Tanzania ni Mwanachama Hai Mahakama Haki za Binadamu Afrika

Amosi Mgonja

Member
Joined
May 15, 2021
Posts
5
Reaction score
5
TANZANIA NI MWANACHAMA HAI WA MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU AFRIKA

The Diplomat

Kumekua na mitazamo hasi inayokosoa kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula aliyoizungumza jana Mei 25, 2021 Siku ya Afrika Duniani kwa kusema "Tanzania ni mwana chama hai wa Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika"

Kutokana na kauli hii wanaharakati wengi hasa wale wasiojua kufuatilia mambo kwa undani, wameamua kupotosha ukweli kwa kusambaza uongo wakiamini Watanzania sio wafuatiliaji wa mambo, jambo ambalo si sahihi, ukweli lazima uzungumzwe.

Kwenye mijadala yao wamepindisha ukweli na kumkosoa Waziri Liberata Mulamula kwa kusema Tanzania ilishajitoa kwenye mahakama hio mwaka 2019 kipindi Prof. Palamagamba Kabudi akiwa Waziri wa Mambo nje jambo ambalo ni la uongo na halina ukweli wowote.

Wanasambaza barua zilizoandikwa 2019 ambazo ukisoma kwa undani ni kwamba Tanzania iliadhimia kuondoa kipengele kimoja tu cha ITIFAKI kwenye mahakama hio. Sababu za Uamuzi huo hazisemwi na badala yake upotoshaji wa makusudi umeendelea kufanyika.

Tanzania iliamua Kuondoa kipengele hicho cha ITIFAKI kinachoruhusu wananchi binafsi (Individuals) na mashirika yasiyo ya kiserikali (Private Sectors) kuishtaki Tanzania katika mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, hatua hiyo ilifikiwa baada ya kuchambua na kujiridhisha kuwa kipengele hicho kinaingiliana na kukinzana au kupingana na sheria za ndani za Tanzania.

Pia Wananchi tuelewe kuwa Tanzania kamwe haiwezi kujitoa kwenye mahakama hii kwani sisi ni miongoni mwa waazilishi wa Mahakama ya haki za binadamu Afrika na makao yake makuu yapo Nchini kwetu, Jijini Arusha Tanzania.

Tuepuke upotoshaji unaoletwa na kusambazwa na Watu wasio na nia njema kwa Taifa letu. Watu hawa ni maadui wa Maendeleo ya Taifa letu, nasi hatutosita wala kuchoka kuwapasha ukweli hadi nyongo ziwapande.

Ukweli Ni kwamba Tanzania ni mwanachama hai wa Mahakama hiyo na haijawahi kufikiria wala kuwa na Mpango wa kujitoa kwani haki za Binadamu ni Miongoni mwa vipaumbele Muhimu kwenye Nchi yetu, kilicho ondolewa ni kipengele cha Kiitifaki ili kulinda Maslahi na sheria za Taifa letu.

The Diplomat
 
Sasa kama individual au Private sector haiwez ishtaki Tanzania kwenye mahakama hiyo, hizo haki za binadam ni za nyangumi.
Acheni blabla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…