Tanzania: Nchi pekee inayoshiriki michuano ya AFCON ambayo Television ya Taifa lake haioneshi michuano hiyo

Tanzania: Nchi pekee inayoshiriki michuano ya AFCON ambayo Television ya Taifa lake haioneshi michuano hiyo

Tetemeko la ardhi bukoba,ilionyeshwa na CNN. Taarabu ilikuwa imepamba moto siku ile TBC

Mechi ya Taifa Stars na Senegal ilionyeshwa na television ya taifa ya jirani zetu Kenya - KBC. Sisi tulimpeleka Ndugai. Macho yake makubwa zaidi ya tv.
 
Tangu Tido aondoke ndiyo basi tena,yaani watu wasiokuwa na ekispiriensi ndiyo wanapewa taasisi zinazohitaji mtu smart,Nadhani baadhi ya sekta ilitakiwa wateule wake wawe wanakuwa wanatambuliwa na katiba kama sieiji na wawe wanaapply siyo kuteuliwa na wanasiasa
 
Mkurugenzi wa TBC anaitwa Dr Ayubu Ryoba , ni msomi wa juu kabisa , ambaye ndani ya TBC ndiye muongoza njia , hawezi kukwepa lawama ya jambo hili.

Taarifa za awali zinaonyesha kwamba kitendo cha TBC kushindwa kuonyesha michuano ambayo timu ya Taifa lake inashiriki tena baada ya karibu miaka 40 kupita , si tu kitendo cha AIBU peke yake bali pia ni REKODI YA DUNIA , TBC kuona ni bora kutangaza vipindi vya propaganda vilivyokosa watazamaji Baada ya wananchi kustuka vya " TUNATEKELEZA " na kuacha kuonyesha AFCON kinaashiria umasikini wa Nchi kifedha na kiakili , jambo linalotia aibu mtu mmoja mmoja na linatia aibu viongozi mmoja mmoja na mwishowe linadhalilisha wananchi wote kwa ujumla .

Nakulilia Tanzania
usimlaumu Ryoba, unamkumbuka TIDO?!!?
 
Back
Top Bottom