Tanzania nchi ya maajabu: Mjue Mtanzania wa kwanza kucheza kombe la Dunia Urusi 2018

Tanzania nchi ya maajabu: Mjue Mtanzania wa kwanza kucheza kombe la Dunia Urusi 2018

Utanzania wake uko wapi hapo
Atakuwa na uraia wa nchi mbili labda.
Kwa Denmark hiyo inawezekana
Kali Ongala baba yake mtanzania mama yake MZUNGU mwingereza. alikuwa na uraia wa Tanzania na England alishindwa kucheza timu ya taifa kwa sababu sheria haikuruhusu uraia wa nchi mbili
 
Personal life
Poulsen is the son of a Tanzanian father and a Danish mother.[8] Poulsen's father had worked on a container ship, oscillating between Africa and Denmark, before he settled in Copenhagen.[2] His father died of cancer when Yussuf was only 6 years old. His father was a Muslim and that is where he got his name Yussuf from.Yussuf had visit Tanzania to his father's descent several times in 1996 and 2002 when he was so young and back again in 2008 and 2011. Yussuf was eligible to switch for Tanzania or Denmark during his career but he did not get any offer from Tanzania federation thus he choose to present Denmark on his career.[9][10]
 
Huwa namuona mara nyingi kajichora bendera ya Tanzania kumbe baba alikuwa wa huku
 
Mpira hatujui tumebaki kupepesa macho tupate wachezaji wa kuazima.vipi na yule wanaesema mpemba anaechezea england sijui dele ali au rashford.
 
View attachment 794596
Anaitwa Yussuf Yurary Poulsen mwana wa ardhi ya Tanzania na Denmark, ambaye ni mcheza soka maarufu nchini Denmark, aliyetajwa kuongoza kikosi cha timu ya Taifa ya Denmark ambako ndiko alikozaliwa na kuishi.

Yusuph alizaliwa Juni 15, 1994 huko Copenhagen nchini Denmark, huku baba yake akiwa ni Mtanzania mwenyeji wa Mkoa wa Tanga, anayeitwa Shihe Yurary aliyekuwa akifanya kazi kwenye meli ya mizigo, ambayo ilikuwa ikifanya shughuli zake kati ya Afrika na Denmark, na mama yake anayejulikana kwa jina la Lene ni raia wa Denmark.

Kupitia kazi zake hizo, Shihe alikutana na Lene na kuanzisha uhusiano uliomleta duniani Yusuf, na akaamua kuhamishia makazi yake jijini Copenhagen, Denmark ni raia wa Denmark.

Yusuf alianza kucheza soka akiwa mdogo, na kujiwekea rekodi mbali mbali mpaka kusajiliwa na timu ya RB Leipzig ya nchini Ujermani, ambako bado yupo mpaka sasa.

Kwenye timu yake ya Taifa ya Denmark Yusuf anacheza nafasi ya mshambuliaji, ambayo ni maalum kwa kufunga magoli, na imetajwa kushiriki kombe la dunia mwaka 2018, ambaloi linatarajia kuanza siku si nyingi nchini Urusi.
asee huyu jamaa kwenye jina la ukoo ningeona jina hata muhando, shemweta, shelukindo na ya kufanana na hayo ningeamini kweli baba yake alikuwa mwenyeji wa Tanga na ana asili ya Tanzania ila kwa jina Poulsen this is a big NO!!
 
hahahaaaaa huu undugu tumeutafuta mpk ukaja
baba yake nahisi ni shombe shombe sio Kwa jina hilo
 
bora nibaki hivi kutokuona maajabu yoyote hapo ya tz.thiago alcantara baba ake ni mbrazil ila yupo hispania.

Aliona mbali sana akaenda Hispania, kule brazil aliona anapoteza future yake..angeendelea kubaki angelikuwa kibaka
 
Aliona mbali sana akaenda Hispania, kule brazil aliona anapoteza future yake..angeendelea kubaki angelikuwa kibaka
kama kibaka Icardi anavyopoteza future yake.
 
Baba yake ni Mtanzania.. ila kazaliwa Denmark.
Tena ana uraia wa denmark.. Mbona baba yake ndio mtanzania.
 
View attachment 794596
Anaitwa Yussuf Yurary Poulsen mwana wa ardhi ya Tanzania na Denmark, ambaye ni mcheza soka maarufu nchini Denmark, aliyetajwa kuongoza kikosi cha timu ya Taifa ya Denmark ambako ndiko alikozaliwa na kuishi.

Yusuph alizaliwa Juni 15, 1994 huko Copenhagen nchini Denmark, huku baba yake akiwa ni Mtanzania mwenyeji wa Mkoa wa Tanga, anayeitwa Shihe Yurary aliyekuwa akifanya kazi kwenye meli ya mizigo, ambayo ilikuwa ikifanya shughuli zake kati ya Afrika na Denmark, na mama yake anayejulikana kwa jina la Lene ni raia wa Denmark.

Kupitia kazi zake hizo, Shihe alikutana na Lene na kuanzisha uhusiano uliomleta duniani Yusuf, na akaamua kuhamishia makazi yake jijini Copenhagen, Denmark ni raia wa Denmark.

Yusuf alianza kucheza soka akiwa mdogo, na kujiwekea rekodi mbali mbali mpaka kusajiliwa na timu ya RB Leipzig ya nchini Ujermani, ambako bado yupo mpaka sasa.

Kwenye timu yake ya Taifa ya Denmark Yusuf anacheza nafasi ya mshambuliaji, ambayo ni maalum kwa kufunga magoli, na imetajwa kushiriki kombe la dunia mwaka 2018, ambaloi linatarajia kuanza siku si nyingi nchini Urusi.
Yusuf SIO MTANZANIA
 
Back
Top Bottom