mambo kwa urefu na mapana na ndiyo maana Sitta pamoja na kuwa aliongea kwa dakika chache tu, lakini hotuba yake imewagusa Watanzania wengi kuliko ile ya mheshimiwa ya masaa matatu na nusu. Kama kaongea pumba lazima aambiwe kwamba mheshimiwa umechemsha!

Ingekuwa ni amri ya Watanzania wengi tungekwambia uachie ngazi sasa badala ya kusubiri 2010 maana nchi imekushinda! Hakuna haki ya binadamu wanaofanya ufisadi wa kuiba mabilioni ya shilingi. Hawa hawaombwi wala kubembelezwa ili warudishe kile walichoiba bali ni kupewa mkong'oto kama ikibidi waseme na kuwekwa mahabusi wakati wanaisaidia polisi katika uchunguzi wake. Haihitaji kuwa na Phd ili kuweza kuanalyse kwamba JK kwa mara nyingine tena ameongea pumba na kushindwa tena kuitumia vizuri nafasi hiyo ili kurudisha credibility yake pamoja na ya serikali yake kwa Watanzania

Date::8/23/2008
Kauli ya Spika Sitta yazidi kupongezwa kuhusu wahujumu uchumi
Na Waandishi Wetu
Mwananchi

WANANCHI mbalimbali wameipongeza kauli ya Spika wa Bunge Samuel Sitta kuwa wahujumu uchumi hawatakiwi kuonewa huruma na kuielezea kuwa imeifunika hotuba nzima ya rais Jakaya Kikwete.

Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesaema maneno machache aliyoyasema Sitta wakati wa kumshukuru Rais Kikwete, yameifunika hotuba nzima ya Rais huyo.

Wakati baadhi yao, wakiwamo wakulima wanampongeza rais kwa kuwakumbuka na kuwamegea fedha za EPA, wengine mmesema Sitta ndiye ameeleweka zaidi kwa kuwa kauli yake imekwenda sawa na matarajio yao.

Kwa mujibuj wa wananchi hao kauli yake ilipendekeza njia ya mkato ya kumaliza ufisadi kwa kuweka kando haki za binadamu, wakati ile ya Kikwete ilionyesha huruma kuwapa nafasi watuhumiwa wa EPA kupumua kwa kuongezewa muda kurudisha fedha walizoiba.

Kauli hizo za wananchi na ile ya Spika zimekuja baada ya Rais kulihutubia bunge Alhamisi wiki hii ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo tangu aingie madarakani.

Kwa ufupi wananchi wamemtaka Rais Kikwete kukumbuka usemi wa "Ukitaka kumuua nyani usimtazame usoni,".

Akitoa maoni yake jana, Shahib Bakari wa jijini Mwanza, alisema Rais alipaswa kutoa ufafanuzi unaoeleweka katika suala la EPA kama alivyofanya katika suala la muungano.

Alisema anashindwa kuelewa kwanini watuhumiwa hao wanabembelezwa badala ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani?

Mariam Simon alisema amefurahisha zaidi na spika wa bunge kwa maelezo yake kutokana na kumwambia Rais kuwa mkali kwa vile hicho ndicho alichotarajia katika hotuba yake lakini hakukipata.

"Kwa kitendo chake kusema kuwa amewaongezea muda nimebaini kuwa rais ameonyesha udhaifu katika kushughulikia ufisadi.

"Yapo ambayo naweza kusema nimefurahishwa nayo lakini si katika mafisadi wa EPA, hapa naungana na spika na ninampongeza kwani ametuwakilisha kwa kutoa mawazo yetu," alieleza.

Naye Jumbe Magati alisema kuwa maefurahishwa na maneno machache ya spika kuliko hotuba nzima ya Rais kutokana na kushindwa kwake kuwachukulia hatua mafisadi hao.

Magati alisema kitendo cha Rais kushindwa hata kuwataja kinakwenda sambamba na hatua yake ya kushindwa kuwachukulia hatua, na kitendo chake cha kuwapa muda wa kurejesha fedha walizoiba kinachochea na kukuza wizi wa mali za umma.

Kwa upande wake, Charles Kibangu alisema kuwa ameridhika na hotuba hiyo kwa rais lakini kumtaka kufanyia kazi maneno ya spika wa bunge Samwel Sitta kwa vile hiyo ndiyo kiu ya wananchi wengi.

"Sina taabu na hotuba yake lakini naomba tu Rais aifanyie kazi maneno ya spika wa bunge ambayo ameyatoa jana, kwani hiyo ndiyo kiu ya wengi na hasa wanapotaka kusikia" alieleza.

Wengine ambao hawakupenda kutajwa majina yao walipiga simu kwenye chumba cha habari kuwa Spika amesema ukweli, kwani suala la haki kwa wahujumu uchumi halileti maana huku wezi wadogo wadogo wakichukuliwa hatua za kisheria na kufungwa.

"Je, hawa hawana na haki kama za hao watuhumiwa wa EPA?" alihoji mwananchi mmoja aliyepiga simu.

Mwingine aliyetoa maoni yake kwa njia ya mtandao, amemtaka Rais atambue kuwa watuhumiwa wa EPA pia wana haki ya kushitakiwa huku wakihoji nini kinachoshondikana kwa Rais kuwauma mafisadi hao.

Alihoji haki za binaadamu alizoziongelea Rais ni haki gani, kama siyo kuwapa uhuru mafisadi wa kutumia walichoiba hao huku wakiendelea kudunda na tai shingoni.

Mwananchi huyo ahoji kuna shida gani kuwataja wahujumu uchumi wa EPA wakati enzi za Edward Sokoine wahujumu uchumi walifahamika na kuminywa.
 
muulize lile carpet mle bungeni alilolazimisha linunuliwe ulaya Kamisheni yake ilikuwa ni 10% au ngapi?

I hope hutompa leadking questions kama swahiba wako Dr Masau
 
Jamani,

Wana CCM Dar wameandamana kwa wingi kumuunga mkono JK kuhusu hotuba yake aliyotoa Dodoma bungeni.

Wananchi wa Tanzania wanaelewa kweli hali ya kisiasa nchini?

Naomba maoni yenu

FP
Wakimaliza hawa vihelehele wa sisiemu sisi tunaandamana kuipinga. Si hivyo tu?
 
Watanzania wengi wa leo siyo kama wale wa mwaka 47!! Wengi wana uwezo wa kuchanganua mambo kwa urefu na mapana Date::8/23/2008
Wakati baadhi yao, wakiwamo wakulima wanampongeza rais kwa kuwakumbuka na kuwamegea fedha za EPA

Wengine ambao hawakupenda kutajwa majina yao walipiga simu kwenye chumba cha habari

Mwingine aliyetoa maoni yake kwa njia ya mtandao


Wananchi wangapi walio katika kundi lile la 80% ambalo nimelitaja hapo juu wana fursa ya kutumia mtandao kutoa maoni yao? Wangapi wana uwezo wa kupiga simu (na sio kubipu) ili kutoa tu maoni? Hao waliopiga simu kwa nini wanaogopa kujitambulisha au ndio kina ninyi wateule wenye maslahi binafsi ya kulinda?

Bubu kitu ambacho wachambuzi hatuelewi ni kuwa Rahisi huwa haongei na sisi wachambuzi wa kisomi anapokuwa anatoa hotuba zake. Hotuba yake huwa inawalenga wapiga kura wake, yaani, hiyo asilimia 80. Ndio maana hata ahadi zake za 50-50, mfuko wa maendeleo ya jimbo na fedha EPA zimeelekezwa huko. Anajua wapi pa kuwakuna. Na hakika amekonga nyoyo zao!

Kumbuka Mzee wa Kiraracha aliwahi kulalamika kuwa watu wanamfagilia sana ila hawampigii kura kwa sababu hawajiandikishi kupiga kura. Je, wewe mchambuzi mahiri jina lako liko katika daftari la kudumu la wapiga kura? Kama halipo basi jua kwamba hotuba ya Rais haikuwa inakulenga msomi weye!Tutapiga kelele wee ila JK katuzidi akili maana anajua upopulisti, na si ukritikali, ndio unalipa!
 
Hivi kuna habari kama polisi iliarifiwa na kuruhusu maandamano hayo ? Maana kumekuwa na mtindo ambao si wakawaida kwa Polisi kutangaza habari za maandamano ya vyuma vya upinzani ,utawasikia wanafikiria ,wameruhusu halafu utasikia wameandika barua kuzuia mpaka itakapotolewa taarifa nyengine.

Wapinzani mupo ? mambo kama haya ni lazima muyachungue na kupata uthibitisho kuwa CCM waliandika barua kuomba kibali au kuiarifu polisi ,maana hi nchi si ya CCM peke yao wafanye watakavyo bungeni na huku mitaani mambu ni hayo hayo.
 
Thanks nimefika hapo lakini kwenye listen shows kuna Podcasts za zamani tu...
nenda chini kulia kabisa mkuu..utakuta kuna player pale chagua yoyote lkn tumia realpalyer ndio inasikika vizuri.....na chagua low bandwidth......
 
nenda chini kulia kabisa mkuu..utakuta kuna player pale chagua yoyote lkn tumia realpalyer ndio inasikika vizuri.....na chagua low bandwidth......

Thanks Yo Yo namsikia Mwanakijiji anaunguruma !!
 
Kasheshe,
Mkuu nadhani unajaribu kupotosha maoni ya wananchi ambao wametoa mchango wao na vizuri kama ukiutazama na kujaribu kuelwa wanachodai kabla hujawavamia.

Binafsi nadhani hotuba nzima ya Kikwete imegusia mambo ambayo sii muhimu kwao..mambo ambayo hayahusiani na umaskini wetu na jinsi ya kuundoa hali matatizo sugu yako wazi. Kila rais ktk National addressing huwa kuna vitu muhimu ambavyo vinategemewa kupatiwa ufumbuzi lakini kama maswala hayo hayataguswa badala yake yakazungumziwa maswala ambayo yanaendelea kwa ubaya wake wakipambwa na kufukizwa udi ndipo wananchi wanapohoji hotuba kama hizi.

Ufa wa ukuta wetu unajulikana lakini kitu anachokifanya Kikwete ni kutoziba ila kupaka rangi mpya juu ya rangi iliyochoka. Hapa huihitaji elimu ama lugha ya Havard.

Binafsi hadi sasa hivi sina hiyo hotuba isipokuwa nimepata vipande vipande ambavyo vinazungumzia zaidi jinsi ya kuimarisha Utawala ktk misingi ya demokrasia kama vile agenda kubwa ya Kikwete ni kusimamisha Utawala bora ktk mazingira ambayo yanaongozwa na viongozi criminals.

Ni ujumbe unaowataka hawa criminals wafuate sheria hali tayari wameisha vunja sheria kwa matumaini kwamba wataweza kubadilika. Sina maana Wabunge wote ni criminals isipokuwa unapota hoja inayohusiana na utovu wa maadili ya uongozi ni lazima kwanza uwajibishaji uwepo, kisha eleza sababu za wewe kuchukua hatua hizo kwa kuwaeleza njia bora wale wanaokaoshika nafasi hizo.

Tatizo la Kikwete ni kwamba hotuba yake imehalalisha Ufisadi na kaomba mwanzo mpya hali njia zote za Ufisadi bado zipo na halali, nyingine kasema hadi mwaka 2010 ndipo atakapo hakikisha mfumo mpya unatumika kufuta baadhi ya ufisadi uiopo as if sio big deal leo hii..yaani hao wahalifu bado wana muda wa kuendelea kujineemesha.

Kama utakumbuka niliporudi kutoka Tanzania mwaka jana nilisema viongozi wengi kama sio wote wanajishughulisha na kununua ardhi zenye matuimaini ya kuwa na rasilimali (madini), sasa wakati ushenzi huo unaendelea utakuja sikia sheria imepitishwa kwa wananchi kuhodhi ardhi (soil) kama mali yao na kwa uhakika viongozi wengi kutajiondoa ktk siasa baada ya kuvuna haki ya Watanzania wote.

Kisheria hizo ardhi wannazonunua leo zitakuwa zao na hakuna sheria ya kuwajibisha viongozi wanaotumia madaraka yao na wakati huu kujineemesha kwa ajili ya miaka ijayo. yaani yale ya Israel kwa Wapalestina yanafanyika nyumbani tena sisi waswahili kwa waswahili na sababu kubwa ni kwamba wananchi ni maskini na fdha ni kivutio kikubwa cha hawa watu kupoteza utirhi wao mkubwa.

Hakuna pendekezo hata moja ambalo nimeliona linahusiana na hali halisi iliyopo na linapatiwa dawa sasa hivi na haraka iwezekananvyo.

Tumesikia uchumi wetu umekuwa sijui asilimia 7 na ushee lakini ni asilimia ngapi ya makuzi hayo inaingia ktk mfuko wa serikali?...nikiwa na maana kuwa ikiwa madini yanauzwa billioni 500 kwa mwaka , kisha ktk hizo ni millioni 100 tu ndiyo inaingia ktk mfuko wetu hii ndio iwe sababu ya kutazama upya mfumo mzima wa pato letu kuliko kulinganisha pato la mwaka jana ambacho serikali ilipata millioni 90 kutokana na mauzo ya Billioni 400..kisha tukatumia maongezeko hayo kujisifia kukua kwa uchumi wakati tulitakiwa kupata zaidi ya billioni moja kama tungefuata taratibu za kisomi ktk makubaliano yetu.

Haya yote ni maendeleo yanayojitokeza ktk sekta zote kubwa iwe madini au Communication ambapo mtu anayeumia zaidi ni mwananchi na hakuna pato la maana kulingana na ukubwa wa investment yenyewe..

Tatizo kama hili Kikwete anawafahamu vizuri waliohusika kashindwa kuwachukulia hatua na kibaya zaidi ni kwamba ktk hotuba yake hakuna marekebisho isipokuwa uundwaji wa tume kuchunguza taarifa za tume nyingine.

Mika mitano hiyooo inayoyoma, sasa hivi tunaanza kuangalia ati mwaka 2010 (long term plan wakati shrt term plan imeshindikana na matatizo yanafahamika wazi....Hakuyagusia bali kayapaka rangi...
 
Binafsi hadi sasa hivi sina hiyo hotuba isipokuwa nimepata vipande vipande ambavyo vinazungumzia zaidi jinsi ya kuimarisha Utawala ktk misingi ya demokrasia kama vile agenda kubwa ya Kikwete ni kusimamisha Utawala bora ktk mazingira ambayo yanaongozwa na viongozi criminals..

Mkandara

Of course,

Mko wengi mnaojadili mzuka (kitu ambacho hamjasikia au kusoma) wengi tulisikiliza masaa yote... ndio maana objectively tunajua ameongelea mambo ya msingi mengi na ya maana sana kwa taifa.

Tatizo la wabongo... ni kwamba sasa hivi uchumi ni EPA... inasikitisha sana...

Mchambuzi makini kama wewe kudhani EPA ndio tatizo au suluhisho la nchi... ni dalili kwamba taifa letu lina matatizo makubwa sana...

kama hoja zote Mh. Rais alizoongelea hamjaziona kweli... taifa liko njia panda kutokana na wananchi wake yenyewe.

Au ninyi ndio akina Shamhuna?
 
Back
Top Bottom