Nami nichangie kidogo. Mwaka huo pia alikuwepo mwana mama aliyechukua fomu, naye alikuwa ni Bi. Rose Lugendo. Ila alipata wakati mgumu alipoingia kwa usaili mbele ya Nyerere.
Kama alivyosema Mkandala, Nyerere alimuomba Dk. Salim aje agombee, wakati huo Salim alikuwa Katibu Mkuu wa OAU. Salim alikubali na kuja Tanzania. Lakini jungu lilianzishwa na Mama Getrude Mongella kuwa nchi hii haiwezi kutawaliwa na Mwarabu. Na hili alilizungumza mpaka kwa Nyerere, akiungana na baadhi ya watu mashuhuri wa CCM toka Bara na waliowengi toka Visiwani. Salim ikabidi asichukue fomu na kurudi Addis Ababa.
Kuhusu Malima, alipoenguliwa CCM alihamia NRA (National Reconstructive Alliance), habari za kujitoa CCM zilisikika kwa Nyerere. Aliitwa na Nyerere na aliombwa kuwa kujitoa kwake CCM kunaweza kukitingisha chama (kumbuka alikuwa nguzo muhimu wakati wa kupigania uhuru). Alikataa na akapanga kujitoa CCM akiwa Tabora, alikata tiketi ya ATC, na alipofika Airport, akaambiwa ndege imejaa, ikabidi asafiri na gari lake hadi Tabora. Akajitoa CCM na kujiunga na NRA, na kubadilisha kifupi cha jina la chama toka NRA kuwa NAREA. Alifariki katika mzingira ya kutatanisha London kabla ya uchaguzi.