Tanzania ni moja ya nchi zaidi ya 50 zilizo kwenye orodha iitwayo "RED LIST". Serikali inafanya jitihada zipi kujitoa humo?

Sasa kama kuna nchi wanaolala na kuamka na kupanga orodha huyu awe red list na huyu awe green list sisi tutawasaidia nini watu hao? Cha kushangaza nchi hizo zenyewe zinajiweka kwenye green list kwa kila kitu yaani. Kiuchumi wao wanajiweka daraja la kwanza na sisi wengine wanatuweka daraja la tatu. Kijamii wao wanajiita nchi zenye furaha duniani wakati sisi wanatuweka nchi zisizo na furaha duniani. Kwenye life span wao wanajiita wanaishi milele na sisi tunakufa mapema. Na kwenye covid wao wameamua kujiita green na sisi wengine red.

Who cares?

La muhimu life halijali red wala green. Utajipangia green lakink covid-19 haijui kusoma rangi. Wanaojiita ni green wanakufa kama kumbikumbi na sisi tunaoitwa red tupo tunadunda.

Kama hustuki kuwa hii ni vita ya kisaikolojia ili kuzidi kudunisha utu wa watu wasio rangi yao ili wawatawale vizuri basi endelea kujihisi upo kwenye red list. Humu duniani hakuna atakayekuthamini, jithamini kwanza ebo!
 
X elfu 3 na ushee. Inasikitisha sana unatest unalipa . Typically business
 
Ndugu, jambo la msingi kuelewa ni kwamba dunia ya sasa imekuwa kama kijiji.

Watu wanasafiri na kufanya biashara na mambo mengine,

Kenya kwa mfano haimo kwenye "RED LIST" kwanini?

Hiyo ni kwa sababu Nairobi ni international Hub ambapo yapo mashirika mbalimbali ya kimataifa na yana ofisi zao pale.

Hivyo ni lazima Kenya ifuate hizi taratibu zao kwamba viwango viwe katika standards tunazozitaka.

Kwahiyo lazima Kenya iwe na up to- date data za Covid ambazo zimekusanywa na dedicated and trusted people.

Sasa huo ni mfano wa Kenya tu lakini zipo nchi zingine kama Sierra Leone walikuwa katika orodha ya njano yaani amber List.

Lakini mwezi June watatoa taarifa huko Geneva kwamba ndani ya wiki nne watu zaidi ya 1000 walikuwa wameambukizwa.

Hivyo hilo ni tatizo na Jumatatu ilopita nchi hiyo imewekwa kwenye Red List.

Hivyo utaona jinsi mifumo ya sasa ya kidunia inavyoweza kuziendesha nchi kama zetu kwa namna fulani hivi.
 
Very True! shadow governments exist, they pull the strings of almost everyone; from the most revered rulers to their most fiercest opposition figures... We need a complete civilian overhaul of the system.


Fruitful exchange mkuu! I categorize you as the intelligentsia humu ndani👍😃
 
I'm humbled.

🤝
 
Chanjo kama imefika ianze kutolewa haraka kuokoa wananchi......
Kachome wewe, mbona mnakuwa na akili za kijinga hivyo? Wewe unaetaka kujikinga nenda kachome, jamanii, na mgharamie wenyewe hiyo michanjo, sio mchote tena kwenye tozo yetu ya kizalendo
 
Mkuu, wanipa kazi ya udalali tena?

😇
Ni udalali tu mnafanya , hata huyo war criminal Tony Blair, ni dalali tu, nobody gives a f* ck about African lives, mfe, msife mtajua nyinyi, wao wanaangalia tu watapata nini kwa kuleta hizo chanjo, ni pesa tu inatafutwa
 
Kachome wewe, mbona mnakuwa na akili za kijinga hivyo? Wewe unaetaka kujikinga nenda kachome, jamanii, na mgharamie wenyewe hiyo michanjo, sio mchote tena kwenye tozo yetu ya kizalendo

Wapi nikachome? Washaanza kuchanja wananchi? Nimepata taarifa kwamba zishafika.
 
Nchi yenye zaidi ya watu milioni 50, wanataka wawe wanafanya vipimo maabara ya Taifa tu. Hiyo akili au matope.
 
Ni udalali tu mnafanya , hata huyo war criminal Tony Blair, ni dalali tu, nobody gives a f* ck about African lives, mfe, msife mtajua nyinyi, wao wanaangalia tu watapata nini kwa kuleta hizo chanjo, ni pesa tu inatafutwa

Mimi si dalali, nina familia moja Tanzania, na mbili katika nchi tofauti za Ulaya na nazunguka, hivyo sina ujanja ni lazima chanjo niipate.

Cha msingi ni kuangalia ni chanjo ipi watanzania watapatiwa kwa wale ambao itawabidi kupata chanjo.

Lakini suala hili ndugu Tanzania haiwezi kulikwepa.

Tutazunguruka huku na huko lakini mwisho wa siku utasikia watu wanapigwa chanjo.

Ila bado watanzania wana uamuzi wa kuchoma chanjo au kutochoma, hakuna apigae udalali hapa.

Ni maoni tu ya msingi yanayotokana na kusoma kinachoendelea.
 
Hiyo mifumo ya dunia ipo, na inajulikana kuwa ipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya western powers. Hebu jaribu kushirikisha bongo yako: hapa bongo kuna wazungu wana mahoteli yao kule mbugani Serengeti na Ngorongoro, na wana migodi yao huko Geita na Kahama. Ulishawahi kuona wanaacha kuingia na kutoka nchini kisa Tanzania ipo kwenye redlist ya corona au kwa sababu haitangazi namba za victims wa corona? Au Blair kilichomleta nchini ni nini kama nchi ipo kwenye redlist?

The thing is hayo maredlist wanakuwekea wewe ili kuonyesha white supremacy yao dhidi yako wewe ili uyeyuke ufanye kila wanachokwambia ufanye.

Ukijiongeza ukatambua janja yao na ukajiongeza ukajikomboa kifikra na ukajitegemea kiuchumi mtakaa meza moja na kuheshimiana kama equals. Umeona China inawekwa redlist pamoja na vijimambo vyao kibao?
 
Jifungie ndani hadi watakapotangaza ili ujikinge na kifo, usife daima

Mkuu jadili hoja kimantiki na si ki james delicious! Kwani chanjo za korona zinazuia kifo? Wazazi wako wangekuwa na akili kama zako wasingekuchanga vaccine za pepopunda,surua,ndui etc tusingekuwa tunaona utopolo wako leo.
 
Nchi yenye zaidi ya watu milioni 50, wanataka wawe wanafanya vipimo maabara ya Taifa tu. Hiyo akili au matope.
Tukisema suala la ajira eneo la sekta ya afya si lazima mtu awe daktari ndo aajiriwe.

Kunakuwepo na shughuli nyingine nyingi tu ambazo zinaisaida sekta ya afya.

Kila mkoa watakiwa kuwa na maabara, taasisi ya utafiti, na mambo mengine.

Kupitia njia hiyo ajira inakuwa "sorted accordingly".
 
China na Russia wao tayari wana dawa zao za chanjo na wananchi wao tayari wamedungwa sindano siku nyingi tu.

Sisi Tanzania ni kujiona tunafahamu kila kitu tuna dawa yoyote in the pipeline kujaribu kupambana na Covid?

The thing is real wake up!
 
Nchi yenye zaidi ya watu milioni 50, wanataka wawe wanafanya vipimo maabara ya Taifa tu. Hiyo akili au matope.
Hii nchi haikuwa na testing capacity to begin with hata kabla ya corona. Kimsingi vifaa vinavyotumika kupima corona, PCR na reagents zake, ni vifaa vinavyotumika kwa ajili ya research mbali mbali nje ya kudiagnose corona. Nchi hii ilineglect biotechnological research kwa muda mrefu sana kwa hiyo kuitegemea eti ijenge maabara za kisasa kufanya mambo kama hayo ndani ya kipindi cha corona ingekuwa maajabu.

Mimi nilishawahi kuandika huko nyuma kwamba serikali ijifunze kupitia hii corona kuwekeza kwenye science na research za kisasa. Kujenga majengo na kuweka mabench eti hiyo ndio science lab ni utoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…