Tanzania nchi ya maajabu: Mjue Mtanzania wa kwanza kucheza kombe la Dunia Urusi 2018

Tanzania nchi ya maajabu: Mjue Mtanzania wa kwanza kucheza kombe la Dunia Urusi 2018

Shida kubwa sis tulio nayo wenye vipaji tunawapiga sana mawe yani wewe ona hata huyu Rais wetu pamoja na kujitoa kwake kote they wish hata kesho afe sijuwi nani katuloga ila Mungu atatutetea.
Na yeye ana kipaji gani?
 
Mafanikio ya awamu ya 5
Mambo ya serikali ya viwanda haya. Angeacha mpira uko aje apate kazi ya Jeshi kama yule kijana wa Nchi ya Mali yule spider man wa Ufaransa
 
Sasa mtu anacheza timu ya taifa ya Denmark ila bado unasema ni mtanzania wakati.mwenzio alishajilipua uraia.

Usikute hata bongo mavumbini hapajui
 
Mac tominey anaasiri ya England anachez Scotland sane anaaasiri ya ghana anacheza German RONALDO anaasili ya Brazil anacheza ureno pogba anaasiri ya Senegal lakini anacheza France sioni cha ajabu hapo na hiyo sio mtanzania pekee wanaokipiga ulaya wapo hata wakina ditti wapo huko Norway
 
Kijana anajitahidi sana ingawa kiufundi ni mkabaji zaidi ya mshambuliaji.

Yusuff ana uwezo wa kusimama au kukaa eneo la hatari la adui na akapoka mipira na kuanzisha mashambulizi upya.

Anacheza kama Roberto Firmino wa Liverpool ambae meneja wake Jurgen Klopp anapenda mtindo huo wa Firmino kusimama au kuzunguka kwenye eneo la adui.

Nilimwangalia pia kwenye mechi na Ireland kwenye mechi ya play-off ambapo Denmark walishinda goli 5-0, Yusuff aliisumbua sana ngome ya Ireland na pia kusababisha goli la pili la Denmark.

Tusubiri kuona makeke ya kijana Yusuff akiwa kwenye fainali za kombe la Dunia.
 
Unamuonaga wapi? Manzese au Mwananya kwenye Ndondo Cup
Mkuu angalia hata picha zake Google basi au mfuatilie kwenye klabu yake ya Rb Leipzig siamini kama umeishiwa namna hii siku ukiambiwa ya Rashford huku patakalika kweli
 
Huyo ni m denmark aliyezaliwa na baba mwenye asili ya Tanzania [emoji1241] na sio mtanzania, mleta uzi refer Civics yako ya form 2/3 aina za citizenship.
 
View attachment 794596
Anaitwa Yussuf Yurary Poulsen mwana wa ardhi ya Tanzania na Denmark, ambaye ni mcheza soka maarufu nchini Denmark, aliyetajwa kuongoza kikosi cha timu ya Taifa ya Denmark ambako ndiko alikozaliwa na kuishi.

Yusuph alizaliwa Juni 15, 1994 huko Copenhagen nchini Denmark, huku baba yake akiwa ni Mtanzania mwenyeji wa Mkoa wa Tanga, anayeitwa Shihe Yurary aliyekuwa akifanya kazi kwenye meli ya mizigo, ambayo ilikuwa ikifanya shughuli zake kati ya Afrika na Denmark, na mama yake anayejulikana kwa jina la Lene ni raia wa Denmark.

Kupitia kazi zake hizo, Shihe alikutana na Lene na kuanzisha uhusiano uliomleta duniani Yusuf, na akaamua kuhamishia makazi yake jijini Copenhagen, Denmark ni raia wa Denmark.

Yusuf alianza kucheza soka akiwa mdogo, na kujiwekea rekodi mbali mbali mpaka kusajiliwa na timu ya RB Leipzig ya nchini Ujermani, ambako bado yupo mpaka sasa.

Kwenye timu yake ya Taifa ya Denmark Yusuf anacheza nafasi ya mshambuliaji, ambayo ni maalum kwa kufunga magoli, na imetajwa kushiriki kombe la dunia mwaka 2018, ambaloi linatarajia kuanza siku si nyingi nchini Urusi.
yeah right....

sell me this and i will convince the entire planet that Obama is a Kenyan.
 
yeah right....

sell me this and i will convince the entire planet that Obama is a Kenyan.
Obama ni Mkenya halisi mengine hayo ni taratibu za kwenye makaratasi tu zinazomfanya kuwa Mmarekani
 
Huyo ni m denmark aliyezaliwa na baba mwenye asili ya Tanzania [emoji1241] na sio mtanzania, mleta uzi refer Civics yako ya form 2/3 aina za citizenship.
Sijasoma Civics mimi sisi tulikuwa na soma linaitwa Siasa.......Huyo ni Mtanzania halisi udenimark wake ni kwenye taratibu za kwenye makaratasi
 
Sasa mtu anacheza timu ya taifa ya Denmark ila bado unasema ni mtanzania wakati.mwenzio alishajilipua uraia.

Usikute hata bongo mavumbini hapajui
Amefika Tanga kwa baba yake zaidi ya mara 6
 
Tanzania kwa ubishi hatujambo wew Leo hata uchukue uraia wa wa wapi lakin utabakia kuwa mtz tu na katika histry yako itabaki hvyo tu
 
Tanzania kwa ubishi hatujambo wew Leo hata uchukue uraia wa wa wapi lakin utabakia kuwa mtz tu na katika histry yako itabaki hvyo tu
Tuko pamoja sana.....wasiojua na wajue hilo.....Obama mwezi ujao anakwenda kijijini kwa baba yake Kogelo Kenya
 
Back
Top Bottom