Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995?

Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995?

yes
kukata mzizi wa fitina naomba umpigie simu jenerali mwenyewe halafu
uje hapa useme ni nini umeambiwa huko.....

usisahau suala la kuchukua fomu ni mchakato..
sio mtu akiambiwa chukua fomu basi ndo kaambiwa unakuwa rais
nyerere actually alimwambia hata msekwa achukue fomu
na msekwa hakufika hata top three
Boss,
OK I take up your challenge. Lakini nikitoa ripoti hapa isiyokidhi kauli zako usiseme nimechakachua. My reputation is on the line here!
 
Miluzi mingi hupoteza mbwa. It is perplexing when everyone comes up with their pieces of information much to our confusion. So which remark should we take with as the discussion has turned pedantic and maddeningly misleading.
 
kwanini inasemwa kuwa Mkapa alibebwa 1995,kama katika raundi kwanza Kikwete hakufikisha 51% iliyohitajika kumfanya mshindi na katika raundi ya pili Mkapa alipata zaidi ya 51% na hivyo kuwa mshindi halali-kikatiba/sheria/kanuni/taratibu za kiccm?
 
Boss,
OK I take up your challenge. Lakini nikitoa ripoti hapa isiyokidhi kauli zako usiseme nimechakachua. My reputation is on the line here!

mkuu huyo jenerali hata mimi nina access nae nikitaka
wewe uwe mkweli na atakachokueleza tu
usije na uwongo tu hapa halafu nikaja na data mwishowe
 
Mkuu wewe ndio huelewi nachokizungumzia. Kote huku tumezunguka pasipo sababu kwa sababu ni wewe uliyesema habari za Udini na JK na kadhalika. Katika hali hiyo umeonyesha wazi haja ya waislaam kuwa na mgombea mwaka 1995, kama vile waislaam walikuwa desperate na uongozi sijui wa kupishana kiawamu..Huu ni upotoshaji wa makusudi kabisa kwani hatukuwa na kitu kama hicho hata kidogo..Hiki ndicho nilichokikataa kutoka statement yako ya kwanza na ndio nikalivuta jina la Salim na Malima kukuonyesha waislaam walikuwepo na wangeweza kugombea na wala halikuwa swala la dini..

Haikuwa sababu mwaka gani nani alichukua form bali kupinga dhana ya udini ambayo wewe unajaribu kuipandikiza..Tena basi ningependa sana labda ulijibu swali la Jasusi ambalo wewe umesema Nyerere alimwambia Jk achukue form kuwalikisha waislaam kisha JKN huyo huyo akamwambia hajakomaa kisiasa!..Mtu alomwambia achukue form kutetea wagombea wa kiislaam kisha akamwondoa mgombea huyo wa waislaam!.. huoni kama hii habari ni potovu!


wewe unachanganya watu humu
walikuwepo na wangeweza kugombea ni sawa na kugombea???????/
swali hapa ni waislamu wangapi walichukua fomu za kugombea urais mwaka 1995????/
jibu ni kikwete na malima tu
usilete habari za salim na wazanzibari,wakati mtu hakuchukua fomu
na alijibu ana kazi nyingi,na wewe article umeileta hapa,********???????
 
wewe unachanganya watu humu
walikuwepo na wangeweza kugombea ni sawa na kugombea???????/
swali hapa ni waislamu wangapi walichukua fomu za kugombea urais mwaka 1995????/
jibu ni kikwete na malima tu
usilete habari za salim na wazanzibari,wakati mtu hakuchukua fomu
na alijibu ana kazi nyingi,na wewe article umeileta hapa,********??????
Haya ndio haya ya Miafrika... Mkuu nachosema mimi napinga dhana yako ya kwamba Nyerere alimwambia JK achukue form kwa sababu hapakuwepo na waislaam. Kiingereza mkuu wangu hata ndoto zangu huota kwa kiingereza achana na kusoma hapa JF...

Huu ulouleta hapa ni uzushi ambao huwezi kuutolea ushahidi (proof), hivyo unadandia maandishi yangu bila wewe kutoa ukweli wa madai yako. Salim kachukua form ama hakuchukua sio swala ambalo lineweza kuwashtua CCM au Nyerere kufikia kumtafuta JK ati awakilishe waislaam.. Huu ni uongo pure mchezo wa kuigiza bob, kwa sababu haikuwa uchaguzi wa kumtafuta kiongozi muislaam au mkristu. Nimelitaja jina la Salim kukuonyesha kama alikuwa chaguo la mwalimu 1995 na alitaka achukue Urais sii kwa sababu ya dini yake bali Salim na CV yake...
 
Je kulikua na front runner kabla ya mkutano kuamua Mkapa awe mgombea? Yani hiyo 1995 kabla ya mchakato wa kutafuta mgombea kuanza kuna yoyote aliyekua anaonekana ndiyo ana nafasi kubwa ya kushinda? Je aligombea? Kama aligombea alishindwaje?
 
Haya ndio haya yaa Miafrika... Mkuu nachosema mimi napinga dhana yako ya kwamba Nyerere alimwambia JK achukue form kwa sababu hapakuwepo na waislaam. Huu ni uzushi ambao huwezi kuutolea ushahidi (proof), kachukua form ama hakuchukua sio swala mablo lineweza kuwashtua CCM au Nyerere kwa sababu haikuwa uchaguzi wa kumtafuta kiongozi musialaam au mkristu. Nimelitaja jina la Salim kukuonyesha kama ni chaguo la mwalimu ambaye alitaka achukue Urais na believr me hakuwa na sababu ya dini yake bali Salim na CV yake...


wewe unaongeza mambo na kupunguza
pale unapokosea huwezi hata kufanya ustaarabu wa kukiri umekosea

hebu kwanza kiri hapa hadharani kwamba maelezo yako mengi yana makosa
kuhusu uchaguzi wa 1995.....anza na hilo kwanza......

kuhusu nyerere kumwambia kikwete achukue fomu 1995
tumekubaliana humu kuwa jasusi atamtafuta jenerali athibitishe tusubiri hilo

but swala la kuwa kikwete achukue fomu kwa kuwa muislam
hukunielewa kabisa..........
so bora tuliache hilo kwanza,tusubiri jenerali athibitishe la nyerere na kikwete 1995
 
Je kulikua na front runner kabla ya mkutano kuamua Mkapa awe mgombea? Yani hiyo 1995 kabla ya mchakato wa kutafuta mgombea kuanza kuna yoyote aliyekua anaonekana ndiyo ana nafasi kubwa ya kushinda? Je aligombea? Kama aligombea alishindwaje?

front runner alikuwa malecela akifuatiwa ni kolimba
wao ndio walikuwa powerfull na wenye nguvu

but nyerere alikuwa tayari hawataki na kashawatungia kitabu
so uwanja ulikuwa wazi for anyone
 
front runner alikuwa malecela akifuatiwa ni kolimba
wao ndio walikuwa powerfull na wenye nguvu

but nyerere alikuwa tayari hawataki na kashawatungia kitabu
so uwanja ulikuwa wazi for anyone

Asante mkuu. Na je Mwinyi yeye alikua na mtu wake?
 
nini ilikuwa nafasi ya mrema laiti angebaki ccm? kungekuwa na posibillity ya yeye kufika top 3? maana japo alikuja fahamika baadae kuwa na madhaifu by then alikuwa ni kipenzi cha wananchi
 
nakumbuka, nyerere alitumia udikteta kumkataa malechela, inadaiwa alisema ALI( akiweka dharau kwa Rais Ally Hassan Mwinyi) kama jina la JOHN (akimaanisha john Malecel) lipo basi mimi narudisha kadi, hii ilikuwa ni dharau kwa rais halali aliyechaguliwa na wananchi

kwangu mimi, naamini nyerere aliingilia uhuru wa kufanya maamuzi wa wajumbe na alipindisha demokrasia , kwani hata huyo aliyekuwa akimtaka yeye bado alikuja kuwa rais bomu aliyeiuza nchi yetu
 
Miluzi mingi hupoteza mbwa. It is perplexing when everyone comes up with their pieces of information much to our confusion. So which remark should we take with as the discussion has turned pedantic and maddeningly misleading.

Tumia ubongo wako vizuri usitake spoon feeding kama mtoto wa darasa la kwanza kufudishwa hesabu kwa kutumia visoda.
 
nini ilikuwa nafasi ya mrema laiti angebaki ccm? kungekuwa na posibillity ya yeye kufika top 3? maana japo alikuja fahamika baadae kuwa na madhaifu by then alikuwa ni kipenzi cha wananchi

kabla ya kuelekea uchguzi mrema alishasoma mchezo
aliondolewa nafasi ya naibu waziri mkuu na akapelekwa wizara ya vijana
so alioondoka mapema kujaribu bahati yake kwingine
 
kabla ya kuelekea uchguzi mrema alishasoma mchezo
aliondolewa nafasi ya naibu waziri mkuu na akapelekwa wizara ya vijana
so alioondoka mapema kujaribu bahati yake kwingine

ni kweli aliondolewa unaibu waziri mkuu kwenda vijana na kazi, lakini je hiyo haikutokana na msuguano wake na rais mwinyi? nachoamini alikuwa amejipatia base ya wafuasi kama ambaavyo jk alijiamini 2005 kiasi alitaka kwenda chadema akijua ana kundi la wafuasi
laiti, nyerere asingeingilia kampeni za 1995, sina picha tungekuwa nchi ya aina gani kwa sasa, maana naamini ccm wangeshindwa uchaguzi
 
nakumbuka, nyerere alitumia udikteta kumkataa malechela, inadaiwa alisema ALI( akiweka dharau kwa Rais Ally Hassan Mwinyi) kama jina la JOHN (akimaanisha john Malecel) lipo basi mimi narudisha kadi, hii ilikuwa ni dharau kwa rais halali aliyechaguliwa na wananchi

kwangu mimi, naamini nyerere aliingilia uhuru wa kufanya maamuzi wa wajumbe na alipindisha demokrasia , kwani hata huyo aliyekuwa akimtaka yeye bado alikuja kuwa rais bomu aliyeiuza nchi yetu

nyerere alikuwa na staili hiyo ya kuwaita watu kwa majina yao ya kwanza
hata kawawa alikuwa anamuita tu rashidi....
 
MwanaFalsafa1,

..let my try my two cents.

..Prof.Malima alikuwa hayuko on the picture. Huyu alikuwa na matatizo makubwa na wafadhili walishashinikiza aondolewe kazini. Aliundiwa tume ya uchunguzi ilyoongozwa na Mohamed Aboud, ambaye alikuwa CAG.

..Salim Salim alikuwa awe mrithi wa Mwalimu tangu mwaka 1985 baada ya kuchukua nafasi ya Edward Sokoine[r.i.p]. Mchezo ulikuwa wawekwe Salim Salim na Mzee Mwinyi ambaye alikuwa ni Raisi wa Zanzibar kuanzia 83/84 baada ya Jumbe kutimuliwa. Inasemekana Seif na Salim walimshawishi Mzee Mwinyi amuachie nafasi hiyo Salim Salim kwa kisingizio kwamba yeye ndiyo kwanza ameshika madaraka makubwa Zanzibar. Mzee Mwinyi aliwageuka wenzake baada ya majina yao kufikishwa mbele ya Kamati Kuu ya CCM. Hiki ni kisa ambacho nadhani kipo ktk kitabu cha maisha ya Seif Sharrif Hamad.

..mwaka 1995 inasemekana Nyerere alimtaka tena Dr.Salim lakini this time akamkatilia kwasababu ilidhani itakuwa vigumu kwa Wazanzibar kushika nafasi ya Raisi wa Muungano kwa vipindi viwili. nadhani baada ya hapo ndiyo Nyerere akaona atupe karata yake kwa Mkapa.

..kwa kumbukumbu zangu walijitokeza wana CCM kama 15 hivi kutaka ridhaa ya chama chao. Ninaowakumbuka ni kama Balozi.Frederick Rutakyamirwa, Njelu Kasaka,Mark Bomani, Joseph Warioba,Pius Msekwa, Horace Kolimba, Benjamin Mkapa,Horace Kolimba,John Malecela, Cleopa Msuya,Jakaya Kikwete, Edward Lowassa,....

..nakumbuka Mkapa alichukua fomu ktk mazingira ambayo ilionekana kama hayuko serious na hana nguvu zozote zile. aliwaita waandishi wa habari ofisini kwake wizara ya sayansi na teknolojia na kwa kweli hata habari zilizoandikwa zilikuwa zinaonyesha kwamba hatafika mbali.

..Cleopa Msuya alichukua fomu nadhani wiki ya mwisho na hakukuwa na taarifa zozote zile. nadhani he did it on a weekend akiwa amekatisha ziara zake za kikazi.

..Edward Lowassa na Jakaya Kikwete walikodisha ndege pamoja kwenda Dodoma kuchukua fomu. waliporudi DSM kulikuwa na msisimko mkubwa kutokana na umaarufu aliokuwa nao Lowassa wakati huo. Kikwete yeye alikuwa anasema yuko pale kama kumuunga mkono kijana mwenzake.

..there are different versions of what transpired in the Kamati Kuu ikiwemo fununu kwamba Nyerere alitishia kurudisha kadi ikiwa Malecela asingeondoa jina lake, na pia kumpiga nyundo Lowassa kwamba alikuwa na utajiri usioeleweka. Nadhani in the end majina matatu ndiyo yalikwenda Halmashauri Kuu kupigiwa kura kupelekwa Mkutano Mkuu.

..kwa kumbukumbu zangu, ktk kura za Halmashauri Kuu, Cleopa Msuya alikuwa mshindi, which was a surprise, akifuatiwa na Jakaya Kikwete which was even a bigger surprise. Benjamin Mkapa alishika nafasi ya tatu. baada ya hapo kukawa na kipindi cha mpito kuelekea wa CCM na ikaonekana Kikwete alikuwa amekosewa. Kuanzia hapo nguvu za Cleopa Msuya zikaanza kufifia.

..katika kipindi cha kuelekea mkutano mkuu upinzani mkubwa, haswa magazetini, ulionekana kuwa kati ya JK na Msuya. magazeti mengi yalielekea kumkubali zaidi JK haswa kutokana na haiba yake ya ujana na kuwa askari mstaafu. Cleopa Msuya alionekana kupingwa zaidi kutokana na kashfa ya kusema "kila mtu atabeba msalaba wake." Msuya pia did not help himself kwasababu alikuwa anahimiza ukusanyaji kodi kipindi hicho akiwa Waziri Mkuu na kuna kipindi alifika Tabora na akalalamika kuhusu wananchi kutokuwa na moyo wa kulipa kodi ambayo yeye alikuwa anaona ni kidogo!! magazeti yalimshambulia sana kwa kauli yake hiyo. Msuya pia alikuwa anaonekana ndiye aliyeshinikiza Augustino Mrema atimuliwe kazi na Raisi Mwinyi.

..kampeni ya Mkapa ilionekana kuibuka kuziba vacuum iliyoachwa na kudorora kwa kampeni ya Msuya. Mkapa alionekana kuungwa mkono na kundi la wana CCM waadilifu waliokuwa wakipiga vita rushwa iliyokuwa imeshamiri wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi. Mkapa alikuwa anapigiwa kampeni kama mtu msafi mwenye nia na uwezo wa kupambana na rushwa.

..sikubahatika kusikia hotuba za wagombea Uraisi wakati wakiomba kura za wajumbe wa mkutano mkuu. nilisikiliza nasaha za Mzee Mwinyi na Mwalimu Nyerere kwa wajumbe wa mkutano mkuu kabla kura hazijapigwa. Mzee Mwinyi alitoa nasaha kwamba wajumbe wafuate kile ambacho wananchi wanataka kwa kumpigia kura mgombea aliyekuwa anasemwa vizuri na wananchi. kwa hotuba ile ilionekana kwamba Mzee Mwinyi alikuwa akimtaka Jakaya Kikwete. Ilipofika zamu ya Mwalimu yeye aliwaasa wajumbe wampigie kura mgombea anayeweza kupiga vita rushwa, ukabila, na udini. Wengi walitafsiri kwamba alikuwa akimtaka Benjamin Mkapa.

..raundi ya kwanza ya kura mshindi alikuwa Jakaya Kikwete, akifuatiwa na Ben Mkapa, na Msuya akashika mkia. Kura ziliporudiwa ilionekana kama kura zote za Msuya zimehamia kwa Mkapa na hivyo akatangazwa mshindi. There is an interesting sub plot baada ya Mkapa kutangazwa mshindi. Inasemekana kuna kundi la mashabiki wa Kikwete waliokuwa wakizomea ushindi wa Mkapa. Mwalimu alionyesha kufurahishwa mno na ushindi wa Mkapa. I dont remember his exact words. Cleopa Msuya alipopewa nafasi ya kutoa concession speech aliwaasa wana CCM waache siasa za "kuchimbana."
 
joka kuu naomba utzame facts zako upya

kighoma malima alichukua fomu za uraisi pia.....
hata kama hakufika mbali.but alichukua fomu
 
The Boss,

..Kighoma Malima stood no chance ya kupewa nafasi na CCM.

..Mabalozi walikuwa wanashinikiza afukuzwe kazi baada ya kuonekana serikali haikusanyi kodi.
 
Back
Top Bottom