Vitambulisho vya urai ni swala nyeti sana, na halianzi tu kwenye uwezo wa kutengeneza hivyo vikaratasi. Vikaratasi hivyo ni kama vile cheti unachopata baada ya kuhitimu shule. Kunamaswala ya msingi ambayo ni muhimu kwetu.
Kwanza, kampuni inayopewa tender, itatumia utaratibu upi kujua huyu ni mtanzania?
Pili, ni nani anayethibitisha urai wa mwananchi? Ni kampuni hiyo hiyo, kama hapana, taratibu za ushirikiano zikoje?
Tatu, uaminifu wa hii kampuni unapimwaje? Kwani watakuwa na habari nyeti za wananchi, ambazo zinaweza kutumika kwa masilahi binafisi.
Nne, Taratibu zipi zitatumika kutoa maombi ya kupatiwa vitambulisho hivyo? Tuwakumbuke watu wavijijini watashiriki vipi kwenye hili? Hii Kampuni itaenda mpaka huko ama?
Tano, gharama za kitambulisho ni zipi?
Sita, database ipi ijengwe kwa watoto wanaozaliwa sasa ili kuepusha ukosefu wa utuzwaji wa data wa kizazi chetu usijirudie?