Tanzania ndio nchi ambayo wajinga wamepata fursa ya kuongoza werevu kwa kuwa wana 'connection'

Tanzania ndio nchi ambayo wajinga wamepata fursa ya kuongoza werevu kwa kuwa wana 'connection'

Ukweli utatuweka huru na kutuvusha, ukibisha na ubishe, hukatazwi.

Kiuhalisia hii nchi ina mfumo mbovu na umeoza wa kupata vyeo na madaraka, yaani inakera. Huhitaji hata degree wala PhD ili ujue ili mradi uwe na connection inatosha.

Hivi umejiuliza ili uwe Mkuu wa Wilaya au Mkoa inapaswa uwe na vigezo gani? Inasikitisha sana wajuzi wa kulivusha taifa wako mtaani halafu wajinga wako madarakani.
Tanzania HAKUNA meritocracy.

Ni mwendo wa connection, nepotism na chawacracy
 
Ukweli utatuweka huru na kutuvusha, ukibisha na ubishe, hukatazwi.

Kiuhalisia hii nchi ina mfumo mbovu na umeoza wa kupata vyeo na madaraka, yaani inakera. Huhitaji hata degree wala PhD ili ujue ili mradi uwe na connection inatosha.

Hivi umejiuliza ili uwe Mkuu wa Wilaya au Mkoa inapaswa uwe na vigezo gani? Inasikitisha sana wajuzi wa kulivusha taifa wako mtaani halafu wajinga wako madarakani.
NAPE NAUYE
 
nchi zote duniani teuzi za kisiasa zinaangalia kwanza loyalty kabla ya kitu kingine
Achana na teuzi za kisiasa. Tanzania mpaka Mkurugenzi wa soko la Kariakoo na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Ndio maana hakuna shirika la umma linalotengeneza faida nchi hii.

Usitegemee MIUJIZA ya maendeleo katika mfumo Kama huo.
 
Njaa haina baunsa unabidi ujifanye chawa ili upate ugali wa familia
 
Degree au Phd hazina maana hapa Tz kwanza Wasomi wenyewe kichwani hamna kitu Mimi naona Tz tatizo la watu kuwa na IQ ndogo ni la watu wengi.
 
Pia hata hali ya kulalamikalalamika nako ni ugonjwa wa akili. Hapa duniani hakutakuja kuwepo system kamilifu, system kamilifu ipo Mbinguni kwenye Ufalme wa Mungu Baba.

Pia hiyo ya werevu kutawaliwa na wadhaifu hiyo kitu inaitwa "Neema". Neema maana yake ni wasiostahili wamestahilishwa na wenye majivuno ya sifa zao kutupiliwa nje huko.
 
Angalieni kwanza wananchi je kichwani wapo vizuri tatizo la ujinga kwa hapa Tz ni kubwa Sana , hao viongozi ni zao la jamii zetu huwezi kuwa smart wakati unaowaongoza hawapo smart.
Wananchi wenye akili wako wengi tu, kinachotakiwa ni kufuta kipengele cha polisi ku attack raia kama defense mechanism. Hapo ndio utaona kwamba mabadiliko kumbe yanawezekana.

Hii ndio iko kwenye nchi zote zenye demokrasia inayojielewa. Hata hapo Kenya tu polisi haruhusiwi kupiga raia ila huku kwetu ni kinyume.

Tuondoe hali ya serikali kuwa mtawala wa wananchi na badala yake iwe meneja. Kisha utaona kama kutakuwa na Waziri aina ya Nape, Makamba au Bashe.
 
Back
Top Bottom