MwanaFalsafa1,
..let my try my two cents.
..Prof.Malima alikuwa hayuko on the picture. Huyu alikuwa na matatizo makubwa na wafadhili walishashinikiza aondolewe kazini. Aliundiwa tume ya uchunguzi ilyoongozwa na Mohamed Aboud, ambaye alikuwa CAG.
..Salim Salim alikuwa awe mrithi wa Mwalimu tangu mwaka 1985 baada ya kuchukua nafasi ya Edward Sokoine[r.i.p]. Mchezo ulikuwa wawekwe Salim Salim na Mzee Mwinyi ambaye alikuwa ni Raisi wa Zanzibar kuanzia 83/84 baada ya Jumbe kutimuliwa. Inasemekana Seif na Salim walimshawishi Mzee Mwinyi amuachie nafasi hiyo Salim Salim kwa kisingizio kwamba yeye ndiyo kwanza ameshika madaraka makubwa Zanzibar. Mzee Mwinyi aliwageuka wenzake baada ya majina yao kufikishwa mbele ya Kamati Kuu ya CCM. Hiki ni kisa ambacho nadhani kipo ktk kitabu cha maisha ya Seif Sharrif Hamad.
..mwaka 1995 inasemekana Nyerere alimtaka tena Dr.Salim lakini this time akamkatilia kwasababu ilidhani itakuwa vigumu kwa Wazanzibar kushika nafasi ya Raisi wa Muungano kwa vipindi viwili. nadhani baada ya hapo ndiyo Nyerere akaona atupe karata yake kwa Mkapa.
..kwa kumbukumbu zangu walijitokeza wana CCM kama 15 hivi kutaka ridhaa ya chama chao. Ninaowakumbuka ni kama Balozi.Frederick Rutakyamirwa, Njelu Kasaka,Mark Bomani, Joseph Warioba,Pius Msekwa, Horace Kolimba, Benjamin Mkapa,Horace Kolimba,John Malecela, Cleopa Msuya,Jakaya Kikwete, Edward Lowassa,....
..nakumbuka Mkapa alichukua fomu ktk mazingira ambayo ilionekana kama hayuko serious na hana nguvu zozote zile. aliwaita waandishi wa habari ofisini kwake wizara ya sayansi na teknolojia na kwa kweli hata habari zilizoandikwa zilikuwa zinaonyesha kwamba hatafika mbali.
..Cleopa Msuya alichukua fomu nadhani wiki ya mwisho na hakukuwa na taarifa zozote zile. nadhani he did it on a weekend akiwa amekatisha ziara zake za kikazi.
..Edward Lowassa na Jakaya Kikwete walikodisha ndege pamoja kwenda Dodoma kuchukua fomu. waliporudi DSM kulikuwa na msisimko mkubwa kutokana na umaarufu aliokuwa nao Lowassa wakati huo. Kikwete yeye alikuwa anasema yuko pale kama kumuunga mkono kijana mwenzake.
..there are different versions of what transpired in the Kamati Kuu ikiwemo fununu kwamba Nyerere alitishia kurudisha kadi ikiwa Malecela asingeondoa jina lake, na pia kumpiga nyundo Lowassa kwamba alikuwa na utajiri usioeleweka. Nadhani in the end majina matatu ndiyo yalikwenda Halmashauri Kuu kupigiwa kura kupelekwa Mkutano Mkuu.
..kwa kumbukumbu zangu, ktk kura za Halmashauri Kuu, Cleopa Msuya alikuwa mshindi, which was a surprise, akifuatiwa na Jakaya Kikwete which was even a bigger surprise. Benjamin Mkapa alishika nafasi ya tatu. baada ya hapo kukawa na kipindi cha mpito kuelekea wa CCM na ikaonekana Kikwete alikuwa amekosewa. Kuanzia hapo nguvu za Cleopa Msuya zikaanza kufifia.
..katika kipindi cha kuelekea mkutano mkuu upinzani mkubwa, haswa magazetini, ulionekana kuwa kati ya JK na Msuya. magazeti mengi yalielekea kumkubali zaidi JK haswa kutokana na haiba yake ya ujana na kuwa askari mstaafu. Cleopa Msuya alionekana kupingwa zaidi kutokana na kashfa ya kusema "kila mtu atabeba msalaba wake." Msuya pia did not help himself kwasababu alikuwa anahimiza ukusanyaji kodi kipindi hicho akiwa Waziri Mkuu na kuna kipindi alifika Tabora na akalalamika kuhusu wananchi kutokuwa na moyo wa kulipa kodi ambayo yeye alikuwa anaona ni kidogo!! magazeti yalimshambulia sana kwa kauli yake hiyo. Msuya pia alikuwa anaonekana ndiye aliyeshinikiza Augustino Mrema atimuliwe kazi na Raisi Mwinyi.
..kampeni ya Mkapa ilionekana kuibuka kuziba vacuum iliyoachwa na kudorora kwa kampeni ya Msuya. Mkapa alionekana kuungwa mkono na kundi la wana CCM waadilifu waliokuwa wakipiga vita rushwa iliyokuwa imeshamiri wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi. Mkapa alikuwa anapigiwa kampeni kama mtu msafi mwenye nia na uwezo wa kupambana na rushwa.
..sikubahatika kusikia hotuba za wagombea Uraisi wakati wakiomba kura za wajumbe wa mkutano mkuu. nilisikiliza nasaha za Mzee Mwinyi na Mwalimu Nyerere kwa wajumbe wa mkutano mkuu kabla kura hazijapigwa. Mzee Mwinyi alitoa nasaha kwamba wajumbe wafuate kile ambacho wananchi wanataka kwa kumpigia kura mgombea aliyekuwa anasemwa vizuri na wananchi. kwa hotuba ile ilionekana kwamba Mzee Mwinyi alikuwa akimtaka Jakaya Kikwete. Ilipofika zamu ya Mwalimu yeye aliwaasa wajumbe wampigie kura mgombea anayeweza kupiga vita rushwa, ukabila, na udini. Wengi walitafsiri kwamba alikuwa akimtaka Benjamin Mkapa.
..raundi ya kwanza ya kura mshindi alikuwa Jakaya Kikwete, akifuatiwa na Ben Mkapa, na Msuya akashika mkia. Kura ziliporudiwa ilionekana kama kura zote za Msuya zimehamia kwa Mkapa na hivyo akatangazwa mshindi. There is an interesting sub plot baada ya Mkapa kutangazwa mshindi. Inasemekana kuna kundi la mashabiki wa Kikwete waliokuwa wakizomea ushindi wa Mkapa. Mwalimu alionyesha kufurahishwa mno na ushindi wa Mkapa. I dont remember his exact words. Cleopa Msuya alipopewa nafasi ya kutoa concession speech aliwaasa wana CCM waache siasa za "kuchimbana."