Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Nimeonelea badala ya mawazo ya kulaumu, kulalamika, kulaani…...nitoe mawazo ya kujenga angalau kujaribu kuepusha matatizo makubwa yanayoisogelea Tanzania.
Ni matumaini yangu wakuu watayaona na angalau kuyafikiria.
Kila mfuatiliaji atajua uchaguzi uliopita, mithili ya chaguzi zote zilizopita lakini kwa viwango tofauti, haukuwa huru na wa haki. Hilo halina mjadala. Mjadala ni kwa nini uchaguzi huu una uwezekano Zaidi wa kuisababishia matatizo Tanzania kuliko zile zilizopita, na nini la kufanya kuiepushia nchi matatizo hayo?
Nitaanza na hili la pili (la nini la kufanya).
Kwanza kabisa, Mheshimiwa Rais na viongozi wakuu wakiri na kukubali moyoni na kwa siri kuwa uchaguzi huu haukuwa huru na wa haki. Nasema 'moyoni' kwa vile haitawezekana kukiri wazi wazi kwa vile hilo litawajibisha hatua za kisheria na pengine kuleta machafuko. Isipokuwa kukiri moyoni kuna umuhimu mkubwa sana.
Mara tu viongozi watakapokiri 'moyoni' hilo litaonekana wazi bila ya kusemwa, kwa jinsi watakavyogeuza mwenendo na silika zao. Na muhimu Zaidi, huenda wakakubali maoni haya, na maoni mengine ya wanaoitakia mema Tanzania. Pia watageuza lugha wanayozungumza kwa wapinzani. Kwa hili, rais aitishe kikao cha wakuu anaowaamini, si lazima wawe wengi, kama watano, wakae na kukubali hili. Nao kwa weledi mkubwa watafikisha ujumbe, kwa njia nyingine na kwa tafsiri na maneno mengine, kwa maafisa wengine waandamizi.
Hatua inayofuata, ni Rais na maafisa wakubwa (itapendeza zaidi wasuluhishi kutoka nchi jirani pia waalikwe) waitishe kikao na upinzani, upinzani wa kweli, siyo ule uliopangwa. Wazungumze kwa dhati kabisa juu ya waliyofikia. Wawaombe radhi na waahidi kurudisha mali na haki nyingine walizowanyang'anya kwa dhuluma. Itazamwe ikiwa itawezekana kuwashirikisha katika Serikali kwa sababu ya kuleta amani, la sivyo, wawaahidi kuwa kuanzia sasa watakuwa huru kabisa katika shughuli zao za upinzani.
Najua haya ni malipo madogo sana ukilinganisha na madhambi waliyotendewa (Mauaji, jela nk), lakini nina Imani sana na mioyo ya Watanzania ya kusamehe, na uzalendo wao . Ndiyo maana nimechagua kichwa hicho cha habari. La muhimu Zaidi hapa ni kuwaahidi kuwa yaliyotokea yamepita na tunafungua ukurasa mpya. Na hii ionekane kwa vitendo mara moja.
Huu tu ndiyo naona utatuzi wa matatizo makubwa yanayoanza kuinyemelea Tanzania, ndani na nje. Haya siyo maoni ya kitaalamu sana au ya usomi mkubwa! Kila mwenye akili na upeo wa historia ya hivi karibuni ya Afrika na dunia ataweza kung'amua haya. Nadhani rais wa sasa wa Zanzibar amekwishaliona hili!
Rais na wakuu wasijidanganye kwa kutegemea mno vyombo vya usalama, jeshi na polisi kuwa vina uwezo wa kupita kiasi kukabili lolote. Inatosha tu kutazama yaliyotokea kwenye nchi zilizokuwa zina upeo huo huo wa fikra: Iran, Ulaya Mashariki, Nchi kadhaa za Latin Amerika….ambazo zote zilikuwa na nguvu kubwa kuliko Tanzania. Ni suala la raia wengi kuamua tu. Na wanaposaidiwa na nchi nyingine, hili halichukui muda mrefu. Wala tusidanganye na kujidanganya kuwa dunia haijui ukweli.
Kwanini mara hii itakuwa tofauti?
Kwanza dunia imebadilika sana na haikubali tena uonevu wa Dhahiri kwa raia. Hii ni kwa sababu wameona madhara ya kufanya hivyo huko nyuma (mauaji, njaa, wakimbizi-ambayo yamewaathiri wao pia). Vyombo vya habari vimechangia sana kufanya hisia za walimwengu kuwa nyeti.
Pili: Tanzania siyo tena nchi maskini wa kutupwa kama zamani, kiasi ambacho chochote kinachotokea hakiwafanyi wengine wapoteze usingizi.
Tatu: mwamko wa Watanzania umezidi
Nne: Tundu Lissu na approach ya kuieleza dunia yanayoendelea Tanzania. Watu wengi, wakiwemo wakuu Tanzania, wanaliangalia hili kuwa litaathiri misaada tu, la hasha!
Nimeishi miaka mingi na katika miaka hiyo nimeona historia ikijirudia! Naitakia sana mema nchi yangu na sitaki iende kule kule zilikokwenda nchi nyingi nyingine za Afrika, baadhi yake zilikuwa na Amani zaidi na utajiri zaidi kuliko Tanzania: Liberia, Ivory Coast, Sudan, Zaire nk.
Wako watakaoona maoni haya ni upuuzi kwa vile Tanzania 'siyo' nchi hizo, Tanzania ni nchi imara, inayokuwa kwa kasi…… Kuna methali moja ya Kiarabu isemayo: Idhaa araada llahu halaaka namlatin am bata lahaa janaahayni' Mungu anapotaka kumwangamiza chunguchungu humpa mbawa mbili!'