Huwa mara nyingi ninauliza kuhusu uwezo wako wa kuelewa mambo, mwanzoni nilidhani kwamba ulikua kidogo upo vizuri ukilinganisha na wakenya wengine, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda, ndiyo ninagundua kwamba ni huna tofauti na wakenya wengine.
Tatizo ni kwamba ninyi wakenya hamfikirii nje ya box, unadhani kinachofanyika Kenya ni unique, mfano mzuri ni jinsi mlivyoshangilia pale mlipofanya operation ya kutenganisha wale mapacha, wengi walisema hii ni operation ya kwanza in east and central africa, sisi tulikua tunacheka sana, Tanzania kuanzia 1994 tulianza kuzifanya hizo operations, wala hujasikia kelele kama ninyi washamba.
Turudi kwenye hili la bima ya afya, katika jibu langu nilianza kwa kusema"hata huku ni hivyo hivyo ", nikimaanisha kuhusu bima ya afya, ukiwa na NHIF unaweza kwenda kutibiwa Hospital yoyote ile, wewe uwa unakuja Tanzania, kwanini usijielimishe juu ya mambo haya?. Je ni asilimia ngapi ya wakenya wenye bima ya afya, na wale wasiokuwa na bima.za afya wanatibiwa wapi?, hapo ndiyo tunapowazidi, kwa sababu bado sehemu kubwa ya wananchi hawajajiunga katika mpango wa NHIF, serikali inapaswa kuhakikisha public hospitals zina ubora wa hali ya juu ili kuhakikisha wananchi hao wanafaidika, huko kwenu ni "man eat man society", masikini hana thamani.