Hujasikia madudu yanayoibuliwa na Waziri Slaa na RC Makonda kwenye masuala ya ardhi? Wamedhulumiwa mpaka wasomi na watu waliowahi kuwa viongozi, maadam tu madhulumati yana hela! Nchi ya amani inaweza kuwa na "upumbavu" kama huo, kiasi cha hukumu ya mahakama kutokuheshimiwa?
Nchi ya amani inazuia watu kutoa maoni yao? Nini kilimpata Ndugai alipolalamika deni la Taifa kuongezeka?
Nchi ya amani inatumia vibaya fedha za wananchi kwa chaguzi zisizo na umuhimu? Kumbuka jinsi wabunge wa upinzani "walafi" walivyorubuniwa kuvihama vyama vyao na kupelekea chaguzi zisizo na tija