Mijini na vijijini manung'uniko yametawala!
Watumishi wa umma wanaonekana wana furaha lakini mioyoni wanaugulia maumivu!
Hata tabasamu za wengine zinaweza zikawa na tafsiri tofauti. Labda ni kilio kilichopunguzwa makali!
Watu wanalia lakini hawataki ijulikane kuwa wana majonzi!
Ndivyo kisiwa cha amani kunavyopaswa kuwa?
Mbona kama Kenya ambayo si Kisiwa cha amani wanafaidi zaidi keki ya Taifa lao kuzidi wananchi wa Kisiwa cha amani?
Ni kisiwa cha amani au makao ya waoga?
Tz sio kisiwa cha amani, na watz sio waoga , kama waoga mbona babu zetu wamepambana na mkoloni kufa na kupona , mfano wakina kinjekitile ,mkwawa n.k ,ni swala la mda tu.
Hatuwezi ogopa machawa hata enzi za ukoloni walikuepo mababu zetu waliopigania haki ila nyuma ya pazia walikuepo machawa walliotumiwa na wakoloni ,kwa kamatisha wananchi wenzao ili kufanikisha biashara ya utumwa kwa wazawa wenzao huku wakilamba miguu na viatu vya wakoloni, so huchawa haujaanza leo ulikuepo na sasa historia inajirudia ,( hakuna jipya chini ya jua wakuu?
Tutafika mda ni mwalim mzuri.
Mwaka mmoja hivi nikiwa Tanga nilikutana na mzee mmoja hivi toka Kigoma enzi za manamba katika mashamba ya Mkonge ,huyu ndo enzi zile alikua agent wa kwenda huko na kuwachukua watu kwa ajili ya kulima mashambani huko Tanga (kwa sasa marehem na alikufa kifo kibaya uyu mzee ,mwili ulioza huku bado anaongea mpaka wazee walipofanya yao)
Hii sio story niliona na nilikua naongea nae kabla ya umauti) .
Yeye ndo alikua agent wa kutafuta manamber ambao walipo fika walikaa kwenye vijumba vya mita 3x4 watu watano , na vipo baadhi mliowahi fika Tanga Ngomeni - umba kama unaenda Kumburu , vipo baadhi vingine vimebomoka , ( unaweza tembelea maeneo ayo) kama upo Tanga au kwenda tembea Tanga ) .
Hawa manamba akiwemo uyu mzee japo alikua boss hakuna alieachwa salama namanisha wengi hawakuweza kuzaa watoto, na ndo maana pamoja na kituo cha wakoma Misufin sijui kama bado kipo, kilihudumia wakoma plus hawa manamba ambao walikua wazee wakiishi apo Ngomeni- umba - kumburu.
Huyu mzee pamoja na majukum yake ila pia alikua ndo mbobezi wa kuratibu na kiongozi wa ngoma za hiari alisema, namanisha ngoma kama za mizim au mazingaombwe, kwamba mtu anaingia aridhini akiwaka moto anatokea upande wa pili akiwaka moto.
Ujira wao mkubwa ikuwa chinjiwa ng'ombe kula nyama na pombe ya kienyeji ,thats waliochukuliwa kama manamba maisha yao yanaishia huko walikopelekwa basi hapakua cha ziada.
Mnaweza ona machawa hayajaanza leo ,yalikuepo na sasa inajirudia.
Funzo
Chawa anaweza kufa kifo kibaya sana na cha mateso kwa laana kuu ambayo ametumia kwa kulamba miguu ya maboss wake ili kuumiza wengine au kuumiza nchi, ndo maana nikaweka mfano hai kupiti huyu mzee aliejulikana kama mzee Mabom na aliishi Umba Ngomeni Tanga.
UCHAWA NI DHAMBI KUU .