kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Tumepata shida hii tena, lakini bila shaka maisha ya watanzania ni lazima yaendelee pamoja na kuwapoteza wapendwa wetu. Tusilie sana kama vile watu tusiokuwa na matumaini. Tuchanganye yale yote mazuri waliyotuachia Marais wetu Nyerere, Mkapa na sasa Dr. Magufuli kama mtaji katika kuijenga Tanzania iliyo bora zaidi kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiteknolojia kuliko ile waliyoicha. Na watu wa kuyatimiza hayo wapo, tuwape support tu.
Kiongozi bora kwetu ni yule atakaefanya yafuatayo:
1. Kuwaunganisha Watanzania wote bila kujali tofauti zao mbalimbali
2. Kumtanguliza na aonekane akimtanguliza Mwenyezi Mungu katika matendo yake.
3. Ajue kuwa siasa za siku hizi ni uchumi, elimu bora, afya bora na usalama wa watu na mali zao.
4. Ajue kuwa vibaraka wa ndani na nje wapo, ukoloni bado upo.
5, Ajue kuwa hakuna msaada wa maana utakaotujengea taifa letu, kujitegemea ndio njia sahihi. Hakuna cha bure duniani.
6. Ajue kuwa ushirikiano mzuri na mataifa mengine ni chanzo bora cha masoko na usalama kwetu
7. Ajue kuwa wala rushwa, wakwepa kodi na mafisadi walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo, iwe ni agenda yake ya kudumu kuwakabili.
Poleni Watanzania wenzangu, hata aje nani bila kufanyakazi kwa kupindukia maisha yako yatabaki vilevile na yaleyale.