Tanzania ni nchi huru hatupaswi kuingiliwa mambo yetu

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Kauli hi imechukua kasi Sana. Tanzania ni nchi huru haipaswi kuingiliwa katika mambo yake hasa demokrasia.

Kauli hi imekua I kitumiwa sana na baadhi ya wanna CCM na Lumumba B7.

Nashangaa kuwa CCM hii ni tofauti na CCM ya akina Nyerere? Maana akina Nyerere walikua mstari wa mbele kuwatetea watu waliokua wakikandamizwa katika nchi zao, je akina Nyerere kumbe walikua wakiingilia Uhuru wa nchi nyingine zisijifanyie zitakavyo kwa Raia wao.

Nyerere alisaidia
Afrika Kusini
Msumbiji
Namibia
Zimbabwe
Sahara Magharibi

Alihifadhi wakimbizi waliomkimbia Mobutu. Alikua akimkaribisha Yeser Arafat n .k

Kwa hiyo Nyerere na wenzake walikua wanakosea?

Je, ni halali mkuu we nchi moja kuwatesa atakavyo baadhi ya Raia na Dunia ibaki inatazama tu?
 
Wanapoomba misaada mbona huo uhuru huwa hawajitapi nao? Kama wewe ni nchi huru jitegemee kwa kila kitu, ndio utaweza kuulinda huo uhuru!! Mbona wanapoingilia kukupa misaada, huikatai, ila wakikukosoa hasa kuhusu Demokrasia, na utawala bora, ndio unaanza kusema hayo maneno ya shombo!!!? Kwa kuwaaminisha watu,.
 
Nyerere alikuwa anapigania waafrika waliokuwa wanatawaliwa na minority (weupe).

Watu wametoka zao makwao wanakuja kwako kisha wanakuchagulia namna ya kuishi na wao wanvyotaka tuishi.

Kwasasa sisi ni nchi huru na waliopo madarakani tumewaweka sisi. Utasema waliiba kura. Ubaya hakuna wa kuthibitisha.

Yanayojulikana serikali iliyopo madarakani imepigiwa kura.
 
Inategemea kipindi cha kina Nyerere inchi nyingi zilikuwa zinadai uhuru,
Kwasasa mataifa yote yapo huru isipokuwa Parestina.
 
Nyerere alikuwa anapigania waafrika waliokuwa wanatawaliwa na minority (weupe).

Watu wametoka zao makwao wanakuja kwako kisha wanakuchagulia namna ya kuishi na wao wanvyotaka tuishi.

Kwasasa sisi ni nchi huru na waliopo madarakani tumewaweka sisi. Utasema waliiba kura. Ubaya hakuna wa kuthibitisha.

Yanayojulikana serikali iliyopo madarakani imepigiwa kura.
Serikali nyingi za kiafrika ,wananchi kupiga kura ni kiinimacho.

Hivi wewe ukiwa unampa kichapo na unamfanyia ushenzi mke wako ndani ya nyumba yako watu watakuacha tu kwa vile ni mkeo na nyumba ni yako?
 
👊🏽👊🏽👊🏽👍🏽

Wakati sisi tulikua mtari wa mbele kuwaingilia Uganda kwenye mambo yao ya ndani wakati wa Amini.
 
Kauli hi imechukua kasi Sana. Tanzania ni nchi huru haipaswi kuingiliwa katika mambo yake hasa demokrasia.

Kauli hi imekua I kitumiwa sana na baadhi ya wanna CCM na Lumumba B7.

Nashangaa kuwa CCM hii ni tofauti na CCM ya akina Nyerere? Maana akina Nyerere walikua mstari wa mbele kuwatetea watu waliokua wakikandamizwa katika nchi zao, je akina Nyerere kumbe walikua wakiingilia Uhuru wa nchi nyingine zisijifanyie zitakavyo kwa Raia wao.

Nyerere alisaidia
Afrika Kusini
Msumbiji
Namibia
Zimbabwe
Sahara Magharibi

Alihifadhi wakimbizi waliomkimbia Mobutu. Alikua akimkaribisha Yeser Arafat n .k

Kwa hiyo Nyerere na wenzake walikua wanakosea?

Je, ni halali mkuu we nchi moja kuwatesa atakavyo baadhi ya Raia na Dunia ibaki inatazama tu?
Wewe umetekwa na kunyanyaswa wapi?
 
Serikali ya sasa hovyo kabisa ni hatari kwa raia.
 
UNAFIKIRI UNAINGILIWA? AU UNAKUMBUSHWA KUSIMAMIA SHERIA NA KATIBA?
 
Nyerere alikuwa anapigania waafrika waliokuwa wanatawaliwa na minority (weupe).

Watu wametoka zao makwao wanakuja kwako kisha wanakuchagulia namna ya kuishi na wao wanvyotaka tuishi.

Kwasasa sisi ni nchi huru na waliopo madarakani tumewaweka sisi. Utasema waliiba kura. Ubaya hakuna wa kuthibitisha.

Yanayojulikana serikali iliyopo madarakani imepigiwa kura.
Jecha vipi?
 
Ukioewa misaada unanengua. Ukiulizwa kuhusu democrasia,uhuru na haki Oho.nchi huru una uhuru Gani wewe hata chanjo za watoto unapewa misaada na hao unaowaita MABEBERU
 
Serikali nyingi za kiafrika ,wananchi kupiga kura ni kiinimacho.

Hivi wewe ukiwa unampa kichapo na unamfanyia ushenzi mke wako ndani ya nyumba yako watu watakuacha tu kwa vile ni mkeo na nyumba ni yako?
Kwanza unakosea kusema serikali nyingi za Africa...serikali nyingi tu Duniani. Sio Afrika tu.

Tatizo tumewaachia watu wengine watuamulie aina ya maisha tunayotakiwa kuishi.

Ndiyo maana kwako unaona ni sahihi....hizo nchi zinazoungilia mambo yetu zina matatizo lukuki usidhani hawana.

State kutwa kupigana risasi.
 
Ni mtu mpumba.vu pekee anayeweza kuamini kuwa watawala wanaweza kuwafanyia uovu watu wao kwa namna yoyote watakayo bila ya kuhojiwa na jamii ya kimataifa.

Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka. Baba huwezi ukawa unaua watoto wako, unawakata vidole wanao, halafu majirani wakikuuliza ukajitetea kuwa, mimi ni familia huru, nina uamuzi wa kufanya chochote ndani ya nyumba na familia yangu! Utaonekana mwendawazimu.

Hakuna uhuru usio na mipaka. Lazima ujue, juu ya familia kuna jamii yako na serikali, juu ya serikali kuna umma wa Taifa/Jamhuri, na juu ya Jamhuri, kuna jamii ya kimataifa na taasisi zake. Na juu ya mwanadamu yeyote, kwa wenye imani, kuna MUNGU. MUNGU ndiyo mamlaka ya mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere alikuwa anapigania waafrika waliokuwa wanatawaliwa na minority (weupe).

Watu wametoka zao makwao wanakuja kwako kisha wanakuchagulia namna ya kuishi na wao wanvyotaka tuishi.

Kwasasa sisi ni nchi huru na waliopo madarakani tumewaweka sisi. Utasema waliiba kura. Ubaya hakuna wa kuthibitisha.

Yanayojulikana serikali iliyopo madarakani imepigiwa kura.
Na yanayojulikana pia ni kuwa wananchi wa Zanzibar hawakumchagua Dr Shein. Hakuna uovu usiojulikana hata kama uthibitisho usipopatikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom