Tanzania ndio nchi ambayo wajinga wamepata fursa ya kuongoza werevu kwa kuwa wana 'connection'

Tanzania HAKUNA meritocracy.

Ni mwendo wa connection, nepotism na chawacracy
 
NAPE NAUYE
 
nchi zote duniani teuzi za kisiasa zinaangalia kwanza loyalty kabla ya kitu kingine
Achana na teuzi za kisiasa. Tanzania mpaka Mkurugenzi wa soko la Kariakoo na Wakurugenzi wa Halmashauri.


Ndio maana hakuna shirika la umma linalotengeneza faida nchi hii.


Usitegemee MIUJIZA ya maendeleo katika mfumo Kama huo.
 
Njaa haina baunsa unabidi ujifanye chawa ili upate ugali wa familia
 
Degree au Phd hazina maana hapa Tz kwanza Wasomi wenyewe kichwani hamna kitu Mimi naona Tz tatizo la watu kuwa na IQ ndogo ni la watu wengi.
 
Pia hata hali ya kulalamikalalamika nako ni ugonjwa wa akili. Hapa duniani hakutakuja kuwepo system kamilifu, system kamilifu ipo Mbinguni kwenye Ufalme wa Mungu Baba.

Pia hiyo ya werevu kutawaliwa na wadhaifu hiyo kitu inaitwa "Neema". Neema maana yake ni wasiostahili wamestahilishwa na wenye majivuno ya sifa zao kutupiliwa nje huko.
 
Angalieni kwanza wananchi je kichwani wapo vizuri tatizo la ujinga kwa hapa Tz ni kubwa Sana , hao viongozi ni zao la jamii zetu huwezi kuwa smart wakati unaowaongoza hawapo smart.
Wananchi wenye akili wako wengi tu, kinachotakiwa ni kufuta kipengele cha polisi ku attack raia kama defense mechanism. Hapo ndio utaona kwamba mabadiliko kumbe yanawezekana.

Hii ndio iko kwenye nchi zote zenye demokrasia inayojielewa. Hata hapo Kenya tu polisi haruhusiwi kupiga raia ila huku kwetu ni kinyume.

Tuondoe hali ya serikali kuwa mtawala wa wananchi na badala yake iwe meneja. Kisha utaona kama kutakuwa na Waziri aina ya Nape, Makamba au Bashe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…