Tony254, ina maana discussion nzima hii hujaelewa wanacholalamikia wakenya wenzako?, uzuri ni kwamba wote wamekubaliana wanazungumza na kulalamikia shida ya nchi yenu.
Siamini kwamba wote hawa ni kabila moja, au wametoka sehemu moja, au ni chama kimoja cha siasa, mambo ambayo yanawafanya kuwa "biased" sana wakati mnapozungumza kuhusu changamoto za nchi yenu.
Ni Mara chache sana kuwaona wakenya kutoka makabila tofauti na vyama tofauti kuungana na kuzungumza lugha moja, hasa katika kuikosoa Serikali, ukiona jambo kama hili linaanza kutokea, jua wazi kunakaribia kupambazuka.
Msikilize mzungumzaji wa kwanza, mzungumzaji wa tatu(Mwanamke), na huyo wa mwisho kwa umakini sana, kamwe hawalaumu PPP, ninakushangaa ukitaka kukwepesha na kuharibu maudhui mazima ya huu mjadala na kukimbilia "None issue" ya PPP.