Kaka ni upofu wa mawazo na kutojua uchumi vizuri ndiko kunakomfanya asifie mishahara mikubwa ya Kenya, 52% ya bajeti yote ya Kenya kwa mwaka inaishia kulipa mishara kwa watumishi wa uma, ambao ni asilimia 2% tu ya wakenya wote, ni 27% pekee ya bajeti ndiyo inayoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo, wakati Tanzania 40% enaenda kwenye miradi ya maendeleo, mishahara yao haina usawa wowote, wanasiasa wanalipwa mara kumi zaidi ya professionals, matokeo yake ni
1)Malalamiko yasiokwisha miongoni mwa watumishi wa umma
2)Migomo ya kutoridhishwa na mishahara, kwa sababu wasomi wanajilinganisha na wanasiasa
3)Rushwa isiyokwisha, kila mtu anataka kulingana na wanasias
4)Mfumuko wa bei kuwa juu muda mwingi, kwa sababu ya mzunguko mkubwa wa pesa usiotokana wala kuendana na ongezeko la uzalishaji
5)Huduma za jamii kuwa duni kwa kukosa pesa, pesa nyingi inatumika kulipa mishahara
6) Kuongezeka kwa gap kati ya tajiri na masikini