Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995?

joka kuu naomba utzame facts zako upya

kighoma malima alichukua fomu za uraisi pia.....
hata kama hakufika mbali.but alichukua fomu
Soma taratibu hapo chini...

 
The Boss,

..Kighoma Malima stood no chance ya kupewa nafasi na CCM.

..Mabalozi walikuwa wanashinikiza afukuzwe kazi baada ya kuonekana serikali haikusanyi kodi.

mkuu hebu jaribu kuelewa kwanza
hatuzungumzii walio kuwa na nafasi ya kupewa
tunazungumzia waliochukua fomu
hata kama hakuwa na nafasi
alichukua fomu,hilo ndo tunataka lizungumzwe
 
Mkuu JokaKuu, asante sana kwa historia hiyo.

Ina maana mkuu JK was not "In it to win it"? Yani alijiunga na kampeni kwa nia ya kumsindikiza Lowassa? Au ilikua kama 2005 walipo ahidiana mmoja atakua raisi na mwingine prime minister.
 

The Boss,
Sidhani Mwalimu Nyerere aliangalia ugombeaji wa kiti cha rais katika misingi ya kidini kama unavyotaka kutuaminisha. CCM ingeweza kusimamisha Waislamu wote na kwa Mwalimu lisingekuwa tatizo. Kadhalika CCM ingeweza kusimamisha Wakristo na wapagani wote na hilo kwa Mwalimu lisingekuwa tatizo. Sidhani alikuwa na mtazamo wa kuangalia kuna Waislamu wangapi wanaogombea na kuna Wakristo wangapi. Hii inadhihirishwa na kauli zake mwenyewe, kama alivyotaja Mkandara somewhere in this thread.
 
Nina kubaliana na The Boss uzushi dhidi ya Salim ulikuwa 2005

Kabla ya uchaguzi 2005 mtandao waliakikisha wanamchafulia mtu yoyote ambaye anaoneka ni tishio kwa Kikwete.Mtikila alitumika kumchafua Sumaye,Magazeti na uzee wa Malecela na Salim kuhusishwa na kifo cha Karume.

1995 magazeti yaliandika mara kwa mara SAS ndio chaguo la Nyerere lakini akaendelea kukaa kimya na bila hata kuonyesha nia.Ndipo Nyerere alipojitokeza hadharani ilikumshinikiza SAS ambaye baadae akaweka wazi hata gombea kwasababu anataka kuendelea na majukumu yake ya OAU.Alipoamua kugombea 2005 Mkapa hakakataa kumuunga mkono SAS na kama sijakosea ndipo mgogoro kati ya taasisi ya Mwl Nyerere na Mkapa ulipoanzia.

 

jokaKuu,
Hapa ningekuwa mwalimu wako darasani ningekupa 100% tena na plus juu yake.
 


jasusi naona hatukuelewana
ninachoongea mimi ndio hiko hiko unachozungumza wewe

but kuna vitu vingine ni maoni yangu na sio facts kutoka kwa nyerere

mwaka 1995 facts ni kuwa kabla ya kikwete kuchukua fomu,
muislam aliechukua fomu alikuwa kighoma malima peke yake
so hawakutaka chama kionekane kinawabagua waislam
unaweza kupinga udini kwa maamuzi ambayo mwingine anaweza ona ndo udini wenyewe
sisemi nyerere alimwambia kikwete achukue fomu kwa kuwa ni muislam...
 
Hapo nimekupata, mkuu.
 
Hii ya ndege Kikwete na Lowassa walitumia kama njia ya kujingea jina lakini it turned out to be disaster kwa Lowassa.Magazeti ya kaanza kuuliza pesa wamepata wapi,kumbuka 1995 kupanda ndege ya kukodisha ilikuwa ni jambo kubwa.utetezi wa Lowassa ulikuwa ni wamefadhiliwa, ikawa ni last nail to his coffin kwamba wafadhili ndio wanakupeleka ikulu ukifika huko watakuja kudai fadhila zao.
 
Kwa mimi ambae nilikwa kijana mdogo na kwa kufuatilia masimulizi hiyo story ambayo leo ingeniongezea elimu [knowledge] ya mchakato mzima kidogo nimemwelewa Joka Kuu ameonekana kiasi kikubwa kugusa kile nilichokuwa nasikia miaka hiyo.

Na ambalo siwaelewi wengi wenu na kwa kiwango kikubwa naona amjalizingatia ni issue ya Lowasa na Kikwete.
Logical Kikwete katika swala la urais wa 1995 alikuwa ni zaidi ya Lowasa japo wengi wanaona Kikwete ndiye ndiye aliyekuwa Msindikizaji.Kama kuna mambo ya kiutu uzima mmoja alikuwa ndio kusudio na Lowasa alikuwa boya na mapesa yake huku mwezie akijua anafanya nini?

Ukizangatia wengine mmesema Mwalimu alimwambia Kikwete akachukue Form,ni kwanini akamwambie kuchukua form za kugombea urais na aliposhindwa Mwalimu inasemekana alimwambia bado ajakua, kuna mdau kasema unexperienced. Ukizungumzia hoja ya kidini haitakuwa na mashiko kwa kuwa rais aliyekuwa madarakani alikuwa ni Mwislamu basi kama kufuata alipaswa kuwa mkristu kama ingekuwa ni mfumo wa CCM katika uchaguzi.Uchaguzi wa mwaka 1995 hata mimi na udogo wangu nilikuwa fans wa Kikwete.

Hivyo kusema Kikwete ndio alikuwa msindikizaji si kweli,na kwa kuwa mmoja kwa kujua mwezie ni charasmatic na kuwa anakubalika kwa Mwalimu Nyerere akaonekana aegemee kwa faida yake.

Hivi tuhuma za marehemu KM kuwa na Account ya mapesa nje,ilikuwa ni kipindi gani ni kabla ya uchaguzi au ni baada ya uchaguzi naomba msaada kujua hili.Manake nasikia mwalimu alijua uwepo wa mabilion ya pesa ambayo mdau huyo alikuwa amejikusanyia na kujiwekea kwenye account moja uko ulaya.

Uchaguzi wa 1995 Salim Ahmed Salim kama sikosei hakushiriki uchaguzi wa mwaka huo baada ya kuwa bussy zaidi na maswala ya kidiplomasia na kwa mtizamo wangu baada ya zengwe la HIZBU kwa upande wa Zanzabara zaid wakati huo 1985 kumkwaza na kitabia anaonekana Uwanadiplomasia umemkaa.Ni muumini wa stay aside and let nature take it cause.

Uchaguzi wa 2005,hapa ndipo kulifanyika vindumbwe ndumbwe kibao,manake kulikua na kambi kibao,Kuna kusanyiko la kambi nyingi na ambazo zingine ndio wahanga wa toka mwaka 1995. Mteule alisimama baada ya kuwa haikuwa hakuna namna yoyote ile kwa utashi wa Wananchi ambao walikuwa na historia yake toka huko nyuma ya mwaka 1995, ukiunganisha na kuwa charasmatic basi hata wale waliokusudia kumpiga chini ikawawia vigumu manake hofu ya mpasuko kama angeamua kuasi chama ikawa ni vigezo vya uteuzi.
 
Dogo kulikuwa na mtu alikuwa anaitwa Tuntemeke sanga huyu aliishia kwenye 5bora lakn huyu alikuwa na uwezo mkubwa kwani alikuwa anafanya maamuzi mazuri hata akiwa bungeni, lakini alikuwa haivi na nyerere hivyo akatoswa.
umenikumbusha mbali sana historia ya huyu Bwana ktk nchi hii
nakumbuka aliwahi kumwambia SPIKA by then alikuwa MSEKWA kuwa "huko kwenu hakuna wakubwa wa kuwa heshimu" hii ilikuwa pale alipo ambiwa muda wa kuchangia (dk 15) umeisha


huyu Bwana aliwa na degree 7 za masomo tofauti tofauti historia yake ni kubwa
 
... Cleopa Msuya alipopewa nafasi ya kutoa concession speech aliwaasa wana CCM waache siasa za "kuchimbana."
Kumbe kuna watu walishayaona haya yanayotiokea sasa hivi tangu zamani na kuonya!
 
Mkuu DSN au mkuu mwingine yoyote yule mnaweza mkatueleza zaidi kuhusu uhusiano wa JK na EL 1995?
 
Kilichojitokeza ni kwamba wale wafuasi wa Msuya walimwunga mkono Che Nkapa na wale Wazenj walikuwa wamepewa maelekezo na Komandoo Salimin (alikuwa bado anakipindi kimoja cha kukaa madarakani) kwamba wasithubutu kumchagua "Play Boy - Kikwete". Kwa hiyo hata Komandoo hakutaka kuwa chini ya Kikwete
 

Ilikuaje tena hapa mkuu? Maana mdau mwingine alisema kura za Zenji ndizo zilizo mfikisha JK tatu bora kwa sababu alisha wahi kufanya kazi huko kama mwanajeshi. Na kuna sababu zaidi za Salim kutomtaka JK au ni kwa sababu tu alikua "Play Boy".
 
kumbe Warioba hana merits za kuwa Rais,sikujua kuwa naye alishachukua fomu 1995.Kumbe angeweza pata favor ya Nyerere kama angekuwa competent kwa vile alifanya naye kazi kwa karibu,lakini badala yake Mkapa ndiye akaonekana anafaa
 
kinachoendelea leo ni dhambi ya kumnyima uongozi JK nchi isingefika katika hali hii tuliyonayo ss ya watu kujiuzia wao na kusahau ,mamilioni ya wenzao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…